Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Friday, February 6, 2015

KUKUBALI MPENZI WAKO ‘AKUCHUNE’ SIYO UBWEGE!

Mpenzi msomaji, wapenzi wako wa aina tofauti. Kuna wale ambao mwanamke anafanya kazi mwanaume hana kazi, mwanaume ana kazi na mwanamke hana kazi ama wote wanafanya kazi.
Katika mazingira hayo, fahamu kwamba mpenzi wako ana haki ya kukuchuna kimtindo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha shida ndogondogo hazimtesi.


Hutakiwi kuwa mbahili hata kidogo na unachotakiwa kufanya ni kumpatiliza katika mahitaji yake muhimu pale atakapohitaji.

Hapa sizungumzii kwamba mwanaume ndiye anayetakiwa kumfanyia hayo mpenzi wake bali hata mwanamke pia anatakiwa kumfanyia mambo fulani mpenzi wake kwa kutumia kipato chake.
Kuna baadhi ya wanawake wao siku zote ni watu wa kuwachuna tu wapenzi wao licha ya kwamba wao pia wana vipato vyao.

Si wanawake tu bali pia kuna hata wanaume ambao ubahili wao umezidi kipimo kiasi kwamba hawezi kuwapa wapenzi wao nafasi za kuwachuna. Unamkuta mwanaume anafanya kazi na anapata mshahara mnono tu lakini mpenzi wake akimgusia tu kuwa ana shida na kiasi f’lani cha pesa, anakuwa mgumu.

Ni kweli mapenzi na pesa ni vitu viwili tofauti lakini mpenzi wako akikulilia shida kama unao uwezo msaidie. Hivi unadhani kama usipomsaidia wewe nani amsadie? Au unataka atafute mwanaume mwingine wa kumchuna?

Ninachoona hapa ni baadhi ya wanaume kuhisi kwamba kuwasaidia wapenzi wao pale wanapolia shida ni sawa na kukubali kugeuzwa mabuzi wa kuchunwa.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG