Michezo
ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, UEFA ilianza kutimua tena vumbi
Jumanne usiku kwa michezo miwili katika hatua ya kumi na sita bora.
Paris
Saint Germain ya Ufaransa iliwaalika Chelsea ya England, huku Bayern
Munich ya Ujerumani wakiwa wageni wa Shaktar Donetsk ya Ukraine. Matokeo
ni kwamba PSG na Chelsea zimemaliza dakika tisini za mchezo kwa
kufungana bao 1-1.
Chelsea
ndio waliokuwa wa kwanza kutikisa nyavu za wenyeji wao katika dakika ya
36, bao likifungwa na Branislav Ivanovic na kudumu hadi mapumziko. PSG
waliendeleza mashambulizi huku kiungo wake David Luiz akiwadhibiti
wachezaji wa timu yake ya zamani, Chelsea. Kwa David Luiz kutawala
sehemu ya kiungo, mshambuliaji Matuidi wa PSG alikuwa akitamba na
kuelekeza mashambulizi makali langoni mwa Chelsea na kumfanya mlinda
mlango wake Curtois kuokoa michomo mingi. Katika dakika ya 54 ya mchezo,
Edinson Cavani aliisawazishia timu yake bao na hivyo hadi mwamuzi
anapuliza filimbi yake ya mwisho, timu hizo zilitoka sare ya bao1-1.
Bayern
Munich ya Ujerumani katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora
walipomenyana na Shakhtar Donetsk na kutoka sare ya 0-0Nayo Bayern
Munich ya Ujerumani ilishuhudia ikitoka sare ya kutofungana na Shakhtar
Donetsk ya Ukraine.
Bayern Munich ilipata pigo kwa mchezaji wake Xabi Alonso kuzawadiwa kadi nyekundu katika mchezo uliojaa ubabe.
Jumatano
usiku, Real Madrid ya Hispania watakuwa wageni wa Schalke 04 ya
Ujerumani katika mchezo mwingine wa klabu bingwa, huku Basel ya Uswis
ikiikaribisha FC Porto ya Ureno.
Mechi za hatua ya kumi na sita bora zitakamilika Machi 18, ambapo michezo miwili miwili itakuwa ikifanyika Jumanne na Jumatano.
Timu
nyingine katika hatua hii ni Juventus ya Italia itakayopambana na
Borussia Dortmund ya Ujerumani, Manchester City ya England itavaana na
Barcelona ya Hispania, mechi zitakazochezwa usiku wa tarehe 24 Februari
na kesho yake yaani tarehe 25 Februari Arsenal ya England itakuwa
ikipimana misuli na Monaco ya Ufaransa, huku Bayern Levkusen ya
Ujerumani wakiwa wenyeji wa Atletico Madrid ya Hispania.CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment