Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Monday, February 16, 2015

Rais El-Sisi asema Misri itajibu mapigo

Rais Abdel Fattah el-Sisi wa Misri
Rais wa Misri amesema nchi yake ina haki ya kujibu mashambulio kwa namna yoyote ile inayoona inafaa katika kulipiza kisasi cha mauaji ya kundi la Wakristo wa madhehebu ya Coptic yaliyofanywa na kikundi cha wapiganaji wa jihad nchini Libya wenye uhusiano na kikundi cha Islamic State.
Rais Abdel Fattah al-Sisi ametoa kauli yake kupitia televisheni ya taifa baada yavideo moja kuonyesha mateka wapatao kumi wa kundi la waumini wa madhehebu ya Coptic kukatwa vichwa.
Waumini ishirini na mmoja wa madhehebu ya Coptic nchini Misri walitekwa nchini Libya wiki kadhaa zilizopita. Maandishi yaliyowekwa katika video hiyo yanaonyesha walilengwa kwa sababu ya dini yao. Misri imetangaza wiki moja ya maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo vya watu hao.
Mamlaka ya Kiislam inayoongoza nchini Misri,-- Al Azhar -- imeshutumu mauaji hayo na kuyaita ni ya "kinyama". Maelfu ya Wamisri wamekuwa wakivuka mpaka kwenda kutafuta kazi nchini Libya licha ya ushauri wa serikali yao ya Misri kuwakataza wasiende huko.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG