Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Monday, February 16, 2015

Mapigano yasita kwa jumla Ukraine

Mpiganaji anayeipendelea Urusi karibu na Debalseve
Viongozi wa Ufaransa na Ujerumani wamesema wameridhika na namna makubaliano ya kusitisha mapigano yanavyofuatwa kwa jumla masharikimwa Ukraine.
Walioshuhudia matukio huko wanasema katika maeneo mengi kuna utulivu, ingawa ni utulivu wa wasiwasi, isipokuwa katika eneo la mji wa Debaltseve ambako wapiganaji wanaoipendelea Urusi wameendelea kuwashambulia wanajeshi wa serikali ambao wamewazingira katika mji huo muhimu kwa usafiri.
Hata katika eneo hilo, mapigano siyo makali kama yalivyokuwa.
Shirika la usalama la Ulaya, OSCE, linasema kuwa wapiganaji wamekataa kuruhusu wachunguzi wa OSCE kuingia katika maeneo yao.
Shirika hilo piya linasema makubaliano ya kusitisha mapigano yanafuatwa.
Hatua ya pili ya kurejesha amani ni kwa pande zote mbili kuondosha silaha nzito kwenye mpaka wa mapigano hapo Jumane.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG