Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Monday, February 16, 2015

Utaliana yafunga Ubalozi Libya

Ubalozi wa Ufaransa mjini Tripoli ulioshambuliwa mwaka 2013
Ubalozi wa Utaliana mjini Tripoli, Libya, umefungwa na wafanyakazi wake kurejeshwa nyumbani kwa sababu za usalama.
Wizara ya mashauri ya nchi za nje mjiniRome imesema hoteli ambamo wafanyakazi hao wa ubalozi wakiishi, siyo salama tena.
Utaliana ndiyo nchi pekee ya Ulaya iliyokuwa imebaki na ubalozi mjini Tripoli, lakini kuna wasiwasi kuwa wapiganaji Waislamu wa siasa kali watailenga ofisi hiyo.
Mapambano baina ya jeshi la serikali na wapiganaji Waislamu yamekuwa yakiendelea tangu Kanali Gaddafi kupinduliwa; na waziri wa ulinzi wa Utaliana,Roberta Pinotti, amesema nchi yake iko tayari kushiriki kwenye hatua za kijeshi dhidi ya wapiganaji hao.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG