Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Thursday, February 19, 2015

WHO watoa ripoti mpya kuhusu Ebola

  • Share on facebook Share on google_plusone_share Share on twitter Share on linkedin

Shirika la Afya Duniani, WHO limetoa takwimu mpya kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
Takwimu hizo zinazihusu nchi za Sierra Leone, Guinea na Liberia tu ambapo taarifa zinasema kumekuwa na wagonjwa 23 218 na vifo 9365.
Mchanganuo wa takwimu hizo unaonyesha kuwa Sierra Leone imekuwa na wagonjwa 11 103, na vifo vya watu 3408, Liberia - wagonjwa 9007, vifo 3900 na Guinea - wagonjwa 3108 na vifo vya watu 2057.
Takwimu hizo ni mpaka tarehe 15 Februari kwa nchi za Sierra Leone na Guinea, na Liberia ni mpaka tarehe 12 Februari.
Pia Uingereza ilikuwa na mgonjwa mmoja bila kifo
Takwimu kwa ajili ya Senegal, Nigeria, Hispania, Marekani na Mali zimeondolewa.Nchi hizo haziko katika karantini ya ugonjwa wa Ebola.CHANZO:BBC

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG