Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Sunday, March 1, 2015

Manchester United yawika

Wayne Rooney
Mkwaju wa penalti uliofungwa na nahodha Wayne Rooney uliisaidiaManchester United kuichapa Sunderland mabao 2-0 baada ya West Brown kupewa kadi nyekundu katika kile kilichoonekana kama maonevu.
Rooney alifunga baada ya mshambuliaji Radamel Falcao kuchezewa visivyo na kusababisha kutolewa kwa Wes Brown badala ya John Oshea aliyecheza vibaya licha ya pingamizi kutoka kwa mashabiki.
Manchester united iliongeza bao la pili baada ya Rooney kufunga kupitia kichwa baada ya mkwaju wa Adnan Januzaj kupanguliwa na kipa.
Ushindi huo umeimarisha harakati za kilabu hiyo kuwania nafasi nne bora katika ligi hiyo.
Matokeo mengine:
West Ham 1 - 3 Crystal Palace
Burnley 0 - 1 swansea
Newcastle 1 - 0 Aston Villa
Stoke 1 - 0 Hull
West Brom 1 - 0 Southampton

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG