- Written by Tupambane Blog
- Tuma Maoni
-
Share on facebook Share on google_plusone_share Share on twitter
Ole Sosopi katika moja yab mikutano yake
Mjasili haachi asiliye Ole Sosopi akipandisha mori kijijini kwao
Na Mathias Canal, Kwanza jamii-Iringa
Anaitwa Patrick Ole Sosopi, Ni mmasai aliyezaliwa na kukulia mkoa Iringa, jimbo la Ismani.
Ana umri
wa miaka 28. Ni msomi wa shahada ya kwanza ya Biashara na utawala
(rasilimali watu) kutoka chuo kikuu cha Ruaha (RUCO). Kwa sasa kazi zake
ni kufuga ng'ombe. Ni Baba wa mke mmoja na mtoto mmoja.
Ni
mgombea wa nafasi ya umakamu mwenyekiti wa BAVICHA Bara- Taifa.Historia
yake ya uongozi na uadilifu wake umekuwa hauna shaka katika vipindi
mbalimbali vya maisha yake.
Historia
yake ya uongozi ilianzia akiwa shule ya msingi, sekondari hadi chuo
kikuu cha RUCO ambapo alikuwa waziri wa Fedha kwenye serikali ya
wanafunzi 2011/2012.
Alijiunga
rasmi na CHADEMA mwaka 2009 alipokuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza
akiamini ni chama pekee ambacho kina tija ya kuboresha maisha ya jamii
yake ya kimasai na changamoto mbalimbali ambazo zilikuwa zikiwakabili.
Ole
Sosopi ni mojawapo wa waanzilishi wa CHASO mkoani Iringa, harakati zake
katika jimbo la Ismani na mkoa wa Iringa kwa ujumla kila mtu anazijua.
Ameshiriki katika mchakato wa ujenzi wa chama kwenye wilaya zote za mkoa
wa Iringa pamoja na Mbeya.
Wakati Daudi Mwangosi akiuliwa kikatili na jeshi la Polisi alikuwa umbali tu wa mita kumi akishuhudia.
Aliaminiwa
na vijana wa Ismani na kupata kura zote bila kupingwa na kuwa
Mwenyekiti wa BAVICHA jimbo la Ismani. Baada ya kushauriwa na
kushauriana na familia yake na vijana mbambali kutoka sehemu mbalimbali
za Tanzania, ameona agombee nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa BAVICHA
Bara.
Ingawa ni
mojawapo wa wasomi wachache kwenye jamii ya yao, ni mtu ambaye usomi
wake haujamfanya asahau mila na tamaduni za nkimasai. Chakula chake,
mavazi yake, desturi yake ya maisha ya kila siku ni desturi za kwao na
zenye kuhuwisha Utanzania.
No comments:
Post a Comment