- Written by Tupambane Blog
-
Share on facebook Share on gmail Share on twitter
Na Beatrice Lyimo, Maelezo-DSM
WAZIRI wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi katika Harambee ya kuchangia kuchangia ujenzi wa nyumba za
walimu vyumba vya madarasa na ununuzi wa samani katika shule ya
Sekondari ya Enaboishu iliyopo mkoani Arusha.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi wa shule hiyo, Bw. Emmanuel Munga leo jijini Dar Es Salaam.
Munga
amesema kuwa Harambee hiyo inatarajiwa kufanyika siku ya tarehe 25
Oktoba mwaka huu katika shule hiyo wilayani Aremure mkoani Arusha ambapo
Kauli mbiu ya harambee hiyo ni 'penye nia pana njia'.
Alisema
kuwa, katika harambee hiyo wamewashirikisha wanafunzi wote waliosoma
katika shule hiyo wakiwemo wazazi, viongozi mbali mbali wa Serikali,
Vyama vya siasa, Mashirika yasiyo ya kiserikali, wadau, shule za jirani
na wananchi kwa ujumla.
"katika
harambee hii tunatarajia kukusanya zaidi ya shilingi milioni 200 na
fedha zitakazopatikana zitatumika kutatua changamoto zinazozikabili
shule", alisisitiza Munga.
Akizungumzia
kuhusu changamoto zinazoikabili shule hiyo alisema kuwa, shule hiyo
yenye mchanganyiko wa wanafunzi wa kike na wakiume iliyoanza mwaka 1966
inakabiliwa na changamoto za nyumba za walimu, nyumba za madarasa,
mabweni ya wanafunzi na maabara.
Ameongeza
kuwa shule hiyo imetoa baadhi ya viongozi wakubwa waliopo serikalini
wakiwemo Naibu Waziri wa Tamisemi Mhe. Agrey Mwanri na Naibu Katibu wa
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole
Gabriel
No comments:
Post a Comment