- Written by Tumbane Blog
-
Share on facebook Share on gmail Share on twitter
Na Anita Jonas-MAELEZO
Umoja wa
Mataifa umeshauri kuchukua hatua za haraka kwa magongwa ya mlipuko
yanayotokea Afrika kama Ebola kwani yanadhiri uchumi wa mataifa husika.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna
Tibaijuka wakati wa Maadhimisho ya Miaka 69 ya Umoja wa Kimataifa leo
Jijini Dar es Salaam.(Thommy kundy)
Prof.
Tibaijuka alisema kuwa Umoja wa Mataifa wanatakiwa kuchukua tahadhari ya
milipuko ya magonjwa hatarishi na kuyachukulia kama ni magonjwa ya
Kidunia kwani yanaathiri mifumo yote ya kimaendeleo.
"Mataifa
yaliyoendelea yasingepuuzia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ulipojitokeza
Afrika hali isingekuwa hatarishi kama ilivyo sasa, hivyo ni rai yangu
kwa Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na mataifa husika kuchukua
tahadhari wakati wote "Alisema Prof. Tibaijuka.
Aidha,
Prof. Tibaijuka alisema kuwa kutokana na tatizo la mabadiliko ya tabia
nchi kuwa tishio miongoni mwa wengi duniani, wahisani wa maendeleo
hawanabudi kusaidia Mataifa mengine ikiwamo utekelezaji wa Mfuko wa
Kijani wa Hali ya hewa.
Akizungumzia
kuhusu hatua ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete kutoa uraia kwa wakimbizi
162,000 kutoka Burundi, Prof. Tibaijuka alisema kuwa Tanzania imeonyesha
ulimwengu kuwa suala la mapambano dhidi ya ukimbizi linaweza kufanyiwa
kazi na kuwafanya wakimbizi kuishi maisha kama binadamu wengine.
Naye
Mratibu muwakilishi wa makazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) Bw. Alvaro Rodriguez alisema kuwa shirika hilo kwa
kushirikiana na serikali na wadau wengine, wamepanga kusaidia na
kuboresha miundombinu ya kiusalama ili kuendeleza amani Duniani kwani
bila amani maendeleo ni vigumu kupatikana.
Pia Bw.
Rodriguez aliipongeza Tanzania katika kutekeleza Malengo ya Millenia
katika sekta ya afya kwa ambapo asilimia 96 ya vituo vyote vya afya
nchini vinatoa huduma ya afya ya uzazi kwa mama na mtoto.
Sherehe hizo zimebebwa na kauli mbiu ya "Leave no One Behind" ikiwa na mlengo wa kuleta maendeleo yenye usawa duniani.
No comments:
Post a Comment