- Written by Tupambane Blog
-
Share on facebook Share on gmail Share on twitter
Bondia
Ally Bugingo akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Amani Bariki
'Manny Chuga' mpambano utakaofanyika Oktoba 25 katika ukumbi wa Frends
corner Manzese Dar es salaam katikati ni Antony Rutta picha na Tupambane blog
Bondia Sadiki Nuru akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa kesho jumamosi
Bondia
Said Mbelwa akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake utakaofanyika kesho
oktoba 25 katika ukumbi wa frends corner manzese ambapo anapambana na
George Dimoso mpambano wa raundi nane picha na
Bondia
Fadhili Boika kushoto akitunishiana misuli na Robinson Msimbe baada ya
kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utajkaofanyika jumamosi ya oktoba
25 katika ukumbi wa Frends Corne Manzese Dar es salaam picha na Tupambane blog
MPAMBANO wa mchezo wa masumbwi mkali utakaokutanisha mabondia mbalimbali kutoka kila kona ya Tanzania utafanyika
Jumamosi
ya October 25 katika ukumbi wa friends Corner manzese jijini Dar es
salaam akizingumza na waandishi wa habari mratibu wa mpambano huo kocha
wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
amesema
kuwa siku hiyo kutakuwa na mpambano wa mahasimu katika mchezo wa ngumi
kati ya bondia Saidi Mbelwa 'Moto wa Gesi' na George Dimos mpambano
mwingine utawakutanisha Amani Bariki 'Manny Chuga' na Ally Bugingo
mpambano unaosubiliwa kwa hamu kila kona ya jiji la Dar es salaam ambapo
mabondia hawo wamejizolea umaarufu mkubwa kupitia mchezo huo
pambano
jingine ni kati ya Juma Fundi atakaezichapa na Hamza Mchanjo wakati
Hasani Mandula ataonyeshana kazi na Mohamedi Jaka na Shabani Kaoneka
atazipiga na Ibrahimu Maokola anaejiandaa kuwania kucheza ubingwa wa
taifa mwishoni mwa mwaka huu Fadhili Boika atazipiga na Godfrey Silver
na Habibu Pengo atazidunda na Abdallah Luanje, Kashinde Mohamedi
atazidunda na Mohamed Kibaga wakati Sadiki Nuru atakumbana na Mohamed
Mbishi
katika
mpambano huo siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha kabisa kutokana na
kujipanga vizuri katika swala hilo kingilio ni shilingi, 5000; kwa kila
mtu mchezo huu utapambwa na burudani mbalimbali

siku hiyo
pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo
mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua
mpaka kujua kitu kamili katika mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd
Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani
No comments:
Post a Comment