Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA
Showing posts with label ndondi. Show all posts
Showing posts with label ndondi. Show all posts

Thursday, July 28, 2016

MAPAMBANO YA NGUMI SASA KURUSHWA LIVE NA STAR TV

index
Mkuu wa vipindi wa Star TV, Yusuph Kamote kushoto  akibadilishana mkataba na Jay Msangi mara baada ya kusainiwa jijini leo. Akishuhudia tukio hilo ni Chief Kiumbe
 Na Mwandishi wetu
Kituo cha Televisheni cha  Star Tv  kimeingia makubaliano na kampuni ya Hall of Fame kwa ajili ya kurusha moja kwa moja ‘live’ mapambano sita ya ngumi za kulipwa nchini kuanzia mwezi ujao.
Hatua hiyo ina lengo la kuendeleza mchezo huo ambao ni wa pili kwa kupendwa nchii kwa mujibu wa Mkuu wa Program wa Star Tv Dar es Salaam, Yusuph Kamote.
Kamote alisema kuwa kwa kupigia kituo chao ambacho kina masafa marefu na kupatikana hadi maeneo ya vijijini,  mashabiki wa ngumi za kulipwa watapata fursa ya kujionea ‘live’ mapambano hayo tofauti na awali ambapo mashabiki wa ngumi za kulipwa wa mjini walikuwa wanapata fursa hiyo.
“Tumezoa kuona mambo haya katika soka lakini sasa Star Tv imepanua wigo na kuingia kwenye ngumi, tutaonyesha live mapambano yote ambayo Hall of Fame itayaandaa iwe ya hapa nchini au nje ya nchi,” alisema Kamote.
Ofisa Mtendaji mkuu wa Hall of Fame, Jay Msangi alisema makubaliano hayo yanatoa fursa kwa kampuni, taasisi na mashirika kujitokeza kudhamini ngumi na kujitangaza ndani na nje ya nchi.
“Mpango uliopo ni kuandaa mapambano sita ya kimataifa kila mwaka ambayo yatafanyika hapa nchini na mengine nje ya nchi, hivyo katika kila pambano moja, Kampuni ya  Star Tv italitangaza kwa siku 35 na siku ya pambano litarushwa live, kama litafanyika Dar es Salaam, watazamaji wa Star Tv wa mikoani watapata fursa ya kulishuhudia vivyo hivyo na wale wa Dar es Salaam ambao hawatakwenda ukumbini.
“Makubaliano haya sasa yanafungua milango kwa kampuni, taasisi na nashirika kutumia nafasi hiyo kudhamini masumbwi na kujitangaza kila siku katika siku 35 kila baada ya miezi miwili.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni inayowasimamia mabondia hapa nchini ya Respect Eagle, Chief Kiumbe alisema makubaliano hayo yatasaidia kuinua mchezo wa ngumi na mabondia hapa nchini.
“Tumekuwa tukishuhudia mashabiki wakikesha kusubiri mapambano ya Ulaya, tunataka hamasa hiyo ifanyije pia katika mapambano ya hapa nyumbani na tunaamini kwa umoja huu tutafanikiwa.
“Tunahitaji kuleta hamasa mpya katika ndondi na kuendana na kasi ya Serikali ya kuleta maendeleo hivyo umoja huu utaleta taswira mpya ya masumbwi,” alisema Chief Kiumbe.

Sunday, July 19, 2015

Wateuliwa kushikiri ndondi C Brazaville


Ndondi
Mabondia nyota wa Kenya Benson Gicharu uzani wa bantam, Rayton Okwiri uzani wa welter na Nick Abaka uzani wa middle wameruhusiwa na shirikisho la kimataifa la ndondi, Aiba, kuiwakilisha Kenya katika michezo ya mataifa ya Afrika mwezi Septemba nchini Congo Brazaville.
Habari hizi ni kwa mujibu wa naibu wa mwenyekiti wa chama cha ndondi cha Kenya Albert Matito.
Awali Aiba ilisema kwamba hawataruhusu mabondia hao wa Kenya washiriki michezo hiyo kwa sababu wanashiriki katika ndondi za kulipwa za Aiba.
Lakini Matito anasema mwenyekiti wa chama cha ndondi cha Kenya John Kameta amezungumza na wakuu wa Aiba wakakubaliana mabondia hao watatu washiriki michezo hiyo.
''Sote tumefurahishwa na uamuzi huo kwa sababu tunajua uwezo wa mabondia wetu na kwa vile wameshiriki ndondi za kulipwa za Aiba sasa wana mbinu mpya za kupambana na wapinzani wao huko Congo,'' alisema Matito.
Okwiri ndiye bondia pekee wa Kenya aliyeshinda medali katika michezo ya kumi ya mataifa ya Afrika iliyofanyika mwaka wa 2011 nchini Msumbiji aliporudi nyumbani na shaba.
Kenya ilimaliza ya kumi pamoja na Lesotho na Uganda huku Algeria ikiibuka mshindi na jumla ya medali saba, tatu za dhahabu. Mauritius ilimaliza ya pili na Cameroon ya tatu.

Tuesday, December 23, 2014

BONDIA TWAHA KASSIM WA MOROGORO AMTWANGA KWA KO, MUSSA CHITEPETE WA SONGEA


  • Share on facebook
    Share on google_plusone_shareShare on twitterShare on linkedin
Mabondia Twaha Kassim wa Morogoro kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Mussa Chitepete wa Songea wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Kassim alishinda kAwa K,O ya raundi ya sita Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Mussa Chitepete wa Songea akiwa chini baada ya kupokea konde zito kutoka kwa Twaha Kassim wa Morogoro wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Kassim alishinda kwa K,O ya raundi ya 6 Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Cosmas Cheka kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Ramadhani Shauri wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Cheka alishinda kwa point mpambano uho wa raundi 8 Picha na SUPER D BOXING NEWS

Monday, December 15, 2014

Amir Khan amchapa Alexander Devon

Amir Khan Kushoto akimzaba makonde bondia Alexander Devon wa Marekani .Amir Khan alishinda pigano hilo la raundi 12 kwa wingi wa pointi
Bondia wa Uingereza Amir Khan ametetea taji lake la uzani wa Welterweight kwa wingi wa pointi dhidi ya bondia raia wa Marekani Devon Alexander mjini Las Vegas.
Baada ya Khan mwenye umri wa miaka 28 kutawala raundi za mapema ,Alexander alitoa upinzani hafifu hadi raundi ya 8 ambapo aliweza kumpiga makonde Khan.
Lakini Khan ambaye anasifika kwa wepesi wake wa kurusha makonde aliendelea kudhibiti pigano hilo huku majaji wote wakimpatia ushindi.
Baadaye Khan alisisitiza mpango wake wa kutaka kuzichapa na bingwa wa dunia katika uzani huo Floyd Mayweather.
''Ninaamini kwamba nimefaulu kupewa fursa dhidi ya Bondia Mayweather baada ya ushindi huu'', alisema Khan.

Friday, December 5, 2014

MPAMBANO WA NGUMI WA KUFUNGULIA NMWAKA 2015


  • Share on facebook
    Share on google_plusone_shareShare on twitterShare on linkedin

Monday, November 24, 2014

Majia suffers KO defeat in Pacquiao supporting bout

Print
Tanzania�s Bantamweight boxer Fadhil Majia
Tanzania’s Bantamweight boxer Fadhil Majia suffered a third-round knockout loss to Philippine’s Jerwin Ancajas in an international, non-title Super Flyweight bout in Macau, China yesterday.

The eight-round fight was among the supporting bouts for the World Boxing Organisation (WBO) Welterweight title fight pitting Philippine’s Manny Pacquiao against USA’s Chris Algieri.

The Pugilist Syndicate of Tanzania (PST) secretary general, Anthony Luta, whose body facilitated Majia’s trip to Macau, said the Tanzanian boxer was sent down by his opponent’s counter-punch in the third round.

Luta said fighting in front of an audience all over the world might have put pressure on Majia and resulted to the loss.

“Majia was the first ever Tanzanian boxer to have landed the opportunity to take part in such a high profile fight…he, therefore, might have failed to handle the pressure accompanying the chance,” Luta said.

Luta said the knockout defeat was also the first for Majia outside Tanzania. The boxer’s record now stands at 15 victories (seven knockouts), six losses (two knockouts) and draw in four bouts.

“We selected Majia for the fight because of his impressive record. Unlike other Tanzanian boxers, he had never lost by knockout outside the country prior to the yesterday fight,” he said.

Majia was among four Tanzanian boxers that were previously shortlisted for the opportunity to take part in the bout. Others were Francis Miyeyusho, Sadick Momba and Mohamed Matumla.

Momba, however, was omitted from the list as he has secured chance to fight Ghanaian Emmanuel Agoye, in an international, non-title bout in Accra on December 5.

The winner of the Accra bout will then take part in the World Boxing Federation (WBF) Lightweight title fight against a German opponent in the latter’s backyard in February, next year.

“Miyeyusho, for instance, does not have a good record in fights outside Tanzania. He has always been losing by knockout and that is why we did not select him”, Luta said.

Friday, November 14, 2014

BONDIA THOMAS MASHALI ASAINI KUZIPIGA JANUAR MOSI 2015

  • Share on facebookShare on google_plusone_shareShare on twitterShare on linkedin
Bondia Thomasi Mashali kushoto akitia saini ya kupigana na Abbdallah Pazi kulia baada ya makubaliano na promota Kassim Texas katikati mpambano utakaofanyika january mosi katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam Picha na SUPER D BLOG
 
Bondia Abbdallah Pazi kulia akitia saini ya kupigana na Thomasi Mashali kushoto baada ya makubaliano na promota Kassim Texas katikati mpambano utakaofanyika january mosi katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam Picha na TUPAMBANE BLOG 
Bondia Thomasi Mashali kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Pazi baada ya makubaliano juzi  ya mpambano wao kufanyika January Mosi 2015 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaa Picha na TUPAMBANE BLOG
Promota Kassim Texas katikati akiwainuwa mikono juu mabondia Thomas Mashali kushoto na Abdallah Pazi kuashilia makubaliano ya mpambano wao utakaofanyika january mosi katika ukumbi wa frends corner manzese Picha na TUPAMBANE BLOG
Bondia Thomasi Mashali kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Pazi baada ya makubaliano juzi  ya mpambano wao kufanyika January Mosi 2015 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaa Picha na TUPAMBANE BLOG

Wednesday, November 12, 2014

MABONDIA IBRAHIMU TAMBA NA JULIUS KISARAWE WANYAKUWA MIKANDA YA TPBO

Bondia Mrisho Adam  kushoto akipambana na Mustafa Dotto wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Adam alishinda kwa pointi mpambano huo Picha na tupambane blog
Bondia Mrisho Adam  kulia akipambana na Mustafa Dotto wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Adam alishinda kwa pointi mpambano huo Picha na tupambane blog
Mabondia Karim Ramadhani Kushoto akipambana na Stevin Kobelo wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita mchazo huo ulimalizika kwa droo picha na  tupambane blog
Bondia Hassani Kiwale kushoto akipambana na Julius Kisarawe wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa Taifa wa chama cha TPBO Kisarawe aluishinda kwa pointi mpambano huo Picha natupambane blog
Bondia Maisha Samson kushoto akipambana na Ibrahimu Tamba wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wili iliyopita Tamba alishinda kwa K,O ya raundi ya Pili na kunyakuwa ubingwa  Picha na tupambane blog
Refarii Sako Mtlya akimnyoosha mkono juu bondia Ibrahimu Tamba baada ya kumgalagaza Maisha Samsoni kwa K,O ya raundi ya pili katika mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Picha na tupambane blog

Saturday, November 8, 2014

NGUMI KUPIGWA JUMAPILI MANZESE UKUMBA WA MANYARA

BONDIA Samsoni Maisha wa kyela Mbeya amewasili jijini Dar es salaam na kutamba kunyakuwa ubingwa wa TPBO kwa kumpiga Ibrahimu Tamba wakati wa mpambano utakaofanyika novemba 9 mwaka huu katika ukumbi wa Manyara Park Manzese Dar es salaam
mpambano huo wa raundi kumi kugombania ubingwa wa taifa unaotambuliwa na TPBO utatanguliwa na mpambano mwingine wa ubingwa kati ya julius Kisarawe na
Moro Best mpambano wa raundi kumi pia mwandaaji wa mpambano huo Jafari Ndame amesema maandalizi yote yapo tayali hivyo wanasubili siku tu kukamilisha mpango mzima
Aliongeza kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi ambapo Karim Ramadhani atapambana na Stevin Kobelo na Robinson Msimbe atamenyana na Fadhili Boika na mipambano mingene mikali zaidi siku hiyo kutakuwa na michezo ya utangulizi zaidi ya nane yenye raundi sita sita
katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha kabisa kutokana na kujipanga vizuri katika swala hilo kingilio ni shilingi, 5000; kwa kila mtu mchezo huu utapambwa na burudani mbalimbali
siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua
mpaka kujua kitu kamili katika
mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd
Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani

Wednesday, November 5, 2014

BONDIA IDDI PIALALA AIBEBA KIWANGWA BAGAMOYO KWA KUNYAKUWA UBINGWA WA KANDA YA MASHARIKI

Bondia Iddi Pialali kushoto akipambana na Fadhili Mkunda wakati wa mpambano wao wa kuwania ubingwa wa kanda ya masharika mpambano uliofanyika Kiwangwa Bagamoyo Mkoa wa Pwani,  Pialali alishinda kwa K,o ya raundi ya tano na kutwaa ubingwa huo 
Bondia Iddi Pialali kushoto akipambana na Fadhili Mkunda wakati wa mpambano wao wa kuwania ubingwa wa kanda ya masharika mpambano uliofanyika Kiwangwa Bagamoyo Mkoa wa Pwani,  Pialali alishinda kwa K,o ya raundi ya tano na kutwaa ubingwa huo 
Bondia Iddi Piyalali akiwa na mkanda wa ubingwa wa Kanda ya Mashariki 
Bondia Iddi Pialali
Bondia Iddi Pialali
Bondia Hashimu Zuber kushoto akipambana na Ally Mahiyo wakati wa mpambano wao uliofanyika kiwangwa bagamoyo mkowa wa pwani Zuber alishinda kwa point mpambano huo 
Wapenzi na mashabiki wa mchezo wa ngumi wakifuatilia mchezo huo uliopigwa siku ya jumatatu kiwangwa bagamoyo mkoa wa pwani 
Bondia Ally Bugingo kushoto akimtupia konde Twalibu Tuwa wakati wa mpambano wao Bugingo alishinda kwa point
BAADHI YA WATU AMBAO WALIKOSA KUINGIA UKUMBINI KWA KUTOKUWA NA PESA WAKIPIGA CHAPO KWENYE DIRISHA…….
……………………………………………………..
Na Mwandishi  Wetu
BONDIA Iddi Pialali mwanzoni mwa wiki hii aliwainuwa mikono juu wakazi wa Kiwangwa Bagamoyo Mkoa wa Pwani baada ya kunyakuwa ubingwa wa kanda ya mashariki kwa kumtwanga kwa K,O  ya raundi ya tano bondia Fadhili Mkundi
mpambano huo wa ubingwa ulianza mnamo saa 4 na dakika 20 usiku
uku mashabiki wakimshangilia Pialali kwa furaha mwanzo mwisho raundi ya kwanza ilianza kwa mashambulizi ya kutupiana makonde ya uku na kule ambayo yaliwavutia sana wakazi wa kiwangwa ilipofika raundi ya tatu mashambulizi yakawa kwa upande mmoja ambapo Pialali alibadilisha mchezo kwa kupiga ngumi za tumbo yani juu na chini kufika raundi ya tano Pialali aliongeza mashambulizi hayo kwa kasi na kumfanya refarii wa mpambano huo Pembe Ndava  kumuhesabia mpinzani ambaye alikuwa akivuja damu puani na mdomoni ambapo mpinzani huyo alisalimu amri na Pialali kuibuka kidede kwa kushinda K,O raundi ya tano
kabla ya mpambano huo kulikuwa na mapambano ya utangulizi yaliyowakutanisha mabondia Hashimu Zuber aliyempiga kwa pointi Ally Maiyo na Ally Bugingo alimsambalatisha kwa pointi Twalibu Tuwa
Mwisho wa mchezo huo promota wa mpambano huo Bernard Mwakyusa amewaahidi wakazi wa Kiwangwa Bagamoyo kuwa atapeleka burudani ya masumbwi mara kwa mara kwa kuwa sasa kuna bingwa anayetambulika rasmi katika tasnia ya masumbwi nchini
TUPAMBANE BLOG