Mkuu wa
vipindi wa Star TV, Yusuph Kamote kushoto akibadilishana mkataba na Jay
Msangi mara baada ya kusainiwa jijini leo. Akishuhudia tukio hilo ni
Chief Kiumbe
Na Mwandishi wetu
Kituo cha
Televisheni cha Star Tv kimeingia makubaliano na kampuni ya Hall of
Fame kwa ajili ya kurusha moja kwa moja ‘live’ mapambano sita ya ngumi
za kulipwa nchini kuanzia mwezi ujao.
Hatua hiyo ina lengo la kuendeleza mchezo huo ambao ni wa pili kwa kupendwa nchii kwa mujibu wa Mkuu wa Program wa Star Tv Dar es Salaam, Yusuph Kamote.
Kamote
alisema kuwa kwa kupigia kituo chao ambacho kina masafa marefu na
kupatikana hadi maeneo ya vijijini, mashabiki wa ngumi za kulipwa
watapata fursa ya kujionea ‘live’ mapambano hayo tofauti na awali ambapo
mashabiki wa ngumi za kulipwa wa mjini walikuwa wanapata fursa hiyo.
“Tumezoa
kuona mambo haya katika soka lakini sasa Star Tv imepanua wigo na
kuingia kwenye ngumi, tutaonyesha live mapambano yote ambayo Hall of
Fame itayaandaa iwe ya hapa nchini au nje ya nchi,” alisema Kamote.
Ofisa
Mtendaji mkuu wa Hall of Fame, Jay Msangi alisema makubaliano hayo
yanatoa fursa kwa kampuni, taasisi na mashirika kujitokeza kudhamini
ngumi na kujitangaza ndani na nje ya nchi.
“Mpango
uliopo ni kuandaa mapambano sita ya kimataifa kila mwaka ambayo
yatafanyika hapa nchini na mengine nje ya nchi, hivyo katika kila
pambano moja, Kampuni ya Star Tv italitangaza kwa siku 35 na siku ya
pambano litarushwa live, kama litafanyika Dar es Salaam, watazamaji wa
Star Tv wa mikoani watapata fursa ya kulishuhudia vivyo hivyo na wale wa
Dar es Salaam ambao hawatakwenda ukumbini.
“Makubaliano
haya sasa yanafungua milango kwa kampuni, taasisi na nashirika kutumia
nafasi hiyo kudhamini masumbwi na kujitangaza kila siku katika siku 35
kila baada ya miezi miwili.
Naye
Mkurugenzi wa Kampuni inayowasimamia mabondia hapa nchini ya Respect
Eagle, Chief Kiumbe alisema makubaliano hayo yatasaidia kuinua mchezo wa
ngumi na mabondia hapa nchini.
“Tumekuwa
tukishuhudia mashabiki wakikesha kusubiri mapambano ya Ulaya, tunataka
hamasa hiyo ifanyije pia katika mapambano ya hapa nyumbani na tunaamini
kwa umoja huu tutafanikiwa.
“Tunahitaji
kuleta hamasa mpya katika ndondi na kuendana na kasi ya Serikali ya
kuleta maendeleo hivyo umoja huu utaleta taswira mpya ya masumbwi,”
alisema Chief Kiumbe.
No comments:
Post a Comment