Mhe Ummy Mwalimu akiwa na waziri wa afya (Uganda) Mhe .Sara Opendi na Mhe Omar Sey Waziri wa Afya wa Gambia.
Waziri wa afya Ummy Mwalimu akifuatilia mkutano huo
Picha ya
pamoja ya wake wa marais na mawaziri wa afya wa afrika,waliohudhuria
mkutano wa 10 wa kupambana na saratani ya shingo ya Kizazi,matiti na
tezi dume (picha/habari na wizara ya afya)
Na.Mwandishi wetu,Addis Ababa
Ugonjwa
wa saratani nchini Tanzania ni chanzo cha magonjwa na vifo,hivyo
inakadiriwa Takribani wagonjwa wapya wa saratani 45,000 hugundulika kila
mwaka.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
Ummy Mwalimu katika Mkutano wa 10 wa kupambana na ugonjwa wa saratani ya
shingo ya kizazi, matiti na tezi dume barani Afrika unaofanyika nchini
hapa.
Waziri
Ummy amesema kati ya wagonjwa hao asilimia 38 ni wa saratani ya shingo
ya kizazi kwa wanawake, asilimia 14 saratani ya ngozi, asilimia 10
saratani ya matiti na saratani ya tezi ni asilimia 4
Hatahivyo,takribani watu 35,000 hufariki kila mwaka kutokana na magonjwa ya Saratani.
Licha ya
changamoto mbalimbali zinazokwamisha jitihada za kukabiliana na magonjwa
hayo ikiwemo uhaba wa Miundombinu ya kutolea huduma za afya, vifaa
tiba, Uhaba wa Watumishi wa Afya, rasilimali fedha na gharama kubwa za
dawa za matibabu ya saratani,Waziri Ummy amesema Serikali ya Tanzania
imepitisha Sera za Kitaifa na Miongozo mbalimbali ya Kupambana na
Saratani, kutoe Elimu kwa jamii na watoa huduma za afya nchini kuhusu
Saratani.
Aidha,
kuanzishwa kwa huduma za upimaji wa saratani katika Hospitali na vituo
vya afya zaidi ya 300 nchini na huduma za Tiba kupitia Hospitali ya
Saratani ya Ocean Road.
“Serikali
itapanua wigo wa matibabu ya saratani katika Hospitali ya Bugando
Mwanza na KCMC, Kilimanjaro. Mipango ya baadae ni huduma hizo pia
kutolewa ktk Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya.”hii itapunguza
wagonjwa kufuata huduma kwenye hospitali ya saratani ya Ocean Road
Mkutano
wa 10 wa Saratani ya shingo ya kizazi, matiti na tezi dume barani Afrika
unafanyika kwa kuasisiwa kwa juhudi za wake za Marais wa bara la
Afrika.
Mkutano
huu unahudhuriwa na Wake wa Marais wa Afrika, Mawaziri wa Afya wa
Afrika, Wanataaluma na Wadau wa Maendeleo. Lengo kuu ni kufanya mapitio
ya hatua zilizochukuliwa na nchi za Afrika, changamoto zilizopo na
kuweka mikakati ya pamoja na ya nchi katika kukabiliana na saratani.
Wakati wa
kukabidhiwa uenyekiti wa Umoja wa Wake wa Marais wa Afrika wa Kupambana
na saratani ya Shingo ya Kizazi, Matiti na Tezi Dume kutoka kwa
Mwenyekiti anaemaliza muda wake, mke wa Rais wa Kenya mama Magreth
Kenyatta, Mke wa Waziri Mkuu wa Ethiopia mama Roman Tesfaye Abneh
ameleeza masikitiko yake kwa jinsi ambavyo ugonjwa wa saratani unavyoua
kuliko hata ugonjwa wa UKIMWI na kifua kikuu. Hivyo ameziomba nchi za
Afrika kuongeza uwekezaji katika eneo hili hasa kwa kuhakikisha dawa
zinakuwepo za kutosha, kuboresha utoaji wa huduma za afya ikiwemo
upimàji na tiba, kuhakikisha nchi zinatoa mafunzo ya Kutosha kwa
watumishi wa afya katika fani hii
No comments:
Post a Comment