Ndani ya wiki moja nimekutana na watu watatu wakitafuta sh.500/= ya sarafu kwa sh.2500/= kwa sarafu moja ya mia 5, mwanzoni nilipuuzia lakini baada ya kutulia na kufanya utafiti nimegundua kwanza hii sarafu imekuwa adimu na inatafutwa kwa udi na uvumba
Pili ni kwamba wale wapenzi wa SILVER sasa unaweza kupata cheni halisi ya silver kwa bei poa kabisa ! sababu ni kwamba zile sarafu za mia tano ndio zinayeyushwa na kutengeneza vidani siku hizi
Hii ni KASHFA nyingine kubwa kuhusiana na pesa yetu na mamlaka zinazohusika ziko kimya kuhusu hili lakini hii ndio hali halisi inayoendelea mitaani TUGUTUKE
No comments:
Post a Comment