Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Thursday, October 23, 2014

Maaskofu; Hatuogopi wala hatutishwi na kauli za Sitta

23
October
2014
Posted by Tupambane blog
TOLEO 40.indd
  • Askofu Sendoro; Askofu hana mipaka ya utume wake isipokuwa Mungu tu.
  • Wasema ni wajibu wao kusimamia ukweli kwa ajili ya taifa
  • Waeleza hana sifa ya kuwa rais
    Na Sarah Pelaji
    Sitta ameshindwa kuelewa wajibu wa dini na siasa. Huwezi kuvitenga kwani masuala ya dini yanahusu siasa na siasa inaihusu dini. Kuongoza nchi bila uadilifu na hofu ya Mungu ndiko kutaleta matatizo.”
    Hayo yameelezwa na  baadhi ya maaskofu wa dini mbalimbali nchini wakieleza hisia zao za kusikitishwa na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta ambaye hafahamu kwamba maaskofu ni viongozi kama alivyo yeye.
    Makamu wa Rais Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki Rulenge –Ngara Mhashamu Severine Niwemugizi akiongea na gazeti hili amesema kwamba,  viongozi wa dini (Maaskofu)  wanao wajibu wa kuonya na kurekebisha pale mambo yanapopelekwa kiujanja na kuchezea wananchi jinsi wanavyotaka.
    Jukumu lake ni kuongoza watu kwa uadilifu. Tatizo lake hakubali mawazo ya upande wa pili na hataki changamoto,” ameeleza Askofu Niwemugizi akiendelea;
    “Ni busara akubali changamoto kutoka upande mwingine. Yale ambayo hapendi kuyasikia kutoka upande mwingine ni lazima ajifunze kuyasikia na sisi pia tukubali changamoto ili tuwe kitu kimoja badala ya kusukuma mambo kimabavu. Sisi tupo kwa ajili ya kujenga si kubomoa.”
    Kusikitishwa na maandiko katika tamko yaliyosema mchakato usitishwe kuna tafsiri tata kwa kuwa ndani ya bunge hilo wapo watu waadilifu ambao wapo kwa ajili ya maslahi ya wananchi na baadhi wapo kwa ajili ya maslahi binafsi. Kusema mchakato usitishwe ni kumuharibia malengo yake binafsi.
    Hata kama rasimu itapitishwa, bado kelele zitaendelea kuwepo kwani wananchi wanaona mambo yamelazimishwa kiujanja na itakuwa katiba ya upande mmoja.
    “Kila chama kikitengeneza katiba yake siku kikitoka madarakani chama kitakachotawala nacho kitaunda katiba yake. Ndiyo maana tunataka kauli moja ambayo inajenga taifa moja,” ameeleza.
    Askofu wa  KKKT Dayosisi ya Kaskazini Dk. Martin Shao ameeleza kwamba hakuna mtu mwenye mamlaka ya kuingilia Kanisa na kuliambia lifanye nini. “ Sisi tunaendelea kutoa sauti za kinabii, kurekebisha na kukemea uovu, na huo ni wajibu wetu. Tusipofanya hivyo tunakwepa wajibu wetu kwa jamii. Tutaendelea kusema ukweli na wala hatuogopi.”
    Askofu Shao wa KKKT amesema kuwa, Kanisa halitaogopa kupingwa na wala halitishwi na vitisho vya mtu ama kundi flani  kwa kauli zake na mitazamo yake binafsi. Kanisa ni sauti ya Mungu, ni sauti ya jamii, linayo haki ya kutetea haki. Hatutishiwi na vita kwani Kanisa tangu zamani lina historia ya kuwa na maadui wengi lakini lipo hai hadi leo.
    Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini Valentino Mokiwa ameeleza kusikitishwa na kauli ya Sitta kwa kuwaambia wameingilia siasa na matamko yao ni kinyume na utukufu wa Mungu.
    “Sisi hatukuandika kwa kutaka sifa kutoka watu wala utukufu wa dunia bali tuna mapenzi na nchi yetu na kutetea haki za watanzania. Sisi tumeongea kama wananchi na viongozi katika jamii kama alivyo yeye.  Wameamua kuvuruga na kupotosha watu alafu anaona huo ndio utukufu wa Mungu? Kauli yake pia haina utukufu wa Mungu na waliosema ana msongo wa mawazo, amejivuruga wanasema ukweli. Kuipotosha jamii kwa mabavu na fedha zao ni kosa ambalo hawatasamehewa,” ameeleza Askofu Mkuu Mokiwa.
    Hata hivyo ameeleza kuwa, Rais aliyeamuru Katiba Mpya iiundwe hawatukani maaskofu lakini yeye aliyepewa cheo cha muda anawatukana maaskofu bila woga na aibu. “Kama wanaotutukana ni wakristo wasije Kanisani kwani wakija sisi ni viongozi wao na tutawaamuru wapige magoti. Vyeo walivyonavyo tumewapa sisi na tunaweza kuwaondoa.”
    Amesema kauli zake hazitalinyamazisha Kanisa kusema ukweli, na hatakama wameilazimisha rasimu yao kupita haina utukufu kwa Mungu. Amesema kwamba anajua wanafedha za kuifanya ipite lakini utukufu wa Mungu haupiti kwa fedha. “ Wameiburuza rasimu lakini tutaona Mungu yuko upande gani watakapokuja kwa wananchi.”
    Askofu Mokiwa amemtaka kuwaomba radhi maaskofu kwa kauli zake za matusi na dharau ingawa halazimishwi ila matokeo yake yataonesha nani anasimamia haki na utukufu wa Mungu.
    Amesisitiza “Cheo chake ni cha duniani na achunge sana midomo yake kwani safari yake bado sana. Tulifikiri ni kiongozi mwadilifu wa kuiongoza nchi kama rais lakini amejishushia heshima. Aombe radhi na Mungu atamuona. Sisi hatujapewa uongozi na Mungu kuongoza kuku na mbuzi bali watu wa Mungu. Hatukuwa tumelewa wakati tunaandika tamko bali tuliandika yale yanayoigusa jamii kwa ajili ya faida ya wote.”
    Naye Askofu Mstaafu wa KKKT Elinaza Sendoro amemuonya Sitta kuweka mipaka ya maaskofu. “Askofu hana mipaka, mipaka yake ni Mungu tu. Ana uwezo wa kukemea jambo hatakama linatendeka duniani kote. Askofu hana mipaka ya kazi kwani yeye ni sauti ya Mungu.”

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG