Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Thursday, October 23, 2014

Papa: Uzee ni kipindi cha Neema

23
October
2014
Posted by Tupambane blog
papa-francisco copy
Vatikani
SEPTEMBA 28 mwaka 2014 Papa Fransisko alikutana na wazee kama ilivyokuwa imeandaliwa na Baraza la Kipapa kwa ajili ya familia, kuadhimisha Siku Kuu ya Wazee, iliyoitwa ” Baraka ya maisha marefu”. 
Papa Mstaafu BenediktoXV1, alikuwa miongoni mwao, ambapo kabla ya adhimisho la Ibada ya Misa, Papa Fransisko, alisikiliza baadhi ya shuhuda za wazee na pia kuongea nao.
Amemshukuru Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Familia, Askofu Mkuu Vincenzo Paglia kwa maandalizi haya , vilevile alipongeza pia Papa Mstaafu Benedikito XV1 kwa uwepo wake, na kwamba, mara nyingi amefurahia kuona anaishi ndani ya Vatikani.
Amemwita kuwa babu mwenye hekima ndani ya nyumba, ameshangazwa na ushuhuda wa wazee wawili kutoka Iraq walioweza kukimbia ghasia na vurugu, na kuita uwepo wao kuwa zawadi kwa Kanisa.
Papa Fransisko amesema, vurugu dhidi ya wazee na watoto siyo kitendo cha kiutu, lakini Mungu hawaachi wazee peke yao, huwapa msaada wake, ili waendelea kutoa kumbukumbu kwa ajili yao na kwa ajili yetu , kwa sababu ni sehemu ya familia kubwa ya Kanisa.
Imani yao ni kama mti unaoendelea kukua na kutoa matunda. Uzee ni kipindi cha neema ambamo Bwana anatualika katika wito wake, kutunza na kuonyesha Imani, anatualika kusali na hasa kuomba na kuwa karibu na wenye kuhitaji. Wazee wana uwezo wa kutambua hali ngumu , na nguzo yao ni sala ambayo ina nguvu, amesema Papa.
Papa aliendelea kuwa enzi babu na bibi kwamba, kwa namna ya pekee wamepokea baraka ya kuona watoto wao (Zab 128,6) na wao wamekabidhiwa kazi kubwa ya kuonyesha uzoefu wa maisha, historia ya familia katika Jumuiya ya watu. Babu ni “ Baba mara mbili”, na ndivyo ilivyo kwa bibi “mama mara mbili” Tukikumbuka wito wa babu wa kuendeleza thamani ya urithi wa Imani.
Papa Fransisko kwa maneno hayo, alikumbuka ziara yake aliyoifanya hivi karibuni nchini Albania na nchi nyingine zinazofanana na hiyo kwa kipindi cha kidkteta ya kikomunisti, kwamba ni wazee waliofanya kubatiza watoto mafichoni , na hivyo kuokoa imani ya watu hao.
Kwa nyakati hizi Papa Fransisko amebainisha kwamba siyo familia zote zinawapokea wazee, ndiyo maana ni vema kuwepo nyumba za kuwapokea , lakini ziwe nyumba ukweli na wala zisiwe mahabusu, nyumba hizo iwe kwa manufaa ya wazee na isiwe kwa manufaa mengine.
Kwa mantiki hiyo Papa amewashukuru kwa wale wote wanaokwenda kuwatembelea wazee katika nyumba za kupokea wazee, na wote wanatoa huduma kwao.Vile vile kwa vijana wengi wanao fanya kazi ya kuwafurahisha wazee wenye nyuso za masikitiko , kurejea furaha ya maisha katika umri wao mkubwa.
Papa amesema kwamba kuna tatizo kubwa la kuwaacha wazee peke yao, akisema katika ukweli hii ni sawa na eutanasia iliyojificha.
Matatizo ya utamaduni wa ubaguzi dhidi ya watoto, vijana wasio kuwa na kazi, na wazee inasikitisha sana, hasa pale inapokuwa kwa sababu za mipango ya kiuchumi na maisha. Papa alitaja ubaguzi huo ni nje ya utu tena ni ubatili mtupu.
Ni lazima kutanguliza utu na si fedha. Aliongeza na kumtaka, kila Mkristo, kupinga sumu ya utamaduni wa ubaguzi, na kuunda jamii tofauti, inayokaribisha zaidi, yenye utu zaidi , na zaidi ya yote ambayo haiweki pembeni wadhaifu na wanyonge.
Watu wasio tunza wazee , ni watu wasiokuwa na maisha endelevu , kwa sababu wanapoteza kumbukumbu, na kupoteza mzizi. Kila Mkristo lazima atunze mzizi wa njia ya sala, neno la Injili na matendo ya huruma. Papa alimalizia akitoa mfano kwamba vitu vizuri katika maisha ya familia , na katika maisha ya binadamu ni kumbembeleza mtoto na kumwacha mtoto abembelezwe na babu na bibi.

Homilia ya Papa kwa wazee, imekuwa ni makutano yaliyojaa furaha ,amani na matumaini

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG