MCHUNGAJI Peter Rashid Abubakari wa Kanisa la RGC lililoko Mbezi ya Shamba jijini Dar, amedaiwa kuoa mke wa pili aitwaye Pamela Didas Asenga akiwa na umri wa miaka 20 tu ‘dogodogo’, Risasi Jumamosi limetonywa.
Mchungaji Peter Rashid Abubakari wa Kanisa la RGC akimuoa ‘dogodogo’, Pamela Didas.
Mke mwingine wa mtumishi huyo wa Mungu anaitwa Zuwena (Catherine) aliyemuoa mwaka 1985. Lakini kuna madai kwamba, mke huyo amemwacha.
Mchungaji Peter Rashid Abubakari akipiga picha na mke mpya wakati wa harusi.
“Alituambia Mungu amemfunulia na amempa mke mwingine mwema ambaye ni binti mbichi, watu wewee,” kilisema chanzo.
Mchungaji Peter Rashid Abubakari akiwa mke mpya.
Sasa baada ya picha za mtumishi huyo kusambaa hadi kwenye mitandao, Risasi Jumamosi, juzi lilifika kanisani kwake Mbezi ili kuzungumza naye lakini hakuwepo.
Mchungaji Peter Rashid Abubakari akiongoza maombi kanisani.
Baadaye mwandishi wetu alimtafuta mchungaji huyo kwa njia ya simu ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Nipo Kiluvya kikazi lakini hilo lipo ila ni jambo langu binafsi siyo la kulitangaza.”
Baadaye alimtumia ujumbe mwandishi akiwa ameuandika hivi:
“Sanchawa mimi ni Nabii wa Mungu Yehova, uliponipigia tu kila kitu Mungu akaniambia nia yako na kusudi lako.”
Mchungaji Peter Rashid Abubakari.
Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yao magazetini, baadhi ya wachungaji hao walimpongeza Mchungaji Peter kwamba, aliona alikokuwa na anakokwenda ndiyo maana aliamua kuchukua uamuzi huo.
No comments:
Post a Comment