- Written by Tupambane Blog
-
Share on facebook Share on gmail Share on twitter
Mwandishi Wetu
MPAMBANO wa mchezo wa masumbwi mkali utakaokutanisha mabondia mbalimbali kutoka kila kona ya Tanzania utafanyika October 25 katika ukumbi wa friends Corner manzese jijini Dar es salaam.
Akizingumza na waandishi wa habari mratibu wa mpambano huo kocha wa
kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema
kuwa siku hiyo kutakuwa na mpambano wa mahasimu katika mchezo wa ngumi
kati ya bondia Saidi Mbelwa 'Moto wa Gesi' na George Dimos.(T.k)
Mpambano
mwingine utawakutanisha Amani Bariki 'Manny Chuga' na Ally Bugingo
mpambano unaosubiliwa kwa hamu kila kona ya jiji la Dar es salaam ambapo
mabondia hawo wamejizolea umaarufu mkubwa kupitia mchezo huo pambano jingine ni kati ya Juma Fundi atakaezichapa na Hamza Mchanjo wakati Hasani Mandula ataonyeshana kazi na Mohamedi Jaka.
Na
Shabani Kaoneka atazipiga na Ibrahimu Maokola anaejiandaa kuwania
kucheza ubingwa wa taifa mwishoni mwa mwaka huu Fadhili Boika atazipiga
na Godfrey Silver na Habibu Pengo atazidunda na Abdallah Luanje,
Kashinde Mohamedi atazidunda na Mohamed Kibaga wakati Sadiki Nuru
atakumbana na Mohamed Mbishi katika
mpambano huo siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha kabisa kutokana na
kujipanga vizuri katika swala hilo kingilio ni shilingi, 5000; kwa
kila mtu mchezo huu utapambwa na burudani mbalimbali
No comments:
Post a Comment