- Written by Tupambane Blog
-
Share on facebook Share on gmail Share on twitter
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefahamishwa na Shirikisho la Mpira
wa Miguu Afrika (CAF) kuwa Tanzania haitaweza kuwa mwenyeji wa Fainali
za Afrika- AFCON 2017 kwa kuwa haijawahi kuandaa fainali zozote za
vijana Afrika. Fainali hizo ni zile za vijana wenye umri chini ya miaka
17 na 20.
Hivyo, TFF inaelekeza nguvu zote katika kuandaa Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka U17 mwaka 2019.(Thommy kundy)
Tunapenda
kuchukua fursa hii kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanazania,
Jakaya Kikwete kwa kututia moyo katika kuomba uenyeji wa AFCON 2017.
Pia
tunamshukuru Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella
Mukangara kwa juhudi binafsi alizozionyesha katika jitihada za Tanzania
kuomba uenyeji wa AFCON 2017.
TFF inaamini kwa dhati kuwa uenyeji wa Afrika U17 2019 utaifungulia Tanzania milango ya kuandaa mashindano makubwa zaidi.
WANYARWANDA KUCHEZESHA MECHI YA STARS
Waamuzi
kutoka Rwanda ndiyo watakaochezesha mechi ya Kalenda ya Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kati ya Taifa Stars na Benin
itakayofanyika Jumapili (Oktoba 12 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Hakizimana
Louis ndiye atakayeongoza waamuzi hao wa FIFA kwa kupuliza filimbi
kwenye mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia
saa 11 jioni. Atasaidiwa na Simba Honore na Niyitegeka Jean Bosco.
Mechi
hiyo itatanguliwa na ile ya viongozi wa dini- Kiislamu vs Kikristo
kudumumisha upendo, amani na ushirikiano itakayoanza saa 9 kamili
alasiri. Tiketi za elektroniki zitakazotumika kwa mechi hiyo tayari
zimeanza kuuzwa kwa kiingilio cha sh. 4,000 na sh. 10,000.
Wakati
huo huo, Kocha Mart Nooij ameongeza wachezaji watatu kwenye kikosi cha
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ili kukiongezea
nguvu kwa ajili ya mechi hiyo.
Wachezaji walioongezwa ni Jonas Mkude na Joram Mgeveke kutoka timu ya Simba, na Gadiel Michael wa Azam.
MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litakuwa na mkutano na waandishi wa
habari kesho (Oktoba 8 mwakahuu). Mkutano huo utafanyika saa 5 asubuhi
kwenye ofisi za TFF, Jengo la PPF Tower.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment