Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Thursday, October 23, 2014

Wakulima mkoani Ruvuma waaswa kuhakikisha kilimo hakiingiliwi na s

Posted By Tupambane blog - (155) Views


Wakulima Mkoani Ruvuma  wametakiwa kuwa makini na kazi yao ngumu ya kilimo kwa kuhakikisha  Kilimo hakiiingiliwi na Siasa kwani Siasa mara zote ndiyo inayoharibu maendeleo ya uchumi wa wananchi kwa maslahi ya wachache. Hayo yamesema na Mkulima Maarufu Mkoani hapa Aizack Mwilamba ambaye pia ni wakala wa pembejeo za kilimo, anasema Mawakala walio wengi hukata tamaa baada ya Serikali kushindwa kulipa Vocha kwa wakati.
IZACK MWILAMBA SHAMBANI KWAKE
Isack Mwilamba akiwa shambani kwake
Mwilamba amesema Msemo wa Kilimo Kwanza uendane na Serikali kuwezesha pande zote zinazolenga kumuinua mkulima ikiwa ni pamoja na kulipa kwa wakati mwafaka Madeni ya Vocha kwa mawakala. Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa Mikoa inayotegemewa kwa upande wa Kilimo, Mkoa wa Ruvuma ambao una wakaazi 1,400,000,  ambao wakaazi wake hutemea Kilimo kwa asilimia 80%.
Maendeleo ya Kilimo katika Mkoa wa Ruvuma yalianzishwa Mwaka 1977 wakati Agizo la Mlale lilipoanzishwa kwa madhumuni ya kumfanya kila mwana Ruvuma kushiriki katika Kilimo.
Wananchi waliounga mkono suala hilo wakiongozwa na Mzee Izack Mwilamba ambaye shughuli zake za Kilimo alianzia Kijiji cha Mgazini Kata ya Kilagano Peramiho, Songea Vijijini kwa kulima Ekari 150 ambazo kila mwaka hutoa kiasi cha Tani 250 na kuendelea. Mafanikio ya Mwilamba na wakulima wengine waliofanikiwa katika Kilimo yametokana na Matumizi mazuri ya Mbolea, yeye hutumia Mbolea za Urea, Minjingu, USA pamoja na Mbolea ya asili.
Mwilamba amesema mara zote Wataalamu hushauri kutumia mbolea kwa mpangilio kuwa na mbolea ya kupandia , ya kukuzia na kutumia mbolea hizo kwa muda maalumu.
Mwilamba amesema utumiaji wa Mbolea kwa kufuata Utaalamu uliozoeleka mara nyingi huweza kumwangusha Mkulima, anasema yeye mbinu alizogundua katika Kilimo cha Kisasa ni ni mchanganyiko wa Mbolea ambao huchanganya pamoja na kutia kwa wakati maalumu.
Amesema anachanganya Mbolea ya Chumvi chumvi Urea na Dap pamoja halafu anazitia kwapamoja baada ya Mhindi kufikia Urefu wa Futi moja na nusu, halafu anasubiri mpaka Mhindi unapokuwa umekaa ukiwa na Majani, siku akishatia mbolea hiyo basi yeye anasubiri kuvuna.
Mwilamba amekuwa mzoefu wa Kilimo ambaye hutumia mbolea ambazo haziwezi kumwangusha, Pia amekuwa wakala wa Mbolea kwa mda mrefu ambapo yeye Pembejeo za Kilimo huzichukua na  kumpelekea moja kwa moja Mkulima Shambani.
Mwilamba ambaye ana ekari 150 za Shamba la Mahindi amekuwa shamba darasa kwa wakulima wanaomzunguka anatoa elimu kwa wakulima wengine katika Matumizi ya Mbegu, anasema Mkulima anatakiwa awe mwangalifu kwa kuwa wako Mawakala wasio waaminifu, huuza Mbegu ambazo hazina ubora, halafu husingizia kuwa Pembejeo za Mbolea siyo nzuri .
Izack Mwilamba amewataka wakulima kuzingatia Utaalamu wanaopewa na Mawakala waliobobea kama yeye, pia kupokea Ushauri wa wataalamu wa Kilimo ambao ni wakulima na siyo wana Siasa kwa kufanya jhivyo wataweza kufaulu katika Kilimo.
Mwilamba amesema kwa hivi sasa amekuwa akitoa Shamba darasa kwa kuwakusanya wanakijiji wanaomzunguka katika Shamba lake la Mgazini ambalo kila Mkulima hufanya zoezi kwa vitendo moja kwa moja kuanzia kulima hadi kupanda na katika utiaji wa mbolea,
Pamoja na kutoa Elimu hiyo ya Shamba Darasa Wana Kijiji wanao kuja Shambani hapo hulipwa Ujira kwa Siku ambapo zaidi ya watu 200 hufika Shambani hapo na wanalipwa Kiasi kinachozidi 600,000 kwa siku.
Mkuima Stadi Izack Mwilamba amesema Kilimo ukikizingatia kinakutoa katika Umaskini. Kwa upande wake kupitia Kilimo amefanikiwa Kujenga Hoteli kubwa ya Kisasa yenye Ghorofa tatu ambayo iko Stendi kuu ya Mabasi iitwayo UGABE. Pia kupitia Kilimo amefanikiwa anaweza kusomesha watoto hadi kufikia kiwango cha Elimu ya juu ya Sekondari na wengine kupata Shahada katika Chuo ingawa yeye hana elimu yoyote, lakini anasema anamudu hayo yote kutokana na Fedha anazozipata kupitia Kilimo.
SHAMBA LA MAHINDI
Shamba la mahindi
Tumbaku shambani
Shamba la Tumbaku
Izack akizungumzia suala la Pembejeo na Mbegu amesema Mkulima hatakiwi kuwa na Shamba la Majaribio kwa Mbolea au Mbegu, Mkulima anatakiwa kutumia Mbegu alizozizoea pamoja na Mbolea aina ya Urea, Minjingu, SA, huvuna Mavuno machache bila kujua kosa alilolifanya.
Anasema Mwilamba kuwa Wataalamu wa Kilimo nao wanatakiwa kuwaelewesha wakulima jinsi ya kutumia Mbolea katika Aridhi zilizochoka, Uking`ang`ania kiutaalamu tuu unaweza kumshushia mkulima Mazao ya kutosha.
Pamoja na Mafanikio hayo amesema zipo changamoto zinazomyumbisha Mkulima asifikie lengo ikiwa ni pamoja na baadhi ya Mawakala wasio waaminifu ambao huzunguka vijijini kwa wakulima na kuwarubuni kwa kukusanya mazao baada ya mavuno wakijifanya wananunua kama Serikali kumbe sivyo ambapo wakulima hulipwa hela kwa vipindi matokeo yake wengine msimu ukipita hulala mbele pasipo kukamilisha malipo kwa wakulima.
MAHINDI KITENGO CHA UNUNUZI
Mahindi kitengo ya Ununuzi
Changamoto nyingine ni upande wa mfumo wa Utoaji pembejeo kwa wakulima kupitia mawakala kwa mtindo wa vocha au stakabadhi haumnufaishi mkulima bali wafanya biashara wakubwa au viongozi wanajinufaisha kupitia mgongo wa wakulima Serikali inapaswa kuangalia kwa makini mfumo huo.
Anaendelea kusema kuwa katika uuzaji wa Mazao katika Vitengo vya kuuzia NFRA wakulima wanauza kwa shida wenye kipato wanauza kupitia mgongo wa wakulima wadogo, wanaomba serikali kama inashindwa kusimamia masoko basi waruhusu wakulima wakauze wenyewe nje kwa kujitafutia masoko kwani ali iliyopo haitawanufaisha hata kama watazalisha kwa wingi masoko na mifumo ni shida kwa mkulima wa kawaida.
Izack Mwilamba ni Mkulima na wakala ambaye amekuwa na maduka 4 ya kuuzia Pembejeo za Kilimo Mkoani Ruvuma, Pia ni wakala wa Pembejeo katika Maeneo ya Peramiho ambapo Uwakala wake umeungwa mkono na Viongozi wa Serikali Mkoa wa Ruvuma akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma said Thabit Mwambungu na Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti. Hata hivyo amewashukuru wasambazaji wa Mbegu za Mahindi aina ya PAN kuwa mbegu zao ni Bora na zina Tija.
Tumbaku iliyokauka Ghalani
Wakulima wakiwa Ghalani na magunia ya Tumbaku iliyokaushwa
Mkoa wa Ruvuma kila mwaka huzalisha kiasi kikubwa cha mazao ya chakula kama mahindi kiasi cha kukidhi mahitaji ya wananchi wa Mkoa mzima na ziada kupelekwa maeneo mbali mbali ya nchi na nje ya nchi ambako kunakuwa na uhaba wa chakula hadi hivi sasa wanapotarajia kuvuna mahindi ya msimu huu bado kuna wananchi wengi wana mahindi ya mwaka jana ambayo walikosa soko la kuuzia baada ya kitengo cha hifadhi ya chakula kukamiliha kununua kiasi walichopanga kwa hifadhi na kuacha mahindi mengi mikononi mwa wakulima.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG