- Written by Tupambane Blog
-
Share on facebook Share on gmail Share on twitter
Thommy kundy
Shirika
la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) laanza kuuza viwanja takribani 444
vyenye jumla ya mita za mraba 465,161 katika eneo la Kiluvya A
Halmashauri ya Kisarawe Mkoa wa Pwani.
Hayo
yamesema na Meneja Miradi wa NSSF Bw.Abdallah Mseli wakati wa ziara ya
waandishi wa habari walipotembelea eneo la mradi huo kuona maendeleo ya
mradi huo .(Thommy kundy)
"Eneo
hili litakuwa na makazi mapya ya kisasa, litakuwa na huduma muhimu za
maji,umeme,barabara na pia kuna maeneo ya kujenga shule, zahanati na
maduka ya kisasa " alisema Mseli
Akifafanua
zaidi kuhusu mradi huo Mseli amesema fomu za maombi ya kununua viwanja
zinapatikana kwa gharama ya shilingi elfu 40,000 katika ofisi ya
Mkurugenzi wa Halmashuri ya Wilaya ya Kisarawe na Ofisi za NSSF Benjamin
Mkapa Pension Towers.
Akizungumzia
bei za viwanja Mseli alisema kwa kiwanja cha makazi pekee (ujazo wa juu
na kati) gharama kwa kila mita ya mraba ni elfu 15,000/- wakati wakati
kwa makazi pekee (ujazo wa chini) Mita moja ya mraba ni 16,000/.
Kwa
upande wa Viwanja kwa ajili ya Makazi na biashara Mseli alibainisha kuwa
gharama ya kila mita ya mraba ni elfu 17,000/ na vile vya nyumba za
ibada vitauzwa elfu 10,000 kwa kila mita ya mraba.
Kwa wale
watakaohitaji viwanja kwa ajili ya makazi maalum (housing estate) Mseli
alibainisha kuwa vitauzwa shilingi elfu 20,000 kwa kila mita ya mraba.
Naye
Meneja uhusiano wa NSSF Bi Eunice Chiume alitoa wito kwa wananchi
kutumia fursa hiyo ambayo imetolewa na shirika hilo ikiwa ni sehemu ya
mkakati wake wa kusaidia jamii na kuchangia katika maendeleo ya Taifa.
Mradi wa
NSSF (Serviced plots) uliopo kata ya Kiluvya-A Madukani Halmashauri ya
Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani una eneo lenye ukubwa wa Hekta 90.5
sawa na ekari 223.6 na una jumla ya viwanja 444 vyenye mita za mraba
465,161.
No comments:
Post a Comment