Pages
Home
HABARI
MICHEZO
BURUDANI
MATANGAZO
DINI
PICHA
SIASA
CONTACTS
UFUGAJI
KILIMO
FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA
Tuesday, November 11, 2014
LILIAN KAMAZIMA MISS TANZANIA 2014 BAADA YA SITTI MTEMVU KUJIUZURU NA KUVUA TAJI
Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza kujiuzuru kwa Sitti Mtemvu aliyekua Miss Tanzania 2014 baada ya kuzuka Sintofahamu kuhusu Umri wake, Lundenga amesema Sitti Mtemvu aliandika barua ya kujivua taji na kuiwasilisha kwa kamati ya Miss Tanzania Novemba 5 2014 ambapo kamati hiyo imeridhia kujiuzuru kwake na kumvua taji , Hivyo taji hili na majukumu ya Miss Tanzania sasa yatachukuliwa na mshindi wa pili
Lilian Kamazima aliyekaa kushoto katika picha
ambaye taratibu za Miss Tanzania zinamruhusu kuchukua jukumu hilo, Hashim Lundenga ametangaza uamuzi huo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya JB Belmonte jijini Dar es salaam leo(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Mii Tanzania 2014
Lilian Kamazima
akizungumza na waandishi wa habari kuelezea furaha yake baada ya kamati ya Miss Tanzania kumvisha taji hilo kutokana na kujiuzuru kwa Sitti Mtemvu aliyekuwa Miss Tanzania, Kulia ni Hashim Lundega Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania.
Hashim Lundega Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania akionyesha barua iliyowasilishwa kwa kamati hiyo na Bi. Sitti Mtemvu mara baada ya kujiuzuru Umiss Tanzania na kujivua taji hilo.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
TUPAMBANE BLOG
No comments:
Post a Comment