Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA
Showing posts with label miss tz. Show all posts
Showing posts with label miss tz. Show all posts

Sunday, December 28, 2014

Mashindano ya Miss Tanzania yafungwa

Mashindanoa ya Miss Tanzania
Serikali ya Tanzania imeyafungia kwa miaka miwili mashindano ya Miss Tanzania baada ya waandalizi kudaiwa kukiuka taratibu na kanuni.
Mashindano hayo yaliofunguliwa mwaka 1994 yamedaiwa kuwa na upendeleo mbali na rushwa kulingana na malalamishi yaliotolewa na wananchi pamoja na washiriki.
Kwa mujibu wa kaimu katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini Tanzania Basata , Godfrey Mngereza,kamati ya miss Tanzania ilikiuka kanuni na taratibu zinazoongoza mashindano hayo.
Alisema bwana Mgereza:"Ni kweli kwamba tumeifungia Miss Tanzania kwa miaka miwili, lakini haya si maazimio ya tathmini iliyofanyika mapema mwezi huu, bali kulikuwa na vikao mbalimbali vilivyofanyika na si kimoja, ni uamuzi mgumu ambao umekuja kutokana na sababu maalumu,"
Imedaiwa kuwa mashindano yaliyofanyika Desemba 12, mwaka huu hayakufikia uamuzi, bali vikao mbalimbali vilivyoendeshwa na wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo kwa kushirikiana na Basata ndivyo vilivyofikia hatua hiyo ili kutoa nafasi kwa waandaalizi kujipanga upya.
Baadhi ya maswala yaliobainika ni kwamba baadhi ya warembo walidaiwa kutumiwa kingono.Vilevile hakuna utaratibu wa kuwasajili warembo hao uliofuatwa kuanzia vitongojini hadi kufikia fainali.
Mngereza alisema baraza limegundua kuwa baadhi ya washiriki walichaguliwa kwa upendeleo bila ya kuwa na sifa zilizohitajika

Saturday, December 6, 2014

MISS TANZANIA AT MISS WORLD IN LONDON 2014

kkkkkkkkkkkk2kkkkkk5kkkkkkkk3kkkkkkkkk1Miss happiness is in town in time for the festive season, the she will experience the famous Christmas spirit that can be found in England’s capital city. For a little over 3 weeks, the contestants will experience the wonder of England’s vibrant multicultural metropolis whilst she takes part in the Miss World Challenge Events and prepare herself for the Big Final!
Events start from 20th November, culminating in the Grand Final on 14th December. She is in high spirit and for the first time , Tanzania has a big chance of becoming one of the big three.
Tanzanians and friends of Tanzania, there is so much you can do to help her out:
 So how does it work?
 Simply download the Miss World App, and you will find you have three slots available for your vote. Once you have decided who your top three are, you can lock in your vote and voila!, you have helped your favourite contestants on their way to being the People’s Choice Award Winner! The winner of the People’s Choice Award is announced during the latter stages of the Miss World Final, and the winner, if she is not already selected, will join the final few contestants on stage. These contestants will then face the judges questions before the winner of Miss World 2014 is announced!
                                                            How many votes do I get?
 This year, you will be allowed one set of three votes, with a bonus set of three votes if you choose to subscribe to the app, which also includes the full Miss World TV coverage of the competition. The most votes any one contestant can receive from an individual is 2 votes. Each set of votes must be for 3 different contestants.
 I can’t find the voting page on the App, am I doing something wrong?
 Voting begins on the 20th of November. Until then you will not be able to vote for your favourite contestant. This is to ensure no votes are lost if a contestant has to pull out at the last minute!
 I haven’t decided yet who my 3rd favourite is, when do I have to submit my vote?
Don’t worry! You have plenty of time to decide. The app will hold onto your choices until you make your final submission. Voting closes one hour after the start of the Miss World Final Show. Once you have submitted your votes, there is no going back, so make sure you vote right!
The time is now to support Tanzania beauty at the world stage

Wednesday, November 26, 2014

MPIGIE KURA MISS TANZANIA 2013 KATIKA SHINDANO LA MISS WORLD 2014

VOTE FOR MISS TANZANIA-MISS WORLD
VOTING HAS OPENED!
You can now register your votes for your Favourite contestants on the Miss World App, and its FREE!
Download the Miss World App on iOS & Android now and you can vote for your TOP THREE contestants in the competition. 
Voting will be open for the next 25 days, closing during the final show.
Download the App Here – http://www.missworld.com/TheCompetition/TheMissWorldMobileApp/
 ****
HAPPYNESS WATIMANYWA (MISS TANZANIA 2013/2014) ANAHITAJI KURA YAKO KATIKA KINYANG’ANYIRO CHA MISS WORLD MPIGIE KURA MISS TANZANIA HAPPYNESS WATIMANYWA. BAADA YA KUDOWNLOAD APP YA MISS WORLD NENDA VOTE FOR YOUR TOP3 KISHA UMPIGIE MREMBO MWENYE SURA HIYO HAPO KWENYE PICHA KATIKA WATATU UTAKAO WAONA
DOWNLOAD APP YA KURA  KATIKA LINK HII  HAPA CHINI

Saturday, November 15, 2014

MISS TANZANIA 2013 AAHIDI MAKUBWA MASHINDANO YA UREMBO YA DUNIA

unnamedMkurugenzi wa Lino International Agency Limited, Bw. Hashim Lundenga (kulia) akiongea na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam kuhusu safari ya Mrembo wa Tanzania wa mwaka 2013 kuelekea katika Mashindano ya Urembo wa Dunia (Miss World 2014) nchini Uingereza.
unnamed2Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano kuhusu safari ya Miss Tanzania 2013 nchini Uingereza kwenda kuiwakilisha Tanzania katika Mashindano ya Urembo wa Dunia yatakayoanza mapema tarehe 14 Desemba, 2014.
…………………………………………………………………………………………
Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM.
 
MREMBO wa Tanzania wa mwaka 2013, Happiness Watimanywa ameahidi kuing’arisha Tanzania katika mashindano ya ulimbwende ya Dunia yatakayofanyika mapema mwezi ujao huko nchini Uingereza.
 
Akiongea na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, mlimbwende huyo amewaeleza waadishi kuwa, kutokana na uzoefu wa kazi zake alizokuwa akifanya kwa jamii kwa muda kipindi cha mwaka mmoja ikiwemo misaada ya hali na mali anayoipata toka  Bodi ya Utalii Tanzania pamoja na wahisani wengine nchini amewaahidi Watanzania kuibuka na ushindi katika kinyang’anyiro hicho huko nchini Uingereza ili kuitangaza Tanzania.
 
Alieleza kuwa, tayari Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza utakuwa tayari kumpokea pindi atakapowasili nchini humo kwa lengo la kuiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo ya ulimbwende yatakayowahusisha walimbwende toka Ulimwengu  mzima.
 
“Nimejifunza mambo mengi hasa kipindi wakati nasafiri sehemu mbalimbali nchini pamoja na kufanya kazi za kusaidia jamii katika kipindi chote, hivyo nawaahidi watanzania ushindi katika mashindano hayo yatakayofanyika huko Uingereza pia mnipigie kura zenu za wingi”, alisema Watimanywa.
 
Naye Mkurugenzi wa Lino International Agency Limited, Bw. Hashim Lundenga ambao ni waandaaji wa Miss Tanzania, alisema kuwa mashindano ya Urembo wa Dunia ni mashindano ya Kimataifa ambayo yanawakutanisha walimbwende toka nchi nyingi duniani ikiwemo Tanzania, hivyo alitoa wito kwa watanzania wote kuunga mkono kwa kumpigia kura nyingi mwakilishi ambaye ndiye mrembo wa Tanzania kwa mwaka 2013, Hapinness Watimanywa ili ajinyakulie taji hilo la dunia ili aweze kuipa sifa Tanzania kimataifa.
 
Mashindano ya Urembo ya Dunia yanatarajiwa kufanyika mapema tarehe 14 Desemba, 2014 huko nchini Uingereza ambapo mrembo huyo wa Tanzania anatarajia kuanza safari yake ya kuelekea nchini humo tarehe 15 Novemba, 2014 tayari kwa ajili ya mashindano hayo.

Tuesday, November 11, 2014

LILIAN KAMAZIMA MISS TANZANIA 2014 BAADA YA SITTI MTEMVU KUJIUZURU NA KUVUA TAJI

2Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza kujiuzuru kwa Sitti Mtemvu  aliyekua Miss Tanzania 2014 baada ya kuzuka Sintofahamu kuhusu Umri wake, Lundenga amesema Sitti Mtemvu aliandika barua ya kujivua taji na kuiwasilisha kwa kamati ya Miss Tanzania Novemba 5 2014 ambapo kamati hiyo imeridhia kujiuzuru kwake na kumvua taji , Hivyo taji hili na majukumu ya Miss Tanzania sasa yatachukuliwa na mshindi wa pili Lilian Kamazima aliyekaa kushoto katika picha   ambaye taratibu za Miss Tanzania zinamruhusu kuchukua jukumu hilo, Hashim Lundenga ametangaza uamuzi huo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya JB Belmonte jijini Dar es salaam leo(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)3Mii Tanzania 2014  Lilian Kamazima  akizungumza na waandishi wa habari kuelezea furaha yake baada ya kamati ya Miss Tanzania kumvisha taji hilo kutokana na kujiuzuru kwa Sitti Mtemvu aliyekuwa Miss Tanzania, Kulia ni Hashim Lundega Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania.1Hashim Lundega Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania akionyesha barua iliyowasilishwa kwa kamati hiyo na Bi. Sitti Mtemvu mara baada ya kujiuzuru Umiss Tanzania na kujivua taji hilo.

Sunday, November 9, 2014

SINEMA YA SITTI MTEMVU YA ENDELEA.........

  • Share on facebookShare on google_plusone_shareShare on twitterShare on linkedin
Mshindi wa Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu, kwa hiari yake mwenyewe bila kulazimishwa na mtu ameamua kulivua rasmi taji hilo la urembo.
Akiongea na EATV mratibu wa shindano hilo Hashimu Lundenga amesema kuwa Sitti Mtemvu ameamua kwa maamuzi yake binafsi na sio wao kama kamati ya Miss Tanzania.
"Sababu kubwa ya Sitti kulivua taji hilo ni baada ya kuchoshwwa na maneno mengi yaliyozushwa juu yake, maana pia aliitwa na RITA kwaajili ya uchunguzi zaidi hivyo ameona mambo yanazidi kuzushwa mengi hivyo ameamua kulivua taji hilo". Amesema Hashimu Lundenga

Saturday, November 1, 2014

CAROLINE BERNARD ANYAKUA TAJI LA MISS UNIVERSE 2014

  • Written by  Tupambane Blog
  • Email
  • Tuma Maoni
  • Share on facebook Share on google_plusone_share Share on twitter 

Mrembo Caroline Bernard akipungia mkono muda mfupi baada ya kutangazwa rasmi kuwa ndio Miss Univerce 2014, katika hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip,Jijini Dar es Salaam.

Mrembo Calorine Bernard akipongezwa na washiriki wenzake

Wednesday, October 29, 2014

WAREMBO WA MISS UNIVERSE TANZANIA 2014 WAANZA KAMBI


  • Written by  Tupambane Blog
  • Email
  • Tuma Maoni
  • Share on facebook Share on gmail Share on twitter 
miss_84ef6.jpg
Warembo wa Miss Universe Tanzania 2014 wameanza rasmi kambi katika hoteli yenye hadhi ya kipekee Golden Tulip Hotel. Hii ni kwa ajili ya kujiandaa na fainali ya Miss Universe Tanzania 2014 itakayofanyika tarehe 02 mwezi Octoba.
Miss Universe Tanzania pia imeandaa mafunzo mbalimbali kwa ajili ya kuwapa warembo ili kujitambua kama vijana na kama wanawake. Mafunzo hayo yatakuwa yakitolewa na wataalamu mbalimbali toka katika Nyanja tofauti.
Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications ambaye pia ndio Mkurugenzi na Muandaaji mkuu wa Kitaifa wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai amesema usaili wa mwaka huu umefanyika katika mikoa mitano ya Tanzania na warembo zaidi ya 70 walisajiliwa kwa mashindano haya.(T.K)
Kambi ya Miss Universe Tanzania 2014 imekamilishwa na warembo 12 kutoka mikoa mitano ya Tanzania ambayo ni Arusha , Mwanza, Mbeya, Iringa na Dar es Salaam, pamoja na mrembo mmoja kutoka Zanzibar.
"Tumechagua warembo ambao wameonyesha uwezo wa kujitambua na kuelewa umuhimu wa kushiriki katika mashindano makubwa kama haya. Tuna wanafunzi wa vyuo wanaosomea udaktari, uhandisi,uhasibu na pia tuna akina dada wajasiriamali . Tunafurahi kuona kila mwaka warembo wetu wanazidi kujitambua na kazi yetu kubwa ni kuwaendeleza" alisema Sarungi
Pamoja na zawadi ya fedha taslimu, mshindi wa Miss Universe Tanzania 2014 atapata fursa ya kutangaza bidhaa mbalimbali na kufanya kazi za kijamii. Pia kama ilivyo ada kwa mwaka wa 4 sasa, mshindi atapewa nafasi (scholarship) ya kusoma New York Film Academy , Marekani. Hivi sasa washindi wa mwaka 2011 na 2012, Nelly Kamwelu na Winfrida Dominique wako New York masomoni.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania yalianza rasmi mwaka 2007 ambapo mrembo wake wa kwanza alikuwa ni Flaviana Matata ambaye mbali na kuliletea sifa Taifa bali pia amepata mafanikio makubwa katika fani ya ulimbwende kwa kuwa mwanamitindo wa kimataifa. 2008 Miss Universe Tanzania iliwakilishwa na Amanda Ole Sulul,2009 Illuminata James ,2010 Hellen Dausen , 2011 Nelly Kamwelu, 2012 Winfrida Dominique,2013 Betty Boniface ambaye ndiye anakabidhi taji kwa mshindi wa mwaka huu.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania yamedhaniwa na Insignia, MeryLight , Golden Tulip, Compass Communications, AzH Photography, Adams Digicom, Opulence, Missie Popular blog, Seif Kabelele blog, Urban Rose Hotel, RichBoys Entertainment (TZ) Ltd na New York Film Academy.

Saturday, October 25, 2014

LUDENGA AFUNGA ZAIDI KUHUSIANA NA SAKATA LA UMRI WA MISS TANZANIA 2014

  • Written by  Tupambane Blog
  • Share on facebook Share on gmail Share on twitter

Mkurugenzi wa Lino Angency International Ltd Hashim Lundenga
Hivi karibuni kulifanyika mashindano ya kumsaka mrembo wa Tanzania kwa mwaka 2014 (Miss Tanzania 2014) ambapo Sitti Mtemvu alitangazwa kuwa mshindi.
Baada ya kutangazwa huko, kukawa na mambo mengi yaliyosemwa kumhusu. Kuanzia tetesi za kuwa kadanganya umri mpaka elimu. Kuwa kuna rushwa ilitumika mpaka kusemwa ana mtoto.
Mkurugenzi wa Lino Angency International Ltd Hashim Lundenga, anazungumza na mitandai ya Vijimambo na Kwanza Production kuweka bayana KARIBU

Wednesday, October 22, 2014

LUNDENGA AOMBA VITHIBITISHO VYA MISS TANZANIA 2014

  • Written by Tupambane Blog
  • Share on facebook Share on gmail Share on twitter


Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency ambao ni waratibu wakuu wa Mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (katikati) akionyesha cheti cha kuzaliwa cha Miss Tanzania 2014 kwa wanahabari (hawapo pichani). Kushoto ni Miss Tanzania, Sitti Mtemvu.

Cheti cha kuzaliwa cha Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu.

Hashim Lundenga akiongea jambo kwa wanahabari.

Hashim Lundenga akionyesha baadhi ya hati mbalimbali za washiriki wa Miss Tanzania mwaka huu.

Afisa masoko wa Sahara, Joan John akimpatia King'amuzi cha kampuni hiyo kama zawadi kwa mshindi wa Miss Tanzania wa kwanza hadi wa tatu.

Sunday, October 12, 2014

SITTI MTEMVU ATWAA TAJI LA MISS TANZANIA 2014

  • Written by  Tupambane Blog
  • Share on facebook Share on gmail Share on twitter Share on linkedin

Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu katika pozi na mshindi wa pili, Lillian Kamazima (kulia) pamoja na mshindi wa tatu, Jihhan Dimachk baada ya kutangazwa mshindi.

MREMBO Sitti Mtemvu kutoka Temeke ametwaa taji la Miss Tanzania 2014 na kujinyakulia kitita cha milioni 18 usiku huu katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Nafasi ya mshindi wa pili imekwenda kwa Lilian Kamazima ambaye amejishindia shilingi milioni 6 huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Jihan Dimachk. Dorice Mollel ameshika nafasi ya nne wakati Nasreen Abdul akichukua nafasi ya tano.
Kwa ushindi huo, Sitti atapeperusha bendera ya Tanzania katika mashindano ya Miss World 2015.(T.K
TUPAMBANE BLOG