Matokeo ya awali ya uchaguzi wa Rais nchini Tunisia yanaonesha kuwa Beji Caid Essebsi anaongoza kwa zaidi ya asilimia 55 ya kura
Licha ya Kujitangaza mshindi, mpinzani wake ambaye ameshika nafasi ya pili Moncef Marzouki amesema matokeo hayo yanakaribiana mno.
Wakati wafuasi wa Beji Caid Essebsi wakishangilia ushindi, kiongozi wa kampeni ya uchaguzi wa Bwana Essebsi, Mohsen Marzouk, amedai ushindi.
‘’…Kulingana na matokeo ya awali kutoka katika vituo vya kupigia kura tunaweza kusema kuwa Beji Caid Essebsi ameshinda katika duru ya pili...'' Anasema Marzouk.
Hata hivyo wakosoaji wake wanasema, ushindi wa bwana Essebsi ni ishara kurudi tena uongozi usioaminika.
Lakini mwenyewe anasema ni mtendaji ambaye ataimarisha nchi hiyo.
Uchaguzi huo unaonekana kama kilele cha mageuzi ya kisiasa ambayo nchi hiyo imepitia kufuatia machafuko ya kisiasa yaliyotokea takriban miaka minne iliyopita.
No comments:
Post a Comment