Ushindi wa mara sita wa Manchester United umefikia kikomo baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Aston Villa ugenini.
Christian Benteke alikuwa wa kwanza kuifungia Villa baada ya kuvamia lango la Manchester United,lakini United ikasawazisha dakika nane tu baada ya kipindi cha pili kuanza baada ya mshambuliaji Radamel falcao kufunga kupitia kichwa likiwa bao lake la kwanza katika kilabu hiyo tangu mwezi Octoba 5.
Hatahivyo motisha wa Villa ulishushwa baada ya Agbonlahor kupewa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Ashley young.
Lakini licha ya hayo yote Villa Iliendelea kuishambulia ngome ya United na katika dakika za mwisho nusra wapate bao la ushindi kupitia Benteke.
No comments:
Post a Comment