Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Sunday, December 21, 2014

Mwanariadha wa Kenya alitumia dawa

Mwanariadha wa kenya Ritaa Jepoo aligunduliwa kutumia dawa za kusisimua misuli
Mwanariadha wa mbio za marathon raia wa Kenya Rita Jeptoo amegunduliwa kuwa alitumia dawa zinazosisimua misuli.
Shirika la riadha nchi Kenya limesema kuwa uchunguzi wa pili ulibaini kuwa mwanariadha huyo alitumia dawa hizo.
Shirika hilo linasema kuwa litasikiliza kesi hiyo mwezi Januari mwaka ujao .
Jeptoo alikuwa ameshinda mbio za Boston marathon mara tatu na za Chicago mara mbili na ni mmoja wa wanariadha maarufu zaidi nchini Kenya kupatikana na hatia ya kutumia dawa za kusisimua misuli.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG