MUME AMLIPUA KWA PETROL MKE WAKE BAADA YA KUKATAA KUPASHA MOTO CHAKULA
Matuko ya kupiga na kunyanyaswa wanawake bado yameendelea kuchukua nafasi katika nchi malimbali za Afrika.
Tumekuwa
tukiona ripoti mbalimbali za matukio mabaya ya unyanyasaji, kutoka
Kenya mwanaume mmoja amefunguliwa mashtaka baada ya jaribio la kutaka
kumuua mke wake kwa madai alishindwa kumpatia chakula cha moto.
Mwanaume
huyo Peter Muthii alimmwagia mkewe petrol akiwa amelala, akawasha moto
na kumfungia ndani ambapo muda mfupi baadaye majirani walikuja kumwokoa
na kumkimbiza hospitali.
Kisa
cha tukio hilo kimetajwa kuwa ni baada ya mwanaume huyo kurudi nyumbani
usiku na kumtaka mkewe kumpashia chakula lakini mkewe alimwambia apashe
mwenyewe kitendo kilichomkwaza, akaamua kumlipua kwa kutumia petrol
iliyokua chini ya kitanda chao.
VIJANA WATATU WALIOTAKA KWENDA IKULU WAISHIA RUMANDE DAR!
VIJANA
watatu wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA,
wamekamatwa na polisi eneo la Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam leo
Ijumaa Januari 2, 2014, baada ya jaribio lao la kufanya matembezi kutoka
mkoa wa Geita wakielekea Ikulu ya Dar es Salaam kumuona Rais Jakaya
Kikwete kufikisha malalamiko yao.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Jordan Rugimbana, vijana hao watatu,
Juma Maganga, Khalifa Selemani na Athanas Michael, walielekezwa na
maafisa usalama kumuona yeye DC baada ya kuwasili kwenye eneo lake la
utawala wakitokea Geita, ili awape baraka za kwenda Ikulu. Lakini
walipofika ofisini hapo, DC huyo alitaka kujua nini hasa kilichowafanya
watembee safari ndefu kama hiyo?
DC
Rugimbana alisema, walimweleza kuwa Mosi, Wanataka Kumnuona Rais ili
wamueleze kuchukizwa kwao na vitendo vya viongozi kula rushwa na hakuna
hatua dhabiti zinazochukuliwa dhidi yao, kukithiri kw amatumizi mabaya
ya rasilimali za taifa, kukithiri kwa vitendo vya unyanyasaji dhidi ya
raia, na kudai kurejeshwa kwa serikali ya Tanganyika.
YANGA VETERANI YATWAA KOMBE LA PSPF BAADA YA KUINYUKA SIMBA VETERANI
Nahodha wa timu ya maveterani wa Yanga, Salvatory Edward, akipokea
kombe kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam
Mayingu, baada ya kuinyuka Simba Veterani kwa penati 5-4 kufuatia sare
ya mabao 1-1 katika pambano la bonanza lililodhaminiwa na mfuko huo na
kupigwa kwenye uwanja wa Bandari Tandika, wilaya ya Temeke jijini Dar es
Salaam jioni Alhamisi Januari 1, 2015. Kufuatia ushindi huo Yanga
veterani pia walijinyakulia kitita cha shilingi milioni 1, wakati watani
wao wa jadi Simba, shilingi laki 5
MBUNGE WA MOROGORO MJINI MH ABOOD ATOA MILION 11 KUTATUA KERO YA MAJI MKUNDI MOROGORO
Mbunge
wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akizindua Tawi la CCM la
Wajasiriamali Bodaboda na Mama lishe lililopo Mgulu wa Ndege Kata Ya
Mkundi Manispaa ya Morogoro.Mara Baada ya Kuzindua Tawi Hilo Mh Abood
Aliongea na Wanachama wa Tawi Hilo Kisha Kuwaelekeza Kujiunga Kwenye
Vikundi vya Wajasiriamali Yeye Atakuwa Tayari kuwawezesha Mitaji ya
Kufanya Shuguli za Kujiletea Maendeleo.
Mbunge wa
Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akiwa Meza Kuu Sambamba na Katibu
wa CCM Kata Ya Mkundi tayari Kusikiliza Kero zinazowakabili wakati wa
Kata Hiyo Ambapo walimwambia Wanakabiliwa na Kero Kubwa ya Umeme,Maji na
Barabara.Aidha Mh Abood Akitoa Majibu Kuhusu Kero Hizo Alesema Kuhusu
Umeme Serikali Imeiweka Kata Hiyo Kwenye Bajeti ya Serikali ya Mwaka huu .Kuhusu
Maji Mh Abood alitoa Shilingi Milioni 11 Kwajili ya Kununua Vifaa vya
Kuwezesha Kufikisha Maji katika eneo la Mgulu wa Ndege Kata ya
Mkundi.Pia Alitoa Shilingi Milion 2 kwajili ya Mafuta Ili Greda la
Manispaa ya Morogoro Kuweza Kuchonga Barabarfa Zote za Kata Hiyo.
Mwenyekiti
wa Mtaa wa Mgulu wa Ndege Kata ya Mkundi Jimbo la Morogoro Mjini
Akisoma Risala yake Kwa Mbunge wa Jimbo Hilo Mh Aziz Abood.
Mmoja
wa Wakazi wa Kata ya Mkundi waliojitokeza Kwa Wingi Kwenye Ziara ya
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Akieleza Kwa msisitizo Kero Kubwa
Inayowakabili wakazi wa Kata Hiyo
Wakazi wa Kata ya Mkundi wakimsikiliza kwa Makini Mbunge wao
Wakazi wa Kata ya Mkundi wakimshangilia Mh Abood mara Baada ya Kutatua kero Kubw ya kata hiyo tatizo la Maji.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akijibu Baadhi ya Kero zinazowakabili wakazi wa Kata ya Mkundi.
NYALANDU AANZA KAMPENI ZA RAIS 2015 KANISANI, AMHUSISHA JK NA MAJINI
Isitoshe, Nyalandu aliongelea utawala wa Rais Kikwete kuwa ni utawala
unaolindwa na majini saba, ingawa hakufafanua alimaanisha nini, lakini
alishangiliwa sana na waumini wa Efata.
MKESHA WA MWAKA MPYA: KILA KONA UCHAGUZI MKUU
Makamu
wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilali akiwaongoza wakazi wa Dar es Salaam
kusherehekea Mwaka mpya katika Uwanja waTaifa, Dar es Salaam. Kulia ni
Mkuu wa Mkoa, Saidi Mecky Sadiki na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya
mkesha, Godfrey Mallase.Ujumbe
mahususi wa jinsi ya kushiriki na kuvuka salama katika Uchaguzi Mkuu wa
Oktoba ulitawala salamu za kuukaribisha mwaka 2015 zilizotolewa juzi na
viongozi wa dini na Serikali katika maeneo mbalimbali nchini.Wakati
viongozi wa dini wakijikita katika kuhamasisha haki kutendekea katika
uchaguzi na kuepuka vitendo vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani na
Makamu wa Rais, Dk Mohamed Ghalib Bilal aliwataka wananchi kuwatosa
wagombea wote watakaotumia rushwa kuwashawishi wawachague.Salamu
hizo zilianza kutolewa juzi wakati wa mkesha na Serikali
ilitahadharishwa kuzingatia haki, usawa na demokrasia katika kusimamia
uchaguzi huo ili kuepuka machafuko hasa katika kipindi cha uchaguzi huo.
OBAMA NA FAMILIA YAKE WAMESHEREHEKEA HIVI KUUPOKEA MWAKA MPYA
Sherehe
kubwa za mwaka kwa mwaka 2014 ni kama zimeisha juzi baada ya kuupokea
mwaka mpya 2015, kila mmoja kasherekea kwa aina yake, Rais wa Marekani
Barack Obama pamoja na familia yake nao walipata nafasi ya kutoka nje ya
Ikulu ya White House na kwenda kuenjoy kama watu wengine.
Vacation
ya Obama na familia yake imeendelea katika visiwa vya Hawaii, alikutana
na watu mtaani akawapa salamu za mwaka mpya; “Happy New Year,
everybody!“, akasalimiana nao halafu wakaendelea kula zao ice cream.
Picha zake na familia yake wakijienjoy hizi hapa.
DK WILLBROD SLAA NA MKEWE WAOMBEWA NA GWAJIMA KUSHINDA URAIS 2015
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima (kushoto),
wachungaji wa kanisa hilo na viongozi wengine wa ngazi ya juu,
wakimwombea Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa (katikati) na mkewe
Josephine Mushumbuzi ili aweze kufanikiwa katika harakati zake za
Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu, wakati wa ibada ya
kuukaribisha Mwaka Mpya, iliyofanyika kwenye viwanja vya kanisa hilo
Kawe, Dar es Salaam, usiku wa kuamkia jana.
DIAMOND PLATNUM NA ZARI NDANI NDIO HABARI YA MJINI TAZAMA HAPA WAKIWA RWANDA KWENYE VIBE PARTY
Staa
Diamond Platnumz ambaye jana alikuwa akipiga show kali pale nchin Rwanda
akiwa na mpenzi wake Zari the Boss Lady na kwa mujibu wa mashabiki wa
Uganda wanasema wanaona kama
Zari Hassan ndie mwanamke wa maisha ya Diamond Platinumz kutokana na
yeyekujali sana kazi za mpenzi wake ambapo wamekuwa wakisafiri kila mara
licha ya kwamba Zari anabishara zake lakin yuko Radhi kuziacha na kumpa
Company mpenzi wake, Zari ambaye amempita Diamond kwa miaka kama 15
lakin siku zote umri ni namba tu kibwa ni Penzi acha Ubuyu uendeelee
BUSH KUIONGOZA MAREKANI KAMA RAIS KWA MARA NYINGINE!
Gavana wa zamani wa Jimbo la Florida nchini Marekani Jeb Bush
ametangaza kujiuzulu mnafasi mbalimbali ambazo anashika kwenye makampuni
kadhaa pamoja na nyadhifa anazoshika kwenye bodi za taasisi mbalimbali
zisizo za kibiashara ikiwa ni ishara ya dhamira ya gavana huyo wa zamani
ya kuingia moja kwa moja kwenye mbio za kuwania urais katika uchaguzi
mkuu utakaofanyika mwaka 2016 .
Kwa mujibu wa msaidizi wa karibu wa mwanasiasa huyo , Jeb ambaye ni
mdogo wa rais wa zamani wa Marekani George Walker Bush ataangalia
uhusiano alio nao kwneye biashara tofauti katika kipindi cha mwaka mwaka
huu akiwa na lengo la kujiondoa kwenye biashara na kuingia kikamilifu
kwneye siasa akiwania nafasi ya kukiwakilisha chama cha Republican
kwenye uchaguzi wa mwakani
Jeb Bush alitangaza mwishoni mwa mwaka 2014 kuwa anafuatilia kwa
karibu mchakato wa urais japo hajaweka wazi azma yake ya kuingia kwenye
mbio hizo .
REAL MADRID NJIA NYEUPE KUMSAJILI NTO HUYU!
Kiungo
mshambuliaji wa Borrusia Dortmund Marco Reus huenda akashindwa kutimiza
ndoto yake ya kujiunga na Fc Barcelona baada ya klabu hiyo kushindwa
kwenye rufaa yake ya kupinga adhabu ya kuzuiwa kufanya usajili katika
madirisha mawili yajayo ya usajili .
Dortmund italazimika kumuuza nyota huyo ambaye ana kipengele
kinachomruhusu kuondoka endapo timu yoyote itakuja na dau la euro
milioni 25 , kipengele ambacho kitaweza kutumika baada ya kumalizReus
ambaye inafahamika wazi kuwa ataondoka Dortmund msimu ujao aliwahi
kuiahidi Barcelona kuwa atajiunga na klabu hiyo baada ya kumalizika kwa
msimu huu lakini ahadi hiyo huenda ikashindwa kutimia kwani Barcelona
wako chini ya adhabu ya Fifa ya kutosajili mchezaji yoyote kwa vipindi
viwili vya usajili baada ya kukutwa na hatia ya kukiuka kanuni za
usajili kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 18.












No comments:
Post a Comment