Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Tuesday, January 13, 2015

Katuni ya Mtume Mohammad kuchapishwa

Gazeti la Vibonzo la Charlie Hebdo
Gazeti la kila wiki la vibonzo la Charlie Hebdo la ufaransa toleo la kesho jumatano litarajiwa kuchapisha kibonzo cha Mtume Mohamed katika ukurasa wake wa mbele chini ya kichwa cha habari "Yote yameshasamehewa"
Walioona kibonzo hicho wanasema Mtume Mohammad ataonekana akishikilia bango lililoandikwa "Je suis Charlie" maneno yenye tafsiri "mimi ni Charlie, yaliyotumika kuonyesha mshikamano, baada ya shambulizi katika ofisi za gazeti hilo jumatano wiki iliyopita ambapo wafanyakazi kumi na wawili wa gazeti hilo waliuawa.
Nakala milioni tatu za gazeti hilo la kesho tayari zimeshachapishwa tofauti na kawaida ambapo huwa linachapisha nakala sitini elfu kwa wiki.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG