Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Sunday, January 18, 2015

MBEYA CITY FC YAWASHA MOTO KIRUMBA, YAICHAPA 1-0 KAGERA SUGAR


10390090_620154081464306_6013253772743772375_n

WAGONGA nyundo wa Mbeya, Mbeya City fc wameanza kurejesha makali yao baada ya kuitandika bao 1-0 Kagera Sugar katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara iliyomalizika jioni hii uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Bao hilo pekee limefungwa dakika ya 80 na Peter Mapunda.
Kikosi hicho cha Juma Mwambusi kilishangiliwa na zaidi ya mashabiki 200 waliosafiri kutoka Mbeya kuipa sapoti timu hiyo.

Ushindi wa huu ni wapili mfululizo kwani desemba 28 mwaka jana waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda fc katika mechi ya raundi ya nane ya ligi kuu kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG