Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Friday, January 9, 2015

Tanzania kushiriki gofu Brazil 2016


Mcheza gofu akiwajibika.
Chama cha gofu nchini Tanzania (TGU) kimesema kuwa kitashiriki michuano ya Olimpiki itakayofanyika huko Rio de Janeiro, Brazil mwakani.Gofu itashiriki kwa mara ya kwanza katika michuano ya Olimpiki tangu michuano ya mwaka 1904 ilipofanyika.
Ushiriki wa mchezo huo, ambao utajumuisha wachezaji wanawake na wanaume katika michezo ya mmoja mmoja (individual team) kutoka katika nchi zitakazofuzu, ulipokelewa kwa shangwe na wadau wa mchezo huo kutoka nchi mbalimbali duniani, ikiwemo Tanzania.
‘Tumejiandaa kwa muda mrefu na zaidi ya vijana 60 kutoka vilabu mbalimbali nchini wanaandaliwa ili kupata timu ya taifa kwa ajili ya michuano ya kufuzu”, alisema makamu wa raisi wa TGU, Joseph Tango
Rwanda itakuwa mwenyeki wa michuano ya Afrika ya Mashariki (kanda ya 5) itakayokuwa ni sehemu ya kufuzu na raisi huiyo wa TGU, Tango amesema Tanzania inategemewa kusafiri kwenda Kigali kwa ajili ya michuano hiyo itakayofanyika tarehe 27-30 mwezi wa kumi.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG