Bw.Mathew
alisema kuwa wakulima pamoja navijana wa kanda ya kaskazini wakiwemo
wanafunzi wa shule za sekondari,walipatana fursa ya kutembelea kituo
hicho na kuona namna inavyoendesha vipindi vyake ikiwemo kipindi cha
afya ya akili kwa vijana(Positive mood),Fahari yangu kipindi kinacho
wagusa wakulima
Alitoa wito kwa Radio zingine kuwa na utaratibu wa kuhadhimisha siku hiyo kwa kuwa itasaidia kuongeza uaminifu mkubwa na wasikilizaji kwa ujumla
Kwa upande wake Mtaalamu wa mnyororo wa dhamani kwenye mauzo ya kilimo kutoka Asasi isiyokuwa ya kiserikali la Farm Radio Bw.Terevael Aremu alisema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kusisitiza jamii kusikiliza radio hasa vipindi vya elimishi vinavyopatikana katika vituo vya radio hapa nchini na Afrika
Aidha alisema kuwa Jamii hasa wakulima wakisikiliza radio watapata elimu na taarifa mbalimbali za kile wanachokiitaji kwa wakati sahihi ikiwemo taarifa za hali ya hewa
(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Alitoa wito kwa Radio zingine kuwa na utaratibu wa kuhadhimisha siku hiyo kwa kuwa itasaidia kuongeza uaminifu mkubwa na wasikilizaji kwa ujumla
Kwa upande wake Mtaalamu wa mnyororo wa dhamani kwenye mauzo ya kilimo kutoka Asasi isiyokuwa ya kiserikali la Farm Radio Bw.Terevael Aremu alisema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kusisitiza jamii kusikiliza radio hasa vipindi vya elimishi vinavyopatikana katika vituo vya radio hapa nchini na Afrika
Aidha alisema kuwa Jamii hasa wakulima wakisikiliza radio watapata elimu na taarifa mbalimbali za kile wanachokiitaji kwa wakati sahihi ikiwemo taarifa za hali ya hewa
(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SHIRIKA LA EQUALITY FOR GROWTH (EfG) LA ZINDUA MRADI WA MSAADA WA KISHERIA KWA WAFANYABIASHARA SOKONI
Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya
Wilaya ya Lushoto, Dk.Hassan Shelukindo (katikati), akikata utepe
kuashiria uzinduzi wa mradi wa msaada wa kisheria kwa wafanyabiashara
sokoni na ofisi ya mradi huo wilayani Lushoto mkoani Tanga jana. Kushoto
ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane
Magigita na Katibu Tawala wa wilaya hiyo (DAS), Josephine Kisigila.
Mradi huo unaendeshwa na EfG.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita akitoa hutuba fupi kwa mgeni rasmi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto, Dk.Hassan Shelukindo akizungumza katika hafla hiyo.
Baadhi ya wasaidizi wa kisheria waliopatiwa mafunzo hayo.
Wanawake wa Wilaya ya Lushoto wakiwa kwenye sherehe hiyo ya uzinduzi wa mradi huo na ofisi.
Viongozi mbalimbali waliojumuika kwenye uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
Equality for Growth (EfG), Jane Magigita (mbele katikati), akiwa katika
picha ya pamoja na wasaidizi hao wa kisheria na maofisa wa EfG.
Wanahabri kutoka vyombo mbalimbali
waliokuwepo kwenye uzinduzi huo. Kutoka kushoto ni Shadrack (Channel
10), Nasra Abdallah (Tanzania Daima), Dotto Mwaibale (Jambo Leo na
Mtandao wa www.habari za jamii.com na Sophia kutoka Televisheni ya Mlimani.
Wanafunzi nao walijumuika kuona shughuli mbalimbali za uzinduzi huo hasa kikundi cha ngoma kilichokuwa kikitoa burudani.
Kikundi cha ngoma kikitoa burudani.
Zawadi zikitolewa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Jane Magigita.
Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Mary
Magigita akiwa ameshika mkungu wa ndizi aliozawadiwa. Kulia ni Katibu
Tawala wa Wilaya ya Lushoto, Josephine Kisigila.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya
Wilaya ya Lushoto, Dk.Hassan Shelukindo (kushoto), akifurahi na
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane
Magigita baada ya kukabidhiwa machapisho mbalimbali ya EfG.
Maofisa wa EfG, Eva (kushoto) na Samora wakiwa katika maandalizi ya uzinduzi huo “Chezea EfG wewe”
******
WAJASIRIAMALI wanawake wametakiwa
kutumia mafunzo ya usimamizi wa sheria katika masoko waliyopata kwa
kuwaelimisha wengine badala ya kukaa nyumbani bila ya kutoa elimu hiyo.
Mwito huo ulitolewa na Kaimu
Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto Dk.Hassan Shelukindo
wakati wa uzinduzi wa ofisi ya mradi wa msaada wa kisheria kwa
wafanyabiashara sokoni na ofisi ya mradi huo wilayani humo mkoani Tanga
jana kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo Jumanne Shauri.
“Ninyi Wanawake wa Lushoto mmepata
bahati kubwa ya kuletewa mradi huu pamoja na mafunzo haya mliyopata
nawaombeni nendeni mkayafanyie kazi katika maeneo yenu” alisema Dk.
Shelukindo
Alisema elimu waliyoipata ya msaada
wa kisheria ni muhimu sana kusaidia jamii katika masoko na itasaidia
kupunguza unyanyasaji wa kijisinsia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
Equality for Growth (EfG), ambalo linaendesha mradi huo, Jane Magigita
alisema lengo la mradi huo katika wilaya hiyo ni kuhamasisha na kulinda
haki za wafanyabiashara iwanawake katika masoko kwa kuwapatia elimu ya
sheria, biashara, elimu ya vicoba, elimu ya uongozi na usimamizi wa
vikundi.
Alisema EfG ni shirika la pekee
nchini linalotoa msaada wa kisheria kwa sekta isiyorasmi hivyo kuonesha
ni kiasi gani sekta hiyo ilivyo sahulika.
Alisema EfG inaendesha mradi huo
katika masoko ya wilaya ya Lushoto pamoja na vikundi mbalimbali vya
maendeleo na kuwa shirika hilo linawajibika kutoa mafunzo ya siku 25
kwa wasaidizi 25 ambao watasambaza huduma sheria kwa jamii.
Alisema mafunzo hayo yanatolewa kwa awamu tano ambapo kila awamu yatakuwa yanafanyika kwa takribani siku tano.
” Shirika linawajibika kutoa mafunzo
mafunzo mbalimbali kwa wafanyabiashara ikiwa na lengo la kuinua hali za
wanawake wafanyabiashara sokoni kupitia mafunzo ya biashara, uundwaji wa
vikundi vya Vicoba, mafunzo mbalimbali kwa watendaji na viongozi wa
Halmshauri ya wilaya ya Lushoto kwa lengo la kuboresha hali za
wafanyabiashara sokoni” alisema Magigita.
Alisema mpaka sasa shirika hilo
limefanikiwa kuwapatia mafunzo ya sheria ya siku tano wasaidizi wa
sheria 25, wanaume 8 na wanawake 17 kutoka katika masoko na wengine
kutoka katika vikundi vya maendeleo ndani ya Halmshauri ya Wilaya ya
Lushoto.
Alisema pia wanakituo maalumu cha
msaada wa sheria katika ofisi za EfG Lushoto ambapo wafanyabiashara
mbalimbali wanaruhusiwa kupeleka matatizo yao ya kisheria kila siku za
Jumatatu na Jumatano kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa 10 jioni.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
MBOWE:TUTAHAKIKISHA KILA MWANANCHI AMEJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA MPIGA KURA LAKINI KWA UPANDE WA KATIBA MSIMAMO WETU KAMA UKAWA UKO PALE PALE WA KUTOSHIRIKI
Mwenyekiti wa Chadema Freman Mbowe akiwa anasoma utuba wakati wa ufunguzi wa mkutano wa viongozi wa chama hicho wa kanda ya kaskazini unaofanyika leo katika hotel ya new Arusha jijini hapa |
viongizo wa chadema akiwemo mwenyekiti wakiwa wanasali kwanza kabla ya mkutano wa viongozi wakanda ya kaskazini kuanza
Naibu katibu mkuu wa Chadema Salum Mwalimu akiwa anaongea nawaandishi wahabari
MWENYEKITI wa chama cha
demokrasi na maendeleo Chadema Freeman Mbowe amesema kuwa chama chao
kimejipanga kuahakikisha kinahamasisha kwa nguvu zote wananchi weweze
kwenda kujiandikisha katika daftari la mpiga kura
Alisemakuwa hii itaweza kumsaidia
kila mwananchi kuweza kupata haki yakumchagua kiongozi bora anaemtaka
katika uchaguzi mkuu ujao wa kuwachagua viongozi wakuu ambao ni rais
,wabunge na madiwani.
Alisema kuwa pamoja ya kuwa tume
wamekuwa wananchelewesha kufanyika kwa zoezi hili , wao wamejipanga
kikamilifu na pindi ambapo zoezi hili litatangazwa kuanza rasmi
watajitaidi kwa njia yoyote kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi
kujiandikisha
Alisema kuwa kwa upande wa kupiga kura
katiba wanaendelea na msimamo wao ambao walitangaza awali wa kutoshiriki
katika mchakato wa kura ya maoni ya katiba huku akisisitiza kuwa swala
la kutoshiriki katika mchakato wakura za maoni auingiliani kabisa na
kuhamasisha wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga
kura
Alimaliizia kwa kuwasihi wananchi
wajitokeze kwa wingi sana pindi pale ambapo watasikia zoezi la
kujiandikisha kwenye daftari la kudumu limewadia ili waweze kupata haki
yao ambayo itawaruhusu kuchgua kiongozi wanao wataka.
habari kwa hisani ya libeneke la kaskazini blog
No comments:
Post a Comment