Mchezaji wa timu ya taifa ya England ambaye pia anakipiga katika klabu ya soka Sunderland Adam Johnson amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kufanya mapenzi na msichana mwenye umri wa miaka 15. Polisi katika eneo la Durham wamesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amekamatwa mapema wiki hii kwa tuhuma za kufanya ngono na binti mwenye umri wa chini ya miaka 16, na amebaki chini ya ulinzi. Taarifa ndani ya klabu yake zinasema kuwa mchezaji huyo amesimamishwa kusubiri matokeo ya uchunguzi wa polisi. Taarifa za kukamatwa kwake zilitolewa mapema kupitia gazeti la The Sun. Kukamatwa kwake kunakuja muda mfupi kabla hajasafiri na timu yake ya Sunderland kwenda kukutana na Hull kwa michezo ya Ligi kuu ya England iliyopangwa kuchezwa leo usiku. Sunderland imesema haitaendelea kuzungumzia kukamatwa kwa mchezaji wake.
Nako nchini Tanzania, timu ya Azam iliyokuwa ikishiriki michuano ya klabu bingwa barani Afrika, imemtimua kocha wake Mcameroon Joseph Omog baada ya kutolewa katika mashindano hayo pale ilipochapwa mabao 3-0 katika mchezo wa marudiano na El Mereikh nchini Sudan mwishoni mwa wiki. Azam ilishinda mchezo wa kwanza dhidi ya El Mereikh kwa kuicharaza mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita. Azam iliyaaga mashindano hayo kwa kuchapwa jumla ya magoli 3-2.
No comments:
Post a Comment