Utafiti umeonesha kuwa watu wanaofanya mazoezi ya kila mara wanaishi kwa miaka mitano zaidi ya wale ambao hawafanyi mazoezi yeyote.
Aidha utafiti huo uliowajumuisha watu waliokomaa umebaini kuwa watu walio na umri mkubwa wanaishi maisha marefu zaidi pindi wanaoacha kuvuta sigara.
Utafiti huo wa miaka 11 uliwajumuisha watu wazima 5,700 nchini Norway ulidhibitisha kuwa watu waliofanya mazoezi kwa takriban saa tatu kwa juma wanaishi zaidi ya miaka mitano zaidi ya wale ambao hawakufanya mazoezi yeyote.
Wanasayansi hao wameanzisha kampeini za uhamisisho wa faida za kufanya mazoezi hasa kwa watu wazima.
Wakiandika katika jarida moja la utabibu wa michezo linalochapishwa nchini Uingereza, wanasayansi hao wanasema kuwa maisha ya
kuketi bila ya kuwa shughuli yeyote inayochemsha damu mwilini inachangia pakubwa kuzorota kwa uwezo wa mwili kuhimili dhoruba ya maambukizo tofauti tofauti haswa mtu anapozeeka.
Chuo kikuu cha Oslo kilithibitisha kufuatia utafiti huo kuwa hata mtu akifanya mazoezi mepesi ni kheri kuliko kukosa mazoezi kabisa.
Takwimu za utafiti zinaonyesha kuwa japo watu wenye umri zaidi ya miaka 65 wakishiriki mazoezi yeyote kwa dakika 150, hiyo itatosha kumweka katika hali nzuri ya kiafya.
Aidha kwa wale wenye umri kati ya miaka 68 hadi 77 wanahitaji kufanya mazoezi kwa zaidi ya saa moja kwa juma ilikupata manufaa yake.
Kwa ujumla asilimia 40% ya washirika waliofanya mazoezi kwa takriban nusu saa kila siku walikuwa bado hai katika utafiti huo uliodumu kwa miaka 11.
Ripoti hiyo iliongezea kusema kuwa hata wale wazee waliokuwa na miaka 73 walipoanza mazoezi asilimia kubwa ilikuwa hai zaidi ya wenzao ambao hawakufanya mazoezi yeyote.
No comments:
Post a Comment