Wakati
wa Mkutano Mkuu wa CCM jana mjini Dodoma, Chama cha Demokrasi na
Maendeleo (CHADEMA) kiliwapoteza wanachama wake watatu baada ya
kutangaza rasmi kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Wanachama
hao waliokihama chama hicho ni Fred Mpendazoe ambaye alikuwa mwanachama
wa CCM pia aliwahi kuwa Mbunge wa Kishapu mwaka 2005 hadi 2010 kupitia
CCM, Mgana Msindai aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida na mbunge
wa zamani wa Iramba Mashariki na mwigizaji wa filamu nchini Tanzania
Jackline Wolper.
Mmoja
wa wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA alipohojiwa jana wakati kikao cha
Kamati Kuu ya chama hicho kinaendelea alisema kuwa, hawana muda wa kukaa
na kuanza kumjadili mtu mmoja mmoja anayesemekana kuhama chama hicho
"Kamati
Kuu ni kikao kizito sana, hatuwezi kuacha kujadili masuala ya msingi na
kuanza kuwajadili hao wanaosemekana kuwa wamehama chama," alisema mjumbe huyo.
No comments:
Post a Comment