Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Thursday, July 28, 2016

Mastaa waliotikisa kwa skendo za mapenzi 2015

Diamond platinumz (2)Mladness Mallya
MWAKA unaelekea ukingoni, kuna mengi yametokea ndani ya mwaka huu wa 2015 katika jamii yakiwemo mazuri na mabaya.
Kama ilivyo kawaida katika ulimwengu wa mastaa hakukosekani vituko vya hapa na pale, leo katika makala haya tunakuletea mastaa mbalimbali waliotikisa kwa skendo za mapenzi, yaani waliokuwa na misuguano na wengine kutajwa kubadili wapenzi kila kukicha.
DIAMOND NA ZARI
Staa huyu wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na mzazi mwenziye Zarinah Hassan ‘Zari,’ walitikisa mwaka huu kwa kupamba vyombo mbalimbali vya habari hasa pale walipopata mtoto Tiffah ambaye ilisemekana siyo mtoto wa msanii huyo na kutajwa kuwa ni wa mume wa zamani wa Zari, Ivan Semwanga na wengine wakidai ni wa pedeshee Muzamil Katunzi, skendo hii ilitikisa lakini Diamond akashikilia msimamo wake kwamba mtoto ni wa kwake.
Wawili hao pia walidaiwa kwamba baada ya kupata mtoto mkataba ulikwisha na sasa Zari anaishi kwake huko Afrika Kusini, hii ilitokana na kushindwa kuishi na mama Diamond kwani alidai familia hiyo ina mambo ya Kiswahili ambayo hakuweza kuyakabili.
NAYNAY NA SHAMSA
Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ msanii wa muziki wa Bongo Fleva na Shamsa Ford ambaye ni msanii wa filamu ishu yao ya kuwa wapenzi ilitikisa sana ikiwa ni muda mfupi tu baada ya Nay kuachana na mzazi mwenzake, Siwema Edson ambapo ilisemekana mapenzi yake na Shamsa yalikuwepo hata kabla hajaachana na mwanamama huyo.
Nay hakuishia hapo, baada ya kutajwa kuwa kwenye uhusiano na Shamsa pia alinaswa na msanii wa Bongo Fleva, Pam D wakiwa kwenye pozi tata la kimapenzi na baada ya hapo hivi karibuni akahamia kwa mrembo kutoka  Marekani, Stella Tilya ‘Chaga Baby’.
WEMA17WEMA SEPETU NA 
LUIS MNANA
Mrembo huyu asiyeishiwa matukio, mwaka huu aliingia kwenye vichwa vya habari kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mshiriki wa Big Brother Africa (BBA)ambaye ni raia wa Namibia, Luis Mnana na kufanikiwa kumbadilisha dini na kuwa Muislamu ili waweze kufunga ndoa.
Kwa bahati mbaya wawili hao hawakuweza kufikia kufunga ndoa, waliachana na sasa kila mmoja yupo na maisha yake.

kiba na jokateeJOKATE NA ALI KIBA

Wawili hawa wamesumbua sana mwaka huu kwani ni wapenzi ambao walikuwa wakionekana pamoja sehemu mbalimbali za starehe.
Penzi hili limekuwa na misukosuko kwani wazazi wa Jokate hawapendi awe na Ali Kiba hata wale wa upande mwingine hawampendi mwanadada huyo.
lulunacheniLULU NA CHENI
Wasanii hawa wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ walitikisa na skendo ya kutaka kuoana ambapo kila mmoja alifunguka lake.
Wawili hao mpaka sasa haijulikani kinachoendelea kuhusu ndoa licha ya Mama Lulu kukubali mwanaye aolewe Kiislamu.
maso-davidAGNES MASOGANGE NA DAVIDO
Mwanadada huyu ambaye ameonekana kwenye video mbalimbali za wasanii wa Bongo Fleva, mwaka huu alitikisa na skendo ya kutoka kimapenzi na Mwanamuziki wa Nigeria, Davido.
Pamoja na kuwa na msanii huyo pia alikumbwa na skendo ya kuvunja amri ya sita na wanaume wawili kwa wakati tofauti kwenye hoteli moja ya Ramada, Dar.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG