Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA
Showing posts with label DIAMOND. Show all posts
Showing posts with label DIAMOND. Show all posts

Thursday, July 28, 2016

Mastaa waliotikisa kwa skendo za mapenzi 2015

Diamond platinumz (2)Mladness Mallya
MWAKA unaelekea ukingoni, kuna mengi yametokea ndani ya mwaka huu wa 2015 katika jamii yakiwemo mazuri na mabaya.
Kama ilivyo kawaida katika ulimwengu wa mastaa hakukosekani vituko vya hapa na pale, leo katika makala haya tunakuletea mastaa mbalimbali waliotikisa kwa skendo za mapenzi, yaani waliokuwa na misuguano na wengine kutajwa kubadili wapenzi kila kukicha.
DIAMOND NA ZARI
Staa huyu wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na mzazi mwenziye Zarinah Hassan ‘Zari,’ walitikisa mwaka huu kwa kupamba vyombo mbalimbali vya habari hasa pale walipopata mtoto Tiffah ambaye ilisemekana siyo mtoto wa msanii huyo na kutajwa kuwa ni wa mume wa zamani wa Zari, Ivan Semwanga na wengine wakidai ni wa pedeshee Muzamil Katunzi, skendo hii ilitikisa lakini Diamond akashikilia msimamo wake kwamba mtoto ni wa kwake.
Wawili hao pia walidaiwa kwamba baada ya kupata mtoto mkataba ulikwisha na sasa Zari anaishi kwake huko Afrika Kusini, hii ilitokana na kushindwa kuishi na mama Diamond kwani alidai familia hiyo ina mambo ya Kiswahili ambayo hakuweza kuyakabili.
NAYNAY NA SHAMSA
Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ msanii wa muziki wa Bongo Fleva na Shamsa Ford ambaye ni msanii wa filamu ishu yao ya kuwa wapenzi ilitikisa sana ikiwa ni muda mfupi tu baada ya Nay kuachana na mzazi mwenzake, Siwema Edson ambapo ilisemekana mapenzi yake na Shamsa yalikuwepo hata kabla hajaachana na mwanamama huyo.
Nay hakuishia hapo, baada ya kutajwa kuwa kwenye uhusiano na Shamsa pia alinaswa na msanii wa Bongo Fleva, Pam D wakiwa kwenye pozi tata la kimapenzi na baada ya hapo hivi karibuni akahamia kwa mrembo kutoka  Marekani, Stella Tilya ‘Chaga Baby’.
WEMA17WEMA SEPETU NA 
LUIS MNANA
Mrembo huyu asiyeishiwa matukio, mwaka huu aliingia kwenye vichwa vya habari kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mshiriki wa Big Brother Africa (BBA)ambaye ni raia wa Namibia, Luis Mnana na kufanikiwa kumbadilisha dini na kuwa Muislamu ili waweze kufunga ndoa.
Kwa bahati mbaya wawili hao hawakuweza kufikia kufunga ndoa, waliachana na sasa kila mmoja yupo na maisha yake.

kiba na jokateeJOKATE NA ALI KIBA

Wawili hawa wamesumbua sana mwaka huu kwani ni wapenzi ambao walikuwa wakionekana pamoja sehemu mbalimbali za starehe.
Penzi hili limekuwa na misukosuko kwani wazazi wa Jokate hawapendi awe na Ali Kiba hata wale wa upande mwingine hawampendi mwanadada huyo.
lulunacheniLULU NA CHENI
Wasanii hawa wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ walitikisa na skendo ya kutaka kuoana ambapo kila mmoja alifunguka lake.
Wawili hao mpaka sasa haijulikani kinachoendelea kuhusu ndoa licha ya Mama Lulu kukubali mwanaye aolewe Kiislamu.
maso-davidAGNES MASOGANGE NA DAVIDO
Mwanadada huyu ambaye ameonekana kwenye video mbalimbali za wasanii wa Bongo Fleva, mwaka huu alitikisa na skendo ya kutoka kimapenzi na Mwanamuziki wa Nigeria, Davido.
Pamoja na kuwa na msanii huyo pia alikumbwa na skendo ya kuvunja amri ya sita na wanaume wawili kwa wakati tofauti kwenye hoteli moja ya Ramada, Dar.

Mastaa waliotikisa kwa skendo za mapenzi 2015 Diamond platinumz (2)

Mastaa waliotikisa kwa skendo za mapenzi 2015

Diamond platinumz (2)Mladness Mallya
MWAKA unaelekea ukingoni, kuna mengi yametokea ndani ya mwaka huu wa 2015 katika jamii yakiwemo mazuri na mabaya.
Kama ilivyo kawaida katika ulimwengu wa mastaa hakukosekani vituko vya hapa na pale, leo katika makala haya tunakuletea mastaa mbalimbali waliotikisa kwa skendo za mapenzi, yaani waliokuwa na misuguano na wengine kutajwa kubadili wapenzi kila kukicha.
DIAMOND NA ZARI
Staa huyu wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na mzazi mwenziye Zarinah Hassan ‘Zari,’...

Friday, August 7, 2015

Diamond na Zari wajaliwa mtoto wa kike

Diamond Platinumz
Msanii wa Bongo mwenye umaarufu wa kimataifa, Diamond Platnumz, maarufu, Naseeb Abdul, amepata majukumu mapya baada ya kujaliwa mtoto.
Mkewe msanii huyo, Zarina Hassan, Zari the boss lady, alijifungua msichana mapema leo na kuipa furaha familia hiyo.
Baada ya kuokota tuzo tofauti kwenye mziki, Diamond hatimaye amepata tuzo kutoka kwa Mungu kwa kufanya juhudi nyingi za kutaka kuwa mzazi.
Diamond alipachika picha ya mtoto wake akibebwa na mamake, Sanura Kassim kwenye ukurasa wake wa Instagram na kupokea pongezi kutoka mashabiki.
Aidha, msanii huyo amemuanzishia mtoto wake ukurasa wa Instagram kwa jina Tiffah Dangote na kuvutia zaidi ya wafuasi elfu kumi na sita.
Diamond mwenye umri wa miaka 25, aliwashangaza wengi kwa kuanza kumfanyia bintiye ununuzi wa vifaa vya watoto kabla ya kuzaliwa.

Saturday, April 4, 2015

DIAMOND THE PLATNUMZ WAFUNGA NDOA NA ZARI


 
 NI KWELI diamondplatnumz WAMEFUNGA NDOA??  UNAKUPA UBUYU KIDOGO -----Kwa imani ya watu wengi, huenda kuanzia Ijumaa ya jana, Zari ni Mrs Naseeb rasmi! Apparenty wawili hao wamefunga ndoa kimya kimya ama

 kuchumbiana – ofcourse kwa mujibu wa picha aliyopost Diamond kwenye Instagram usiku wa jana..na kucaption hivi--- “Wakati Mwingine Usiri Unabaraka zaid

Friday, September 5, 2014

DIAMOND AELEZA ALIVYODHALILISHWA

  • Written by Tambane Blog
  • Email
  • Maoni (1)
  • Share on facebook Share on google_plusone_share Share on twitter 

Stori: Shakoor Jongo
SIKU chache baada ya kufanyiwa fujo katika shoo yake nchini Ujerumani, staa wa Mdogo Mdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ameibuka na kueleza namna ambavyo alidhalilishwa nchini humo.
Diamond aliponea chupuchupu kupewa kipigo baada ya kuchelewa kwenye shoo iliyokuwa ifanyike katika Ukumbi wa Sindelfingen katika mji wa Stuttgart, Ujerumani.

Staa wa Mdogo Mdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Akizungumza na paparazi wetu baada ya kutua Bongo Jumanne iliyopita, Diamond alisema anasikitika kwani alidhalilishwa wakati alipokuwa akidai haki ya kumaliziwa malipo yake ya shoo euro 250 (zaidi ya sh 500,000).GPL(P.T)
“Inaniuma sana kwani mimi pale nilikuwa nasimamia haki yangu, kwani nilikuwa nawadai euro 250 sasa nikaona wananizungusha na nilipokomaa zaidi huku wakiona muda wa shoo unapita, ndipo walipoanza kunitukana bila sababu.
“Wamenitukana mimi, wamewatukana hadi ndugu zangu ambao hawakuhusika na chochote na wala hawakuwepo kule. Wamenidhalilisha bila kosa. Kimsingi sikutaka kupanda jukwaani pasipo kumaliziwa fedha zangu licha ya kuwa si nyingi kiivyo,” alisema mtoto huyo wa Tandale.

Hali halisi ya ukumbi nchini Ujerumani ulivyoharibiwa na mashabiki waliovurugwa kwa kucheleweshewa shoo ya Diamond.
Kwenye maelezo menginena paparazi wetu, Diamond alisema baada ya kutokea vurugu hizo alilazimika kurejea nchini pasipo kumaliziwa fedha zake lakini promota wa shoo hiyo, Kamabritts aliahidi kuandaa shoo nyingine ya bure ili kujisahihisha kwani kosa lilikuwa la kwake.
Kwenye mvutano huo kati ya msanii na promota huyo, Diamond alitegemewa kupanda jukwaani saa nne usiku lakini ilishindikana hadi ilipofika saa 10 alfajiri kitendo ambacho kilisababisha mashabiki wafanye vurugu kwa kuvunja viti na thamani nyingine za ukumbi zinazokadiriwa kufikia Euro 128,222 (Sh. milioni 280).
TUPAMBANE BLOG