Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA
Showing posts with label AJALI. Show all posts
Showing posts with label AJALI. Show all posts

Sunday, October 4, 2015

TAARIFA KUHUSU NDEGE YA JESHI ILIYOPATA AJALI


NDEGE ya mafunzo ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), imepata ajali ikiwa na marubani wawili katika eneo la Silversands, Visiwa vya Bundya, katika Mwambao wa Bahari ya Hindi Kaskazini Mashariki mwa Jiji la Dar es Salaam.Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano, Makao Makuu ya Jeshi, Upanga, ilisema marubani hao wanaendelea kutafutwa baada ya kuzama habarini.
Tukio hilo limetokea Oktoba mosi, mwaka huu, saa tatu 3:30 asubuhi ambapo marubani waliopotea ni Luteni Kanali Talkisiyo Ndongoro na Kapteni Gaudence Hamis.
Chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu ya injini ambapo baada ya marubani kugundua hitilafu hiyo, walifanya juhudi za kujiokoa kwa kutoka katika ndege, kuangukia baharini na kuzama. 

VIJANA SITA WA JKT BULOMBORA KIGOMA MAPOTEZA MAISHA,21 WAJERUHIWA KATIKA AJALI


VIJANA sita waliokuwa katika mafunzo ya kijeshi ya kujitolea katika kikosi cha 821 JKT Bulombora mkoani Kigoma wamefariki dunia na wengine 21 kujeruhiwa vibaya kutokana na ajali ya gari iliyotokea jioni hii.
Mganga Mfawidhi wa hospital ya mkoa wa Kigoma Dkt. Fadhil Kibaya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
"Ni kweli leo majira ya saa moja jioni tumepokea miili minne ya vijana wa JKT ambao waliletwa hapa tayari wamefariki na majeruhi 21. "Wengine wawili wamefariki hapa hapa wakati tukiendelea kuwapa huduma"alisema Dkt Fadhili.
Alisema hali za majeruhi mpaka sasa siyo nzuri sana kwani wengi wameumia sehemu za kichwa na mwilini. "Bado tunaendelea na jitahada za kuwapatia matibabu na majina ya waliopoteza maisha pamoja majeruhi tutatoa kesho, sababu majeruhi wengi hawana fahamu"alisema.
Naye kamanda wa polisi mkoa wa kigoma Afande Ferdinand Mtui alisema chanzo cha ajali hiyo ni gari hilo la jeshi kushindwa kupanda mlima na kusababisha tairi mbili za nyuma kupasuka.
Alisema ajali hiyo imetokea katika eneo la Kasaka karibu na mizani ambapo lori hilo la jeshi lilikuwa likitoka mjini kwenda kambini likiwa limebeba makreti ya soda na unga.

Credit: Michuzi

Wednesday, July 8, 2015

MKUU WA HIFADHI YA RUAHA APATA AJALI


Mkuu wa hifadhi ya Ruaha Christopher Timbuka Apata ajali hifadhi ya Mikumi akiwa safarini kuelekea Jijini Dar es salaam na Familia yake. Chanzo cha ajali ni tairi la mbele kuchomoka hakuna aliyepoteza maisha. Kwa sasa wanaendelea na matibabu katika hospital ya St Kizito Mikumi.

Thursday, April 23, 2015

Watu 10 Wafariki Dunia Baada ya Basi la kampuni ya Unique Kugongana na Gari la Coca Cola


Habari zilizotufikia zinaarifu kuwa basi la Unique lenye namba za usajili T148 BKK likitokea jijini Mwanza kwenda Tabora limegongana uso kwa uso na lori la kampuni la Cocacola katika kijiji cha Ibingo kata ya Samuye Shinyanga.
Watu 10 wamefariki na 50 wamejeruhiwa.Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.



Sunday, April 19, 2015

AJALI! AJALI! :, WATU 24 WAMEPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA HIACE KUKATA BREAK MKOANI MBEYA MAPEMA LEO


MIILI YA WALIOKUWA ABIRIA
MUONEKANO WA GARI
Ajali ya Hiace imeua watu 24 eneo la Uwanja wa ndege Kiwila Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya.
Wadau Niko eneo la tukio, mpaka sasa miili 22 imefanikiwa kutolewa. Kwani Hiace hii ilidumbukia mtoni na bado miili miwili imenaswa, ndo inatolewa muda huu.
Watu wawili tu ndio wamepona akiwemo kondakta. Ajali hii imetokea wakati Coaster zinazofanya safari zake kati ya Mbeya na Kyela kugoma hivo baadhi ya hiace za mjini kuamua kubeba abiria. Inaonekana ni ugeni Wa barabara, speed na gari kukosa break za kuaminika.Inauma sana.

Friday, March 20, 2015

GARI LA LUINZO LAGONGANA USO KWA USO NA GARI LA MSANGA EXPRESS NA KUUWA WATU WANNE

Watu wa nane wamefariki Dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia ajali ya Basi la Luinzo lililokuwa likitokea njombe kwenda DSM kugongana na gari la Msanga EXPRESS lililokuwa likitokea morogoro kwenda Mahenge wakati likijaribu kulipita lori lililokuwa mbele yake katika Eneo la hifadhi ya Mikumi Barabara ya Iringa Morogoro hapo jana.



Thursday, February 12, 2015

Ajali ya moto katikati ya Jiji la Dar es Salaam


Taarifa kutoka katikati ya Jiji Dar es Salaam, hali haikuwa shwari leo asubuhi, tukio kubwa ni ajali ya moto ambao ulianza katika majengo yanayomilikiwa na Shirika la Nyumba NHC.Moto ulianza saa tatu asubuhi mtaa wa Libya na Mosque, ambapo ulishika katika majengo matatu ya ghorofa yaliyoongozana na kuunguza vitu ambavyo thamani yake haijafamika.Vikosi vya Zimamoto vilifika na kuudhibiti moto huo huku wakiendelea na uchunguzi kujua chanzo cha moto huo.
Kamanda wa Polisi Suleiman Kova amesema hakuna mtu aliyefariki wala kuumia kutokana na ajali hiyo.
Hapa kuna picha za tukio hilo.















Friday, January 16, 2015

AJALI MBAYA YATOKEA MAENEO YA MKATA,DEREVA ANUSURIKA KUFARIKI

 Gari ndogo ikiwa imeharibika vibaya baada ya kugongana na Basi la Meridian
 Wasamaria wema wakinasua dereva wa gari ndogo

Dereva wa Gari ndogo akiwa haamini kama amepona
 Ajali hii imehusisha basi la abiria la Meridiani pamoja na gari ndogo binafsi.Dereva wa gari binafsi amenusurika kifo baada ya gari yake kuharibika vibaya.
 Ajali hii imetokea maeneo ya Mkata barabara ya kwenda mikoa ya Kaskazin

Sunday, January 4, 2015

AJALI ENEO LA KIBADA, KIGAMBONI JIJINI DAR

Magari mawili madogo yakiwa yamegongana eneo la Kibada, Kigamboni jijini Dar es Salaam jana.


Wananchi wakiwa eneo la tukio baada ya ajali hiyo.



Taswira kutoka eneo la ajali hiyo.
AJALI hii iliyoyahusisha magari mawili madogo ilitokea jana majira ya saa 11 jioni eneo la Kibada, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Msichana anusurika ajali ya ndege




Ajali ya ndege
Mtoto mmoja wa miaka saba ametembea hadi katika nyumba moja katika jimbo la Kentucky nchini Marekani ili kuripoti kuanguka kwa ndege aliyoabiri.
Kulingana na polisi ndege hiyo baadaye ilipatikana imeanguka huku watu wanne wakiwa wamefariki katika kaunti ya Lyon yapata kilomita 50 mashariki mwa mji wa Paducah
Kituo cha runinga cha NBC nchini Marekani kimesema kuwa msichana huyo alimwarifu mtu aliyemfungulia mlango kwamba wazazi wake walifariki katika ajali hiyo ya ndege.
Picha ya ndege hiyo haijatolewa na polisi hawajatoa tamko lolote kuhusu uhusiano wake na waathirwa.
Shirika linalosimamia anga za juu limesema kuwa maafisa wanaodhibiti usafiri wa ndege walipoteza mawasiliano na ndege hiyo aina ya Piper PA-34 baada ya rubani kuripoti matatizo ya mitambo.

Wednesday, December 31, 2014

Ndege iliyopotea: Utafutaji wachelewa

Ndugu wa abaria waliopotea kwenye ndege ya AirAsia wakilia kwa uchungu
Hali mbaya ya hewa imechelewesha zoezi la anga na majini la utafutaji wa ndege ya AirAsia aliyoanguka ikiwa na watu 162 baada ya kuwepo kwa dhoruba katika pwani ya eneo la Borneo siku ya jumapili.
Kufuatia kupatikana kwa vipande vya mabaki ya ndege hiyo siku ya jumannne, kiongozi wa taasisi ya uokoaji na utafutaji amesema miili mitatu imepatikana hadi sasa kutoka katika eneo la bahari ya Java.
Wapiga mbizi wa kikosi cha maji cha jeshi wanatarajiwa kuanza kutafuta miili na kinasa sauti cha ndege hiyo katika kina cha chini cha maji katika eneo linalosadikiwa ndipo ndege hiyo ilipoangukia.
Ndege hiyo ilipotea ikiwa safarini ikitokea mji wa Surabaya nchini Indonesia kuelekea nchini Singapore.

Miili 40 yaopolewa baharini

Sala za kuwaombea waliokuwa wasafiri katika ndege hiyo zinaendelea
Kufuatia kupotea kwa ndege ya shirika la ndege la Asia ndege namba QZ8501At ,miili arobaini imeopolewa kutoka baharini katika utafutaji wa mabaki ya ndege hiyo na utafutaji unaendelea.
Miili hiyo ilionekana ikielelea karibu na taka za bahari pwani ya Indonesia,eneo la Borneo moja ya eneo la utafutaji mabaki ya ndege hiyo.Na taarifa kutoka serikali ya Indonesia zimethibitisha kwamba miili hiyo inatoka katika ndege iliyopotea.
Ndege hiyo aina ya Airbus A320-200,ilikuwa imebeba abiria mia moja na sitini na wawili ikitokea Surabaya nchini Indonesia kuelekea Singapore,ilipotea siku ya Jumapili.
Utafutaji wa mabaki ya ndege hiyo umeingia katika siku ya tatu,na eneo la utafutaji limeongezwa na kufikia kanda kumi na tatu hii inashirikisha nchi kavu na baharini.
Wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliooneshwa wazi kwenye runinga ya taifa la Indonesia picha za taka bahari zilioneshwa zikiwa zimechanganyika na mabaki ya miili ya abiria ikielea majini.
Ndugu wa mabaki hayo walipoona picha hizo walipigwa na fadhaa kuu na walionekana kushtushwa na picha hizo.Baadaye askari wa majini nchini Indonesia wameeleza kuwa miili hiyo arobaini iliopolewa na meli ya kivita .
Mkurugenzi mtendaji wa AirAsia Fernandes ali ingia katika mtandao wa twitter na kueleza huzuni yake kwa ndugu waliopoteza ndugu zao katika ndege QZ 8501. Na kwa niaba ya shirika la ndege la AirAsia ametuma salamu za rambi rambi .
Utafutaji miili na mabaki ya ndege hiyo unashirikisha meli thelathini,ndege kumi na tano na chopa saba.
TUPAMBANE BLOG