Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA
Showing posts with label MSANII. Show all posts
Showing posts with label MSANII. Show all posts

Thursday, July 2, 2015

BANZA STONE AWASHANGAA WANAO MZUSHIA KIFO(VIDEO)


Mwimbaji wa mkongwe kwenye muziki wa dance Tanzania Banza Stone alikutana na Waandishi wa habari wachache kwa ajili ya kukanusha taarifa za kuzushiwa kifo, maisha yake kwa sasa na kilichokua kinamsumbua kiafya.

Tuesday, May 12, 2015

MDOGO WAKE ADEBAYOR MIKONO JUU…AOMBA MSAMAHA YAISHE


Ndugu wa mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Emmanuel Adebayor ameomba msamaha baada ya nyota huyo kumshtumu katika mtandao wa Facebook na watu wengine wa familia yake.
Rotimi Adebayor ameiambia BBC kwamba anaomba msamaha kwa makosa aliyofanya na kwamba angependa nduguye arudi katika familia.
Emmanuel Adebayor ambaye pia anaichezea Togo alisema wiki iliopita kwamba mzigo wa kifedha wa kuisadia familia yake pamoja na ugomvi katika familia yake umemuahiribia kazi yake.
Amesema kuwa anazitaka familia nyungine barani Afrika kupata funzo kutoka kwenye hili ishu. Kama unakumbuka kwamba Rotimi alitajwana Adebayor kwa matatizo ya kuwa mwizi wa vitu vya nyumbani pamoja na kwa rafiki zake.

Thursday, April 23, 2015

MTANZANIA MAYUNGA ALIVYOZIMIA KENYA BAADA YA KUTAJWA MSHINDI AIRTEL TRACE MUSIC STAR



Mtanzania Nlimi Maunga alizimia kwa furaha wakati akiimba mara baada ya kutangazwa mshindi wa Airtel Trace Afrika na kuwaacha hoi washiriki wengine 12 kutoka nchi za Afrika katika fainali zilizofanyika Naivasha, Kenya mwishoni mwa wiki.
Akon akimpongeza mayunga kwa kuibuka mshindi wa Airtel Trace Music Stars katika shindano la Afrika lililofanyika Naivasha Kenya
Nalimi Mayunga akiimba wakati wa fainali ya shindano la Airtel Trace Music Star la Afrika lililofanyika Naivasha Kenya
Mashabiki kutoka Tanzania wakipepea bendera ya kumshangilia mwakilishi wao Nalimi Mayunga wakati wa shindano la Airtel Trace Music Stars
21 Apr 2015 

Saturday, March 21, 2015

RAPPER FID Q APEWA TUZO YA `CHAMPION NA UMOJA WA NCHI ZA ULAYA EU

Umoja wa nchi za ulaya EU wampa tuzo Fareed Kubanda a.k.a Fid Q ya CHAMPION of the 2015 Europe Year for Development in Tanzania ,Pia Fid Q alifunguka kwenye Amplifaya ya Cloudsfm nakusema amefarijika sana kupata Tuzo hiyo kwani itampa hamasa ya kufanya kazi kwa bidii zaidi.

Pia Fid Q alisema amepata Tuzo hiyo kutokana na kujitolea kusaidia vijana katika jamii ili waache miadarati na japo kuwa darasa kwa sasa limefungwa ila anampango wa kulifungua tena upya darasa hilo.

Thursday, March 5, 2015

Ray C 'Mapaja Yangu Makubwa Yananitesa Sana'


Baada ya Kuachana na Madawa ya kulevya Mwanamuziki Ray C kwa sasa anahangaika na zoezi la kupunguza Mwili wake baada ya kuwa mkubwa sana kiasi cha kupoteza lile umbo lake la kiuno bila mfupa......

Soma Hapa Alichosema:

'No Filter,No Make Up!Mapaja bado yananitesa sana ila najua nitafikasafari yangu ya kupunguza uzito hadi nifike mkoa wa kilo 65........Bado Njia ni ndefu na safari ndo kwanza imeanza ila ninachojua ni kwamba ukitaka chochote kizuri maishano ni lazma ukitolee jasho!ma ndio ninachofanya!Hakika nitafika!

20kg to go!Safari ya kupunguza mwili bado inaendelea!nashukuru nimeanza kuona mwanga mbele yangu!Si rahisi ila nimezoea kupambana na lolote mbele yangu na na uhakika ntashinda na hili pia!Am doing ths for all my fans around the world!' Ray C

Wednesday, February 25, 2015

WASTARA ANADAIWA KUPOTEZA FAHAMU KISA MPENZI WAKE BOND KAPATA MTOTO WA NNE NA MWANAMKE MWENGINE

Wastara Juma ambaye kwa sasa anaripotiwa kuwa katika mapenzi na mwigizaji mwenzake, Bond Bin Suleiman anadaiwa kupoteza fahamu mara tu baada ya kupewa taarifa kuwa mpenziwe huyo amepata mtoto wa nne kwa mwanamke mwingine.
DIVA wa filamu nchini, Wastara Juma akiwa hospitali baada ya kuzimia.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, Wastara alipenyezewa ubuyu na mpenzi wa zamani wa Bond, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ na kuambiwa kwamba asijishebedue kwani Bond ana mwanamke mwingine ambaye amejifungua mtoto wa nne hivi karibuni.
“Tunakushangaa unavyojinadi kuwa Bond ni wako na kumpa zawadi ya keki ya bethidei wakati mwenzako amezaa na mwanamke mmoja baamedi hivi karibuni. Tena si kwamba mtoto huyo ni wa kwanza, ni wa nne,” kilisema chanzo hicho kikimnukuu Aunty.
ALIVYOZIMIA
Chanzo hicho kifunguka kuwa, baada ya kupewa taarifa hizo na Aunty Lulu, alizimia ghafla na kulazwa hospitali.“Wastara alizimia punde tu baada ya kupewa taarifa hizo, nasikia walimkimbiza hospitali, akapewa huduma nasikia kidogo sasa hajambo. Ishu ilikuwa mbaya, Aunty Lulu alimmchana laivu.”
Wastara Juma akiwa na Bond Bin Suleiman.
AUNTY LULU ANASEMAJE?
Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Aunty Lulu ambaye hapo awali alikuwa akilalamikia penzi la kitumwa la kupigwa mara kwa mara na Bond na hata kufikia mahali na kushukuru Mungu kwa kutengana kwao na kumuuliza kama habari hizo zilikuwa na ukweli wowote.
“Ni kweli nilimwambia kila kitu Wastara na tulikuwa tumepanga kwenda kumuona mtoto aliyezaliwa ili kujua kama kweli ni wa Bond.“Mimi niliamua kufunguka baada ya Bond kunitukana na kunitolea maneno mazito, kwani nilichoka, kama amepata presha na kulazwa hilo mimi silijui,” alisema Aunty Lulu.
TUJIUNGE NA WASTARA
Kwa upande wake, Wastara naye alikiri kupoteza fahamu na kulazwa hospitalini, lakini akakataa mambo hayo kumtokea kwa sababu ya kusikia taarifa hizo, bali kutokana na kuzidiwa na malaria.
“Nimepata nafuu na nimeshatoka hospitali, nilikuwa nimepatwa na homa kali ya malaria, madaktari waliniambia nilikuwa na malaria 10, kwa muda wa wiki mbili nilikuwa naumwa, lakini nikazidiwa kidogo, hivi sasa niko sawa na hapa ndiyo nashuka uwanja wa ndege natokea Mwanza,” alisema.
AMEKWEPA VIUNZI?
Mwanahabari wetu alipombana zaidi Wastara kutaka kujua kuzimia kwake kama kulitokana na kupata habari za Bond kuwa na watoto wanne, alisema siyo kweli kwani asingeweza kushangazwa na jambo hilo hasa kwa vile Bond ni mwanaume lijali na pia ana maisha yake ambayo hayamhusu.
“Mimi nina maisha yangu, yeye ana maisha yake, sasa jamani mimi nitapatwaje na presha kwa mambo hayo? Labda nikuambie tu kuwa hakuna lolote linaloendelea kati yangu na yeye zaidi ya masuala ya kikazi tu. Ninaomba uelewe hivyo kwa sababu huo ndiyo ukweli,” alisema.

Read more: http://www.vitukovyamtaani.com/2015/02/wastara-anadaiwa-kupoteza-fahamu-kisa.html#ixzz3SmczSqJy

Tuesday, February 24, 2015

CHEGE AKANUSHA KUVAA HIRIZI KWENYE PICHA ILIYOZAGAA MTANDAONI


Chege Chigunda amekanusha vikali tuhuma zilizotokana na kusambaa kwa picha akiwa jukwaani na huku mkononi mwake (karibuni na kwapa) akiwa na kitambaa cheusi ambacho baadhi ya watu wanahisi ni hirizi.

Mtu wa kwanza kuikuza picha hiyo na kuandika kuwa ana mashaka kuwa kitambaa hicho huenda kikawa hirizi, ni Maimartha Jesse.

“Angalia mkono wa kushoto wa chegge @chegechigunda hiiii ni hirizi ? any way isiwe kesi jiachie chege ila mziki mziki wako naupenda hata ukiniroga saw a Tu…japo cna imani hiyoo,” aliandika mtangazaji huyo wa zamani wa EATV.

Kauli hiyo ya Maimartha ilimfanya Chege kuamua kutoa ufafanuzi.

“Ushamba+roho mbaya+uandishi bila kusomea ni hatari sana hahaaahahahahahhaa eti waandishi magumashi wanadai nimevaa hirizi hahahhaaaaa hii tulivaa juzi Dodoma siku ambayo alifariki msanii mwenzetu marehemu mez b,msiwe vimbele mbele @maimarthawajesse @waandishimagumashi,” aliandika Chege.

Saturday, February 21, 2015

JACK PATRICK ANENA MAZITO AKIWA JELA MACAU CHINA

Wakati akiendelea kutumikia kifungo akiwa jela huko Macau, Hong Kong nchini China, modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff  ‘Jack Patrick’ amenena mazito juu ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Juma Khalid ‘Jux’, Vanessa Mdee, Aunt Ezekiel na Moze Iyobo.
Modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff  ‘Jack Patrick’.
BARUA KUTOKA CHINA
Jack aliyekamatwa nchini humo kwa msala wa madawa ya kulevya ‘unga’ mwaka 2013 kisha kufungwa miaka sita kwenye Gereza la Macau, hivi karibuni alilitumia gazeti hili barua nzito akionesha kushtushwa na vitu fulani vya mastaa hao.
MIMBA YA AUNT
Moja kati ya mambo yaliyomshtua Jack ni mimba ya mwigizaji Aunt Ezekiel ambaye ni mke wa mtu, Sunday Demonte anayodaiwa kupachikwa na mcheza shoo wa Diamond, Moze Iyobo.
Hata hivyo, katika skendo hiyo, Jack aliwataka watu wamuache Aunt apumzike kwani mapenzi hayachagui hasa kama ana furaha.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Wema Sepetu.
“Nimeshtushwa na udaku special Lol! Sasa Aunt ameamua kutulia na Iyobo…acha apumzike mapenzi hayachagui as long as ndiyo furaha yake, that’s okey,” aliandika Jack.
DIAMOND, ZARI
Mbali na mimba hiyo ya Aunt inayoelekea kuzaa matunda muda si mrefu, modo huyo alionesha kushtushwa na penzi la staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na Zari akishangaa ilikuwaje hadi jamaa huyo akaachana na Wema Sepetu kisha kutua kwa mrembo huyo mwenye maskani yake nchini Afrika Kusini na Uganda.
“Heh! Kwani Diamond aliachana na Wema tena?” Alihoji Jack na kuongeza:
“Sasa Zari si anakaa South Africa ‘Sauzi’? Wanaonana vipi na Platnumz? Mh! Wala hawatadumu maana mapenzi ya mbalimbali. Labda kama Nasibu (Diamond Platnumz) atahamia South.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ wakiwa kwenye pozi.
KAJALA Vs WEMA
Pia video queen huyo wa Ngoma za Nataka Kulewa (ya Diamond), She Got A Gwan (ya Marehemu Ngwea) na Kamugisha (ya Linex) aliulizia lile bifu zito la Wema na Kajala Masanja kama lilikwisha kwani mastaa wa Bongo Movies walishazoeleka kugombana na kupatana.
Bifu hilo ni lile la Wema kumtuhumu Kajala kumchukulia bwana’ke (CK) huku akisahahu kwamba alimlipia Sh. Milioni 13 ili asiende jela miaka mitano baada ya kukutwa na hatia ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.“Ya Kay (Kajala) na Wema naona mwishowe watarudisha urafiki tu. Ya Bongo Movies nimeshayazoea huwa wako hivyo kila muda, kawaida yao.”
JUX, VANESSA
Jack alipofika kwenye ishu ya kusalitiwa na staa wa Bongo Fleva, Jux akidaiwa kuwa kwenye malovee na sexy lady wa muziki wa Kizazi Kipya, Vanessa ‘Vee Money’, aliandika ishu hiyo kwa hisia zaidi huku akijilaumu mwenyewe kwa kosa alilofanya.
Juma Khalid ‘Jux’, akiwa na mpenzi wake Vanessa Mdee.
“Ya Jux na Vanessa nimeamua tu kuyaacha coz nipo jela siwezi kumzuia kufanya lolote then ni makosa yangu yaliyofanya hayo yote kutokea.“Sijui hata kama itakuja kutokea tena kuwa wote tena mimi na yeye, that chapter closed already, nahesabia muda mfupi tu now nitatoka lakini sina chochote cha kufanya nionane naye,” alimalizia kuandika Jack.
Jack Patrick alihukumiwa kifungo hicho mwaka jana lakini taarifa zilieleza kuwa endapo ataonesha nidhamu gerezani ataachiwa mapenzi hivyo hatakaa jela miaka yote sita.

UJUE UNDANI WA MAREHEMU MEZ B

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva aliyekuwa akiwika na kundi la Chamber Squad, Moses Bushagama ‘Mez B’ amefariki dunia asubuhi ya leo majira ya saa 4:30 mjini Dodoma.
Mez B akiwa katika moja ya mahojiano yake na kituo cha TV.
Hii imekuwa ni pigo la pili kwa kundi la Chamber Squad kupoteza memba wake baada ya awali kumpoteza Albert Mangweha ‘Ngwear’.Katika makala haya yanauelezea undani wa Mez B mpaka kufikia umauti.
MEZ B NI NANI?
Mez B amekulia mjini Dodoma maeneo ya Area C. Akiwa anasoma katika Shule ya Sekondari ya Mazengo, Dodoma ndipo alipokutana na wenzake Noorah, Ngwear pamoja na Dark Master.
Kwa mara ya kwanza walipokutana shuleni hapo, walianzisha kundi la CFG yaani Chemba Fleva Guys lililokuwa likiundwa na Ngwear, Mez B pamoja na Nzeku.
Walipomaliza shule, wakaamua waendeleze kundi na kubadilisha jina na kujiita Chamber Squad.
Awali Chamber Squad ilianzishwa na Tino Mkale, Mgulu George na wengine kibao ambao hawakuwa na majina kabla ya kuliacha kundi hilo likimilikiwa na Ngwear, Noorah, Mez B na Dark Master.
Rehema Chalamila (picha ya chini) ambaye ni mmoja ya mastaa waliowahi kushirikisha na Mez B katika Wimbo wa Basi Kama Vipi.
AANZA KUNG’ARA
Mez B alianza kutambulika kama mwanamuziki wa R&B ambapo alitoka na Wimbo wa Fikiria na baadaye akawika na nyimbo kama Furaha Tele, Mama na Mwana, Nichukue pamoja na Mpenzi njoo aliyokuwa amemshirikisha Afande Sele.
Nyimbo nyingine zilizompa umaarufu ni pamoja na Kidela, Nimekubali, Shemeji, Basi Kama Vipi akiwa ameshirikiana na Ray C na Noorah.
Miongoni mwa wimbo uliopandisha kundi la Chamber Squad ni pamoja na Home Sweet Home ambao Mez B aliutendea haki kwa upande wa kiitikio.
Marehemu, Albert Mangweha 'Ngwair' enzi za uhai wake.
NGWEAR AFARIKI, MMOJA APUNGUA
Mei 28, 2013 Kundi la Chamber Squad lilipata pigo kwa kuondokea na memba wao, Albert Mangweha ‘Ngwear’ ambaye alifariki akiwa nchini Afrika Kusini alikokwenda kufanya shoo kwenye miji mbalimbali nchini humo ikiwemo Johannesburg na Cape Town.Alizikwa mkoani Morogoro, Juni 6, 2013 katika makaburi ya Kihonda.
Baada ya hapo kundi la Chamber Squad lilibakiwa na vichwa vitatu ambavyo ni Noorah, Mez B pamoja na Dark Master.
Memba mwenzao, Dark Master alishawahi kusema kuwa kundi hilo bado lipo na walikuwa njiani kuja na nyimbo mfululizo.
Mez B akiwa na majeraha baada ya kujerehuliwa na mtu asiyejulikana.
ASHAMBULIWA, ATAKA KUULIWA
Zikiwa zimepita wiki chache tangu Mez B ampoteze memba mwenzake, Ngwear alipata balaa la kushambuliwa na mtu asiyemfahamu akiwa sehemu ya burudani maeneo ya Sinza, jijini Dar.
Usiku huo Mez B alikuwa ameenda kutafuta chakula (Chips) na kushuhudia mtu mmoja akiamuliwa na mabaunsa achomwe visu.
Tukio hilo lilianzia pale Mez B alipofika eneo hilo ambalo alishangaa mtu mmoja akiitusi serikali pamoja na Mez B mwenyewe hali iliyozua tafrani.Kitendo cha Mez B kuondoka, baunsa mmoja alimfuata mtu aliyekuwa akitukana na kumuamuru amchome visu Mez B. Ujasiri ulimsaidia Mez B kwani alikuwa achomwe shindoni lakini alikwepa na kuchoma baadhi ya maeneo ya usoni.
Suala hilo alilipeleka mbele ya vyombo vya sheria ambapo bado kesi ilikuwa ikiendelea.

AFUMWA AKIJIACHIA NA WASICHANA UFUKWENI
Septemba mwaka jana, Mez B alilingia katika msala wa kukutwa katika Fukwe za Mikadi, jijini Dar akiwa na wasichana ambao walionekana wakiwa watupu.
Moja ya magazeti pendwa, yalichapisha habari hiyo ambayo picha zilimuonyesha Mez B akiwakumbatia huku wasichana hao wakionekana watupu kama walivyozaliwa.
Wasichana hao waliotambulika kama Vicky na Rebecca walikuja kubainika kuwa siyo raia wa Tanzania na kudaiwa kuwa Mez B alikuwa akitengeneza video ya wimbo mpya na wasichana hao waliomba kupiga picha naye tu baada ya kumuona.
Marehemu, Mez B akiwa studio enzi za uhai wake.
AANZA KUUGUA
Februari mwaka huu, Mez B alianza kuugua na kulazwa katika hospitali moja mkoani Dodoma akiwa anasumbuliwa na maumivu ya kichwa na shingo hali iliyomfanya awe chini ya uangalizi wa madaktari.
Kauli yake ya mwisho baada ya kuugua ilikuwa ni kuomba msamaha kwa mashabiki kwa kuchelewa kuanza ‘projekti’ mpya kutokana na hali iliyokuwa ikimkabili.
“Bado nasumbuliwa na Pneunomia tangu mwezi wa 12 mwaka jana lakini kwa sasa naendelea vizuri na matibabu na nategemea kuruhusiwa muda wowote. Nikitoka nitaendelea na projekti yangu,” alisema Mez B.
AFARIKI DUNIA
Mez B amefariki dunia saa 4:30 asubuhi katika Hospitali ya Mwananchi mjini Dodoma ambapo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Homa ya Mapafu ambao kitaalamu unajulikana kama Pneunomia.
Taratibu juu ya mazishi bado hazijafanyika na tutaendelea kukujuza zaidi.
Uongozi na wafanyakazi wa Global Publishers unatoa pole kwa ndugu na wana familia wa Mez B kwa msiba uliotokea.Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana  lihimidiwe Amen.

Friday, February 20, 2015

MASTAA WAMCHANA VIBAYA DIAMOND KISA MISIBA


Wasanii wa sinema na Bongo Fleva wamemchana vibaya staa wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwamba si mtokaji kwenye misiba ya wenzake.


Staa wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’.

Wakizungumza na Amani kwenye maziko ya baba mzazi wa Mbongo Fleva, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’, Ebby Sykes, Jumatatu iliyopita, wasanii hao walioomba majina yao yalindwe walisema kumbukumbu za vichwani mwao zinaonesha kuwa, Diamond amekuwa akichagua misiba ya kujitokeza hasa ile ambayo itampa  ‘kavareji’ kwenye vyombo vya habari.

WASIKIE WENYEWE
“Mimi nakumbuka wakati wa kifo cha Kanumba (Steven), Diamond alitokea kwa sababu ulikuwa msiba mkubwa sana na kweli alipata kavareji ya kutosha kwenye media.

“Halafu akaonekana tena kwenye msiba wa baba yake Wema Sepetu, nadhani kwa vile alikuwa mtu wake Wema wakati huo asingeacha kwenda. Lakini baada ya hapo sikumbuki,” alisema msanii mmoja.
Msanii mwingine aliongeza: “Halafu Diamond na Dully ni washikaji, sasa jamaa tunasikia yuko Zenji tu hapo anakula bata na Zari (Zarina Hassan) lakini ameshindwa kuja Dar kumzika baba mzazi wa mshikaji  wake.”

Akaongeza tena: “Kama sijasahau hata kwenye kifo cha mwanamuziki wa Bendi ya Msondo, marehemu Maalim Gurumo hakutokea japokuwa alikuwa amerudi nchini kutoka nje. Magazeti mliandika kwamba Wema alimzuia kwenda kuzika. Sasa ni vizuri kweli?”

WEMA AMUUMBUA KAJALA NA ASHANGAA KIGOGO CK AMBAYE NI MPENZI WA KAJALA KUISHIWA

Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amedaiwa kumuumbua shosti wake wa zamani, Kajala Masanja kwa kumwaga ‘ubuyu’ kwamba amefilisika baada ya kigogo maarufu kama CK anayedaiwa kuwa ndiye mpenzi wake, kuyumba kiuchumi,


Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.

Kigogo huyo aliyewahi kuwa na uhusiano na Wema kisha kumwagana naye, imedaiwa kuwa ile jeuri ya kununua magari ya kifahari, kumiliki biashara mbalimbali mjini, kwa sasa ameangukia pua kwani hawezi tena kujitutumua.

TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na Wema, baada ya kuhamishia majeshi kwa Kajala, Wema hakufurahia hivyo aliposikia uchumi umeyumba, amefurahia sana kufuatia ule msemo wa ‘adui muombee njaa.’

“Wema amefurahi sana, anawaambia marafiki zake kuwa malipo ni hapahapa duniani, Wema alimlipia Kajala dhamana ya sh mil. 13 ili asifungwe kwa msala wa kutakatisha fedha uliokuwa ukimkabili lakini akamgeuka na kumchukulia bwana wake, ule si ubinadamu kabisa,” kilisema chanzo hicho.

KAJALA ANA NUKSI?
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, Kajala ana nuksi kwani CK alipokuwa na Wema alikuwa na mafanikio na kupata fedha kila kukicha lakini alipohamia kwa Kajala mambo ndiyo yakaharibika.
“Kajala ana nuksi, CK alipokuwa na Wema walikuwa wanapata fedha nyingi kila wakati lakini kwa Kajala wamefilisika kwelikweli,” kilisema chanzo na kuongeza:


WEMA AMSHANGAA CK
“Madam mwenyewe amemshangaa sana CK kuishiwa fedha wakati alikuwa mtu wa kucheza na dola nyingi kila kukicha na aliwekeza fedha zake katika miradi mbalimbali.”

CK AMEPATWA NA NINI?
Jitihada za kumpata CK ili azungumzie ishu ya kuyumba kiuchumi hazikuzaa matunda lakini kwa mujibu wa mmoja wa watu ambao wanafanya naye kazi, kigogo huyo ameporomoka kiuchumi kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kufanya magumashi ya fedha kazini hadi kufikia hatua ya kutaka kufukuzwa kazi.


Staa katika tasnia ya filamu Bongo,Kajala Masanja.

“CK hayuko vizuri kazini, ana majanga kibao, ile jeuri aliyokuwa akifanya na Wema na Kajala ilikuwa ni fedha za magumashi sasa kimemnukia kazini,” kilisema chanzo hicho ingawa mwenyewe alipotafutwa kwenye simu hakupatikana.

MAZUNGUMZO YA WEMA YATHIBITISHA
Wakati mwanahabari wetu akiendelea kuichimba habari hiyo, alifanikiwa kunasa ‘clip’ ya sauti ya Wema iliyoonesha dhahiri kwamba mrembo huyo amefurahishwa na kitendo cha wawili hao kukalia kuti kavu.

Sauti hiyo ya Wema inasikika akizungumza na shosti yake kumueleza jinsi gani Kajala ameumbuka maana alifikiri kutembea na shemeji yake ameula kumbe matokeo yake ameangukia pua kwani mwanaume amefilisika.“…Kajala sasa hivi anaendesha Noah (Toyota) ile yenye mastikamastika nakwambia…” ilisikika sehemu ya clip hiyo.

WEMA ASAKWA
Paparazi wetu alimvutia waya Wema ili aweze kufunguka zaidi kuhusiana na sakata hilo namna ambavyo amefurahia, simu yake iliita bila kupokelewa.Hata hivyo, mwandishi wetu alikwenda nyumbani kwake, mtaa wa Bwawani-Kijitonyama jijini Dar zaidi ya mara tatu kwa nyakati tofauti lakini hakufanikiwa kumpata baada ya mlinzi kudai amelala.

SNURA AFUNGUNGUKA JUU YA KUDHALILISHWA KWA KUAMBIWA AMEZAA


Msanii anayefanya muziki na filamu Bongo, Snura Mushi ameeleza kushangazwa kwake na taarifa zinazozidi kuenea kuwa amejifungua, jambo ambalo anadai eti siyo kweli.
Msanii anayefanya muziki na filamu Bongo, Snura Mushi.
Madai ya staa huyo kujifungua kwa siri yameenea na hata wasanii wenzake wanajua hivyo lakini mwenyewe amekuwa akikanusha na kuwaacha mashabiki wake njia panda.Akipiga stori na Ijumaa hivi karibuni, Snura alisema yeye ana mtoto mmoja mkubwa lakini madai ya kwamba amejifungua hivi karibu hayana ukweli.
“Mimi sina mtoto mdogo, mwanangu ni yule mnayemjua, hao wanaosema nimezaa mbona wananizalisha?” alihoji Snura ambaye baada ya muda mrefu kupotea, juzikati aliibukia kwenye Ukumbi wa Escape One ulipo Msasani, jijini Dar.

WALIOZAA NA NAY WA MITEGO WAMALIZA BIFU


Mabinti wawili waliozaa na msanii wa muziki, Emmanuel Elbarik ‘Nay wa Mitego’, Siwema na Skyna Ally ambao awali ilidaiwa walikuwa na bifu zito, sasa wameamua kuwa mashosti.Ijumaa hivi karibuni liliwanasa wawili hao kwenye Ukumbi wa Escape One, Msasani jijini Dar wakiwa beneti kama mtu na mke mwenza na lilipotaka kuzungumza nao wote walichenga na kutaka waachwe.
Mrembo aliyezaa na msanii wa muziki, Emmanuel Elbarik ‘Nay wa Mitego’ Siwema.
Hata hivyo, mmoja wa marafiki aliyekuwa ameongozana nao aliyeomba hifadhi ya jina lake alimwambia mwandishi wetu kuwa, baada ya wawili hao kuwa na bifu kwa muda mrefu, waliamua kukaa chini na kumaliza tofauti zao kwani kilichotokea tayari kimeshatokea.
Skyna Ally.
“Sasa hivi ni mashosti ile mbaya, sehemu mbalimbali wamekuwa wakienda pamoja, yaani ni kama vile wamekubali kuwa wake wenza licha ya kwamba anayekaa na Nay ni Siwema,” kilieleza chanzo hicho.

MZEE YUSUPH KUOA TENA MKE WA TATU, WAKE ZAKE WATUPIANA VIJEMBE MTANDAONI!




Mwimbaji mahiri wa muziki wa Taarab nchini ambaye pia ni mkurugenzi wa kundi la Jahazi Modern Taarabu,Mzee Yusuph anatarajia kuoa tena mke wa tatu hivi karibuni huku wake zake wawili wakiwa kwenye bifu zito wakitupiana vijembe mtandaoni. 
Akipiga stori na paparazi alisema kuwa anatarajia kuoa mke huyo ambaye anaishi huko visiwani Pemba,na kwamba mipango ikiwa tayari kila kitu kitakuwa hadharani. 

Hivi karibuni wake zake wawili ambao ni Malkia Leila Rashid ambaye pia ni mwimbaji wa kundi hilo na mke wake mdogo aitwaye Chiku wamekuwa wakirushiana vijembe kwenye mtandao wa kijamii wa ‘WathsAAp’ kwa kuandikiana ‘Status’ za vijembe.
 Mzee Yusuph akiwa na mke wake pili,Chiku.
Habari zinasema kuwa wake hao wamekuwa kama chui na paka na mzee Yusuph hana mpango wa kuwapatanisha kwa kuwa hakuna hata mmoja aliyeonyesha chuki kwa mwenzake akiwa na nao. 

‘’Waache tu warushiane vijembe tena ndiyo vizuri na dawa yao nawaletea mke wa tatu na wala sina mpango wa kuwapatanisha,’alisema Mzee Yusuph.

Thursday, February 19, 2015

Labda ulikua huyajui haya kuhusu hizi picha za Wema Sepetu na Ommy Dimpoz


  • Share on facebook Share on google_plusone_share Share on twitter Share on linkedin

Zile picha za mahaba zilizosambaa kwenye mitandao zikimuonyesha Staa wa Bongo Fleva,Ommy Dimpoz na Wema Sepetu wakiwa kitandani zimezidi kuzua utata baada ya Ommy kusema hakujua alipigwa saa ngapi kwani hakuwa na fahamu bali aulizwe Wema.Ommy amezungumza na Uheard na Soudy Brown
alisema kuwa hana maelezo zaidi ya kuzungumza zaidi ya kusema kuwa hajui ni muda upi zilipigwa picha hizo.Wiki hii picha hizo zilisambaa mitandaoni na kuzua
hizo zilisambaa mitandaoni na kuzua maswali kuwa Ommy Dimpoz ameamua kujiweka kwa Wema baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Diamond Platinum,lakini Aunty Ezekiel ambaye rafiki wa Wema alisema kuwa rafiki yake huyo alikwenda nchini Afrika Kusini kufanya video mpya ya ngoma ya Ommy. Hata hivyo picha nyingine zilisambaa Wema akiwa na aliyekuwa mume wa Zari wakiponda raha nchini humo na kuzua sintofahamu.

Wednesday, February 18, 2015

LADY JAY DEE' AELEZA JUU YA UMILIKI WA EFM RADIO 93.7


Maswali yamekuwa mengi kwa mwimbaji mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva hapa nchin Judith Wambura 'Lady Jaydee' juu ya maisha yake ambapo aliulizwa juu ya kuachana na mumewake lakini pia kuhusiana na kufungua kituo cha matangazo kwa njia ya sauti (Radio) na au umiliki wa EFM Radio inayo patikana kwenye masafa ya 93.7 Fm jijini Dar es Salaam.
Haya ndiyo aliyo sema kupitia account yake ya Instagram.

Ulituahidi utafungua Radio mbona kimya mpaka leo?
JIBU : "Niliandika hiyo kitu siku ya wajinga duniani, April 1, sikuwahi kuahidi.
Lakini matamanio yangu ni siku moja kumiliki kituo cha radio na ikibidi hata television.
Hakuna linalo shindikana, palipo na nia.EFM radio ni yako?
JIBU : Hapana sio yangu
Nafikiri inadhaniwa hivyo kutokana na kila mtu ku tamani, mimi niwe na radio.
Je!mtaniruhusu na mimi niwaulize swali?
Kwanini mnatamani sana niwe na radio? ?
Mungu akijaalia ntakuwa nayo " Ameandika Lady JayDee.

FAIZA KESSY AWACHOKOZA TENA WABONGO ATUPIA PICHA 2 AKIWA NA KICHUPI UFUKWENI


Mrembo na muigizaji wa filamu, Faiza Ally ambae ni mama wa mtoto mmoja amezibandika picha hizi kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa maeneo ya ufukweni mjini Bagamoyo.
Mbali na ukweli kuwa hapa amevalia nguo za ufukweni, mahabiki wengi wamemshabulia kuwa..
mavazi haya hayafai kwani yeye sasa hivi ni mama tena amezaa na Muheshimiwa, huku wengine wakisema hapo ndio mahali pake na wa muacha afurahie maisha yake.

Japokuwa ni kweli kuwa Faiza aliwashangaza wengi mwaka jana kwa kuvalia “pampers” kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa, lakini kwa hizi  nadhani  tumwache, amependeza sana.

Saturday, February 14, 2015

Msafiri Zawose mwimbaji nyimbo za kigogo

14 Februari 2015 Imebadilishwa mwisho saa 05:00 GMT
Katika visiwa vya Zanzibar kunafanyika tamasha la sauti za busara.
Mmoja wapo wa wasanii ambao wanatumbuiza mwaka huu, ni Msafiri Zawose anayeimba muziki wa kigogo kutoka Dodoma katikati mwa Tanzania Mwandishi wetu Tulanana Bohela ameweza kukutana naye akiwa katika mazoezi kabla ya kwenda jukwaani na kuzungumza naye.

Thursday, February 12, 2015

WEMA ANA MIMBA? HEBU JIONEE PICHA HIZI ZINAZOSAMBAAMTANDAONI


Hizi ni picha za mwigizaji Wema Sepetu ambazo zinasamabaa kwa kasi huko Instagram zikionyesha watu wakiwa wamemshika tumbo kwa nyataki tofauti huku wote sura zao zikiwa hazionekani.
Moja kati ya akaunti kwenye mtandao huo inayoendeshwa na shabiki mkubwa wa Wema, inayokwenda kwa jina la WEMADAILY, ilizitupia picha hizi na 

CHRISTIAN BELLA 'KING OF THE BEST MELODIES' AAHIDI MAKUBWA SHOO YA VALENTINE'S DAY, DAR LIVE


Christian Bella (kulia) akijibu baadhi ya maswali ya wanahabari (hawapo pichani) kuhusu maandalizi ya shoo yake ya Valentine kwenye Ukumbi wa Dar Live.
Bella akisisitiza jambo kwa wanahabari (hawapo pichani).
Christian Bella (kulia) akiwapa vionjo vya wimbo wake mpya wa 'NASHINDWA' wanahabari (hawapo pichani). Kushoto ni mmoja wa viongozi wa Malaika Band, X-Bass Babu Bomba.
Bella akitoa vionjo vya wimbo wa 'NANI KAMA MAMA' kwa wanahabari.
Bella akiwa na Mhariri wa Gazeti la Risasi Jumamosi, Erick Evarist.
X-Bass Babu Bomba na Bella katika pozi na Mpiga Picha wa GPL, Musa Mateja.
X-Bass Babu Bomba na Bella wakiwa katika picha ya pamoja na Mhariri Mwandamizi wa GPL, Walusanga Ndaki.
X-Bass Babu Bomba na Bella wakipozi na Shafii Mohamed wa GPL.
X-Bass Babu Bomba na Christian Bella katika pozi ndani ya GPL.

PREZIDAA wa Bendi ya Malaika Music, Christian Bella 'King of the Best Melodies' amewaahidi shoo kali mashabiki wake watakaohudhuria katika Ukumbi wa Kisasa wa Dar Live, Jumamosi ijayo ambayo ni Siku ya Wapendanao 'Valentine's Day'. Staa huyo ameyasema hayo hivi punde wakati wa mkutano na wanahabari wa vyombo mbalimbali uliofanyika katika ofisi za Global Publishers.

Bella amesema atakuwepo ndani ya kiwanja hicho mapema kuanzia saa 7 mchana na atapiga picha za red carpet na mashabiki wake watakaohudhuria sambamba na kuzungumza nao mawili-matatu. Mbali na kuwahi ukumbini, Bella amewaandalia nyimbo zake zote kali za mapenzi kama vile Msaliti, Safari Siyo Kifo, Nakuhitaji pamoja na wimbo bora uliofunga mwaka wa Nani Kama Mama.

Kuonyesha kuwa utakuwa Usiku wa Wapendanao, Bella amewaandalia mashabiki wake zawadi ya wimbo mpya uitwao NASHINDWA ambao atauchia kwa mara ya kwanza huku video akienda kuifanyia nchini Afrika Kusini wiki ijayo. Mbali na Bella usiku huo ambao ni maalum kwa wapendanao, mkali wa muziki wa Mwambao, Mfalme Mzee Yusuf naye atakuwepo katika kuwaburudisha mashabiki wote watakaokuwepo ukumbini hapo.

Usiku huo Mzee Yusuf atashuka na kundi lake la Jahazi Modern Taarab na kuangusha ngoma zake zote kali za mapenzi kama vile My Valentine, Wapendanao, Tiba ya Mapenzi,  Wasiwasi Wako pamoja na hii ambayo ni habari ya mjini kwa sasa ya Mahaba Niue.
TUPAMBANE BLOG