Mhammad Faraj Salem Al Saiy
Sala ya Idi
imeanza kusaliwa katika mwaka wa mwanzo wa Al Hijra, mwaka
ule Mtume (Swalla Llahu alayhi
wa sallam) alipohamia Madina akifuatana na Sahibu
yake wa pangoni
Al Siddique (Radhiya Llahu anhu), na
hukmu yake Sala hiyo ni
'Sunnah Muakkadah'.
Mtume (Swalla Llahu
alayhi wa
sallam) hakupata kuiacha Sala hii
na alikuwa akihimiza watu wote kwa pamoja,
wanawake kwa wanaume kuisali Sala hiyo.
INAPENDEZA MTU
KUKOGA, KUVAA NGUO NZURI NA KUJIPAKA MAFUTA MAZURI
Kutoka kwa
Jaafar bin Muhammad, kutoka
kwa babake, kutoka kwa babu
yake, ameeleza kuwa;
"Siku ya
Sikukuu, Mtume (Swalla Llahu alayhi
wa sallam)
alikuwa akipenda kuivaa nguo yake
nzuri aliyoletewa kutoka Yemen"
Imam Shafi
Anasema Ibnil Qayim;
"Mtume (Swalla Llahu alayhi
wa sallam) alikuwa akiwavalisha wajukuu zake nguo
nzuri kabisa na alikuwa yeye
mwenyewe ana guo lake zuri akilivaa
kila Ijumaa na katika siku
za Sikukuu.”
KULA CHOCHOTE
KABLA YA KWENDA MSIKITINI
Siku ya Sikukuu
ya Idd al Fitri ni Sunnah
kula tende moja au tatu au tano nk. (kwa
hesabu ya witri) kabla ya
kwenda kusali.. Ama katika Sikukuu
ya Idd al Adh-ha, tunatakiwa tule baada ya
kurudi kusali.
Anasema Anas (Radhiya
Llahu anhu);
"Mtume (Swalla
Llahu alayhi wa sallam)
alikuwa hatoki kwenda kusali mpaka
kwanza ale tende, na alikuwa akila kwa
hesabu ya witri. (1 au 3 au 5 nk.)".
Ahmed na Bukhari
Na kutoka kwa Bureida
(Radhiya Llahu anhu) amesema;
"Mtume (Swalla
Llahu alayhi wa sallam)
alikuwa katika Sikukuu ya Idd
al Fitri hatoki mpaka ale, na katika
Idd al Adh-ha hali mpaka arudi".
Ahmed-Attirmidhy na Ibni
Majah
BORA KUSALI
UWANJANI
Sala ya Idi
inaweza kusaliwa ndani ya msikiti,
lakini kuisali nje penye uwanja
ni bora
zaidi, kwani Mtume (Swalla Llahu
alayhi wa sallam) alikuwa akisali Sala za
Idi zote mbili (Sikukuu kubwa na Sikukuu
ndogo) nje penye uwanja, isipokuwa
panapotokea dharura kama vile mvua
nk.
Abu Daud, Ibni Majah
na Al Hakim
KUBADILISHA NJIA
Mtu anapokwenda kusali Sala ya
Idi ni vizuri
abadilishe njia. Ende kwa njia
nyingine na arudi kwa njia
nyingine.
Imesimuliwa katika Sahih Bukhari kuwa;
"Mtume (Swalla
Llahu alayhi wa sallam)
alikuwa Siku ya Idi akenda
kusali kwa kupitia njia nyingine
na anaporudi akibadilisha njia".
Inajuzu pia kwenda
na kurudi kwa njia ileile.
WAKATI WAKE
Anasema Imam Ibni Rushd al Qurtubiy;
"Sala ya
Idi inasaliwa kuanzia pale jua linapochomoza mpaka wakati wa
Zawal (jua linapokuwa utosini)."
Mtume (Swalla Llahu
alayhi wa
sallam) alikuwa akiichelewesha kidogo Sala ya Idd
al Fitri, ama Sala ya Idil
al Adh ha alikuwa akisali mapema zaidi, huenda sababu
ya kuichelewesha Sala ya Idd
al Fitri ili watu wawahi kutoa
Zakatul Fitri kabla hapajasaliwa, na akisali mapema
zaidi Sala ya Idd al Adh-ha
ili watu wapate kuwahi kwenda
kuchinja wanyama wao.
Maulamaa wamekhitalifiana juu ya watu
waliochelewa kupata habari za kuonekana
kwa mwezi. Je, watasali wakati wowote pale itakapowafikia habari, hata wakizipata
habari hizo wakati wa Alasiri?
Imepokelewa kuwa Mtume (Swalla Llahu
alayhi wa
sallam) aliwaamrisha watu waliochelewa kupata habari ya
kuandama kwa mwezi wasiendelee kufunga (wale), na washerehekee kama
wenzao lakini waisali Sala hiyo
siku ya pili
yake wakati wa asubuhi".
Abu Daud
SIKUKUU
IKIANGUKIA SIKU YA IJUMAA
Wamekhitalifiana ikiiwa Sikukuu itaangukia siku ya Ijumaa,
je, inatosha watu wakisali Sala ya
Idi peke yake au wanatakiwa pia wasali Sala
ya Ijumaa?
Amesema Ataa;;
"Siku hiyo
haisaliwi Ijumaa wala adhuhuri, bali inasaliwa
Sala ya Idi
tu, kisha Sala ya Alasiri
pale unapoingia wakati
wake".
Ama Ibni Jariyr
amesema;
"Walioruhusiwa kufanya hivyo ni
watu wanaokaa mbali na miji
tu, ili wasihangaike
kuja mjini asubuhi kwa ajili
ya kusali Sala ya Idi
kisha waje tena mchana kusali
Ijumaa, kama ilivyopokelewa kuwa Uthman (Radhiya Llahu anhu) aliwahutubia
watu siku ya iliyosadifu Sikukuu kuwa siku
ya Ijumaa akawaambia;
"Enyi watu mnaokaa sehemu
za mbali, ikwa mnataka kubaki
na kusali Ijumaa pamoja na
sisi basi bakini, ama mkitaka
kurudi makwenu mnaweza kurudi".
Malik katika 'Muwataa'.
ADHANI NA IQAMA
Mtume (Swalla Llahu
alayhi wa
sallam) alikuwa mara baada ya
kuwasili uwanja wa Sala anaanza
kusalisha, na alikuwa akenda huko kwa miguu
yake na wala
hakuwa akipanda mnyama.
Mara anapowasili hapo, alikuwa akianza kusali bila ya
Adhana wala Iqama, na wala
hakuwa akisema;'Assalaatu jaamiah'.
'Hakuwa akiadhini wala hakuwa aqiqimu
katika Sikukuu zote mbili'
Bukhari na Muslim
TAKBIYR KATIKA
SALA YA IDI
Sala ya Idi
ni raka-a mbili, na imesuniwa
mtu katika raka-a ya mwanzo
kukabir mara saba baada ya
Takbiratul Ihram, na katika raka-a ya
pili akabir mara tano na
awe ananyamaza kidogo baada ya kila
takbira kama alivyokuwa akifanya Mtume wetu (Swalla
Llahu alayhi wa sallam).
Takbira ni Sunnah,
na haibatiliki Sala mtu akiacha
kwa kusahau au kwa makusudi.
Imam Al Shoukani anasema;
"Mtu akiiacha kwa kusahau
hatakiwi kusujudu Sajdatu sahau".
Wamekhitalifiana maulamaa katika kunyanyua mikono katika Takbira
zote, baadhi yao wakasema hainyanyuliwi
isipokuwa katika Takbiratul Ihram peke yake, ama Imam Shafi amesema kuwa
inyanyuliwe mikono katika takbira zote.
KUSALI SALA YA
SUNNAH KABLA YA SALA YA IDI AU BAADA YAKE
Hapana dalili yoyote
ile kuwa pana Sala ya
Sunnah kabla ya Sala ya
Idi wala baada yake, na hakuwa Mtume (Swalla Llahu
alayhi wa sallam) akisali sala yoyote ile
kabla ya Sala ya Idi
wala baada yake, na Sahaba
zake (Radhiya Llahu anhum) pia
hawakuwa wakifanya hivyo.
Amesema Ibni Abbas;
"Mtume (Swalla
Llahu alayhi wa sallam)
alitoka siku ya Idi kuelekea
uwanjani akasali Raka-a mbili (za
Idi) na wala
hakusali sala yoyote ile kabla
yake wala baada yake".
Imepokelewa na
maimam wote wa hadithi
Wapo baadhi ya
maulamaa wanaosema kuwa ni Makruh
mtu kusali Sala yoyote ile
kabla au baada ya Sala ya
Idi lakini hapana dalili ya
kukataza kusali, muhimu isiwe katika
zile nyakati zinazokatazwa mtu kusali.
HOTUBA YA IDI
Kutoa hotuba baada
ya Sala ya
Idi ni Sunnah,
na kuisikiliza pia ni Sunnah.
Kutoka kwa Abu Said (Radhiya Llahu anhu)
amesema;
"Alikuwa Mtume
(Swalla Llahu alayhi wa sallam)
katika Sikukuu ya Idi al Fitri
na Idi al Adh-ha akitoka kuelekea mahali panaposaliwa, na jambo la mwanzo analofanya mara baada ya kuwasili
hapo ni kusalisha
watu, na baada ya kutowa
salamu anawakabili watu wakiwa bado
wamekaa katika safu zao na
kuanza kuwapa mawaidha huku akiwausia
na kuwaamrisha mema, na alikuwa
katika hutoba yake akikithiri katika kusema 'Allahu Akbar', na alikuwa kama anataka
kuchaguwa ujumbe wa kwenda mahala
au kuchagua jeshi au kutoa amri yoyote
ile, basi alikuwa akifanya wakati huo kisha
anaondoka"
Anaendelea kusema Abu Said (Radhiya Llahu anhu);
"Mtume (Swalla
Llahu alayhi wa sallam) alikuwa
akeshasalisha akisema;
No comments:
Post a Comment