Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Wednesday, December 10, 2014

CRDB YAIBUKA KIDEDEA KATIKA TUZO ZA NBAA UPANDE WA MABENKI

Naibu waziri wa fedha Adam Malima akimkabidhi meneja wa fedha
wa benki ya CRDB Sosteness Biseko
tuzo  ya NBAA ya ushindi  katika
uandaaji wa taarifa bora za fedha mwaka 2013-2014,jumla ya benki tisa
zilishiriki ambapo Benki ya CRDB iliibuka mshindi wa kwanza katika kundi la
mabenki, hafla hiyo ilifanyika juzi katika hotel ya Mount Meru jijini Arusha
*********
Mashirika binafsi ,taasisi
na idara mbalimbali za serikali zimehimizwa   kushiriki katika mashindano ya tuzo
zinazotolewa na bodi ya wahasibu  
na wakaguzi wa hesabu nchini NBAA katika
uandaaji bora wa taarifa za fedha za mwaka ili kuboresha hesabu za mashiriki
hayo na kuongeza uwazi katika shughuli za biashara za ndani ya nchi na
kimataifa 
Mwenyekiti
wa bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini NBAA Profesa Issaya Jairo ametoa kauli hiyo jijini Arusha wakati wa kufunga  mkutano mkuu wa mwaka wa bodi hiyo ulio enda
sambamba na utoaji wa tuzo na vyeti kwa washindi  katika uaandaaji  bora wa taarifa za fedha za mwaka ambapo kwa
mwaka 2014 jumla ya washiriki 40 walishiriki ambao waligawanywa katika makundi
11 kulingana na huduma wanayo itoa
Katika kundi
la mabenki, benki ya crdb ilibuka mshindi  wa kwanza kwa mwaka2013-2014 na kupata tuzo
maalumu ya uandaaji  wa taarifa bora  za fedha za mwaka iliyokabidhiwa na naibu
waziri wa fehda Adam Malima  kwa meneja
wa fedha wa benki hiyo Sosthenes Biseko ambaye akizungumzia ushindi huo amesema
ni njia mojawapo ya kuudhihirishia umma wa watanzania kuendelea kuwa na Imani nabenki.

Wafanyakazi mbalimbali wa benki ya CRDB wakiwa katika picha wakati wa makabidhiano hayo.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG