Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Wednesday, December 10, 2014

LEO KWENYE SIKU YA UHURU NIMEONGEA NA WANAFUNZI WA IRINGA UNIVERSITY..


  • Share on facebook
    Share on google_plusone_shareShare on twitterShare on linkedin
Ndugu zangu,
Leo sisi wa Kwanza Jamii/ Mjengwablog tulipata bahati ya kutembelewa na wanafunzi wa mwaka wa kwanza BA Journalism Iringa University.
Walikuja kwetu kujifunza, lakini, nasi tumejifunza pia kutoka kwao. Nilipata bahari ya kuwa na darasa nao. Mbali ya mambo mengine, niliongea juu ya umuhimu wa tafiti bora kuhusiana nambazo zinaweza kutumika na wanahabari pia.
Kwamba njia ya kuelekea kwenye tafiti bora inajengwa kwanza na hamu ya kutaka kujua jambo. Kisha unatengeneza maswali ambao tafiti yako ikusaidie kuyajibu. Ukitoka hapo unachagua njia ya kuifanya tafiti hiyo': Qualitative/Quantitative, au zote mbili.
Baada ya hapo ndipo huanza kazi ya kukusanya taarifa ( Data). Ukishakusanya taarifa, unakuwa na empiri, kwa maana ya mzigo wa taarifa unaotakiwa uchambuliwe. Kuna makapi ya kuayaacha na mchele wa kuchukua.
Ndipo baadae unapopata matokeo ya tafiti.
Na tafiti bora ni ile ambayo, matokeo yake yanaweza kupelekea kufanyika tafiti nyingine ambayo matokeo yake yanaweza kutofautiana na tafiti iliyofanyika. Nadharia hii inatokana na mwanafalsafa wa Kisayansi Karl Popper ( Falsifiability au refutability)
Nikatoa mfano, kuwa kama Taasisi ya Tahea imekuja na matokeo ya utafiti yenye kusema kuwa Iringa ni ya tatu kitaifa kwa utapia mlo, sababu za Tahea zaweza kusemwa kuwa ni kutokana na gharama za juu za pembejeo za kilimo.
Lakini, mwingine anaweza kufanya utafiti mpya akagundua, kuwa akina mama wa Iringa, ambao ndio wenye majukumu makubwa ya malezi, kwamba idadi ya akina mama hao wenye kushiriki ulevi wa pombe inaongezeka.
Hivyo, wanapoamka asubuhi, huona uvivu kuchuma mbogamboga kwa chakula cha watoto. Huona uvivu pia kupika chakula maana lazima pia waende shambani pia. Kwamba wengine hufikia hata kuwanywisha pombe watoto wao mapema asubuhi, na ukawa ndio mlo wa mtoto.
Hakika, tulikuwa na mjadala mzuri na wanafunzi wale wa Iringa University.
Maggid,
Iringa.    

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG