- Written by Tupambane Blog
- Tuma Maoni
-
Share on facebook Share on google_plusone_share Share on twitter
Wachezaji Liverpool wakishangilia ushindi
Ligi kuu ya England ambayo imendelea jumapili kwa timu sita kujitupa uwanjani katika michezo mitatu.
Katika
mechi ya kwanza Meneja wa Liverpool Brenden Rodgers alitimiza mechi yake
100 tangu aichukue usukani wa kuifundisha liverpool kwa kushuhudia timu
yake ikiisambaratisha Tottenham Hotspur kwa jumla ya magoli 3 kwa 0.
Liverpool walianza kuonja ushindi katika dakika ya 8 kwa goli lililofungwa na Raheem Sterling.
Baadae
Nahodha wa timu hiyo Steven Gerrald katika dakika 49 akafunga goli la
pili kwa mkwaju wa penalty baada ya Joe Alllen kudondoshwa kwenye
kisanduku cha 18 kwenye goli la Tottenham.
Goli la
tatu la Liverpool lilifungwa na Alberto Moreno Perez baada ya kuwatoka
mabeki wa Tottenham na kufunga goli la tatu katika dakika 60.
Hadi mechi hiyo inamalizika Tottenham 0 Liverpool 3
Nayo Aston Villa ambao waliiadhibu Hull City magoli 2 na Hull City 1.
Aston Villa ndio walioanza kufunga goli lililofungw Gabriel Agbonlahor katika dakika ya 14.
Aston villa wakaandika goli la pili ambalo lilifungwa na Andreas Weimann katika dakika ya 36.
Nao Hull City walipata goli moja la kufutia machozi lililofungwa na Nikica Jelavic.
Mechi ya
mwisho iliyomalizika usiku ilikuwa ni kati ya Leicester City na Arsenal
na matokeo ni kwamba Leicester goli 1 na Arsenal wamepata goli 1.
Kwa
matokeo hayo sasa Chelsea ndio wanaoongoza msimamo wa ligi ya England
kwa pointi 9 wakifuatiwa na Swansea iliyoshika nafasi ya pili nayo ikiwa
na pointi 9 ila ikiwa na toufuti ya magoli Aston Villa ya tatu,
Manchester City ya nne, Liverpool ya tano, Tottenham ya sita, Arsenal ya
saba na Manchester United ikishika nafasi ya kumi na nne.
No comments:
Post a Comment