Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Saturday, October 25, 2014

Diamond asalimisha magwanda polis

  • Written by  Tupambane Blog
  • Share on facebook Share on gmail Share on twitter

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul 'Diamond', amekiri kuhojiwa na polisi baada ya kukutwa na hatia ya kuvaa mavazi yanayoaminika kuwa ni sare (magwanda) ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Hata msanii huyo alidai kwamba mavazi hayo hayakuwa sare za jeshi hilo na kwamba yeye aliyanunua alipokuwa Ujerumani ingawa baada ya kuhojiwa aliyasalimisha.
Diamond alipanda jukwaani Jumamosi iliyopita katika onyesho la Fiesta jijini Dar es Salaam akiwa na mavazi hayo jambo ambalo liliibua mjadala.
Akizungumza jana Alhamisi, Diamond alikiri kupata ujumbe uliomtaka kufika Kituo cha Oysterbay, Dar es Salaam na madansa wake akiwa na nguo hizo.(T.K)
"Awali Meneja wangu alishikiliwa kwa muda na mimi nikatakiwa kufika na zile nguo nikiwa na madansa wangu ambao pia walizivaa, nilifanya hivyo na kuziacha nguo baada ya taratibu zote za kisheria kukamilika," alisema.
"Nisingeweza kukaidi amri ya dola, nilifika na yale mavazi na nikahojiwa kwa saa kadhaa. Nikaeleza kwamba yalikuwa yakifanana tu na ya jeshi na hayakuwa sare rasmi za jeshi, kikubwa nilihitaji kumaliza tatizo," alisema.
Diamond alifafanua pia kwamba si kweli kwamba alichukuliwa dhamana na Chief Kiumbe, ukweli ni kwamba alisindikizwa na mdau huyo wa sanaa kama kaka tu kutokana woga aliokuwa nao, lakini hakushikiliwa na kutakiwa kutoa dhamana yoyote.

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG