Kocha wa zamani wa Simba, Zdravko Logarusic, raia wa Croatia.
KOCHA wa zamani wa Simba, Zdravko Logarusic, raia wa Croatia, amesema amezisikia taarifa za kuyumba kwa Mbeya City na kuwaambia viongozi wa klabu hiyo, wampe nafasi ya kuinoa waone kazi.
Logarusic aliyeinoa Simba kwa nusu msimu, amesema iwapo atakipata kikosi cha Mbeya City, chenye wachezaji anaowajua vizuri, basi kila kitu kitabadilika.
Logarusic aliyeinoa Simba kwa nusu msimu, amesema iwapo atakipata kikosi cha Mbeya City, chenye wachezaji anaowajua vizuri, basi kila kitu kitabadilika.
Akizungumza kutoka kwao Croatia, Logarusic maarufu kama Loga, amesema ana uwezo wa kusababisha mabadiliko makubwa kwenye kikosi cha Mbeya City.“Kwangu naona wana wachezaji wazuri tu, kama unakumbuka nilikuwa nimependekeza Simba wasajili wachezaji zaidi ya watatu kutoka Mbeya City baada ya kuwa nimewaona.
“Kama wale au nusu yao bado wapo, nakuhakikishia mabadiliko ya haraka yatafanikiwa. Waambie viongozi Mbeya City niko tayari ili niwafanyia kazi,” alisema Loga.
Loga ni mmoja wa makocha maarufu katika ukanda wa Afrika Mashariki hasa kutokana na umaarufu alioupata akiwa na Gor Mahia ya Kenya.Aliinoa Simba kwa nusu msimu, lakini akatupiwa virago baada ya Simba kufungwa mabao 3-0 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Zesco ya Zambia.
No comments:
Post a Comment