Blogger Widgets FURSA KWA VIJANA WOTE TUPAMBANE KWA KILA NJIA ILI MRADI TUWEZE KUEPUKA HUU UMASKINI TANZANI NA AMIN KILA ATAFUTAYE KWA NIA HUPATA MAANA ATA MAANDIKO HUSEMA PENYE NIA PANA NJIA

Friday, February 6, 2015

Fwd: KILIMO CHA MBOGA MBOGA (3)- AINA YA MABOGA.


(ii) MATIKITI

Kuna aina mbili za Matikiti, Tikiti- Maji (Water Melon) na Tikiti-
Tamu (Sweet Melon). Asili yake ni Afrika na kwa sasa zao hili
linalimwa sana Afrika Magharibi na Mashariki, India, Indonesia, na
katika Visiwa vya Caribean.

Aina zilimwazo zaidi ni hizi zifuatazo;

Tomo Waston, Dixie Queen, Charleston Grey, Congo, Florida Giant. Aina
zote hizi ni Tikiti- Maji.
Ustawishaji: Zao hili hustawi toka usawa wa bahari hadi 1,000.
Huvumilia tofauti za hali ya hewa, na huhitaji unyevu wa kawaida
kutosha katika hatua za mwanzo mradi tu upungue kadri linavyokaribia
kukomaa. Unyevunyevu ukizidi sana husababisha magonjwa na kupunguza
utoaji wa maua. Pia joto kali sana hudhuru matunda.

Kupanda: Mbegu hupandwa nyakati za mvua, na matunda huvunwa nyakati
za kiangazi. Hupendelea ardhi yenye rutuba, tifutifu, na isiyotuamisha
maji. Mbolea ya takataka au samadi ndiyo ifaayo zaidi.
Mbegu hupandwa kwenye matuta au vilima vya udongo. Tia mbegu mbili
au tatu ktk shimo, baadaye ng'oa na kubakiza mche mmoja ulio na afya.
Umbali wa kupanda ni sentimeta 60 hadi 90 kati ya mimea, na sentimeta
120 hadi 180 kati ya mistari.
Ni muhimu kupalilia na kutandaza nyasi kwa kuzungushia mashina
kusudi kuzuia mizizi isidhuriwe na jua. Nyakati za ukame, umwagiliaji
ni lazima. Katika hatua fulani ya kukua, inapendekezwa kukata ncha za
mimea jambo ambalo linasababisha kutoka kwa matawi mengi pembeni
pembeni, ambayo hatimaye hubeba matunda. Matunda huwa tayari kuvunwa
baada ya majuma 12 hadi 15 tangu kupandwa.

Magonjwa: Magonjwa ya zao hili ni sawa na yale ambayo hushambulia
matango, yaani Cucumber Mosaic, Bacteria Wilt, Downy Mildew na Powdery
Mildew. Hata hivyo njia za kupigana na magonjwa hayo ni sawa na za
kwenye Matango.
Anthracnose- Ugonjwa huu hushambulia sana zao hili kuliko
unavyoshambulia mazao mengine yaliyo ktk kundi hili. Hutokea madoa
meusi kwenye matunda na sehemu zenye madoa huonekana zimebonyea.
Nyunyizia dawa ya Malathion au copper

No comments:

Post a Comment

TUPAMBANE BLOG