Waziri
huyo ambaye aliwahi kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar mara mbili
(mwaka 2000 baada ya Dk Salmin Amour kumaliza muda wake na mwaka 2010
wakati Amani Abeid Karume alipokuwa akiondoka madarakani), alisema
hatagombea tena nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015.
"Sina nia
wala dhamira ya kugombea tena urais. Mimi dhamira yangu kubwa
ilikuwa
ni kuiunganisha Zanzibar kazi ambayo Rais aliopo (Dk Ali Mohamed Shein)
ameifanya vizuri,"alisema.
Aboud
alisema sifa ya Rais ni uadilifu na kuwaunganisha Wazanzibari na
Watanzania kwa jumla, sifa ambazo zote amekuwa nazo Rais wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar Dk Shein. Hata hivyo, alisema kazi yoyote
inayofanywa na mwanadamu inakuwa na upungufu, haiwezi kuwa kamili.
"Mimi
nina uhakika matarajio ya Wazanzibari yamepata majibu katika
Rasimu hii
ya Katiba. Na ninaamini kuwa wataipokea vizuri. Lazima
tufahamu kuwa
Katiba ni mchakato," alisema.
Aboud
alisema kama kuna jambo ambalo hawakulipata katika mchakato
wa sasa wa
Katiba unaomalizika Oktoba 4 au hawakufikia mwafaka ,
kesho wanaweza
kupata nafasi ya kulizungumza.
Alipoulizwa
kero zilizopatiwa ufumbuzi katika Katiba hiyo, Aboud aliitaja
kero ya
mafuta na gesi ambapo sasa Zanzibar itakuwa na uwezo wa kushughulikia.
"Zanzibar
sasa itaweza kutunga sheria na sera zake za kushughulikia mafuta
na
gesi, lingine lilikuwa ni ushiriki wa Zanzibar katika taasisi za
kimataifa," alisema Aboud.
Alisema
Rasimu imetoa haki ya Zanzibar katika mikopo na imetoa fursa ya
kupunguzwa kwa mambo ya muungano ambayo ilikuwa ni sehemu ya kero
ya
Wazanzibari.
Ukawa kuondoka bungeni
Aboud
alisema Ukawa na wajumbe wanaotokana na CUF, kususia Bunge hilo,
hiyo
haitaathiri uendeshaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa vile bado
wana umoja.
"Hawa
walijitoa si kwa sababu hawaoni umuhimu wa Bunge la Katiba.
Walijitoa
kwa sababu waliamini suala la serikali tatu ni suala la msingi.
Sisi
tumeona mfumo wa Serikali mbili ndiyo utakaodumisha muungano,"
alisema
na kuongeza:
"Sisi
tumejali sana masilahi ya wananchi, sasa wao pengine wamejali sana
masilahi yao. Sisi tumeona kuwa mfumo wa serikali mbili ndiyo utaweka
msingi wa muungano."
Alisema pengine CUF wamejali sana faida watakazopata kutokana na mfumo
wa serikali tatu.
"Wanajua
wao kwa nini wanataka mfumo wa Serikali tatu. Lakini kwa mimi na
imani
kabisa serikali mbili ndiyo njia sahihi," alisema Aboud.
Showing posts with label ccm. Show all posts
Showing posts with label ccm. Show all posts
Thursday, July 28, 2016
MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA SEKRETARIETI NA WAFANYAKAZI WA CHAMA DODOMA MJINI DODOMA
Monday, September 29, 2014
‘Katiba itaibeba CCM Zanzibar’
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
(SMZ),
Mohamed Aboud Mohamed amesema Katiba inayopendekezwa, itaibeba
CCM katika
uchaguzi mkuu ujao visiwani humo.
Akizungumza
katika mahojiano maalumu bungeni jana, Aboud alisema katiba hiyo
itawasaidia katika kujibu kero mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwani
imejibu
asilimia 90 ya kero hizo.
"Kwa
asilimia zaidi ya 90 kero za muda mrefu za wananchi wa Zanzibar
zimejibiwa.
Kwa hiyo wananchi watajua kuwa tumeshughulika na kero zao
kwa kuzipatia
ufumbuzi,"alisema.
Aboud
alisema watakwenda kwa wananchi wa Zanzibar wakiwa kifua mbele
kufafanulia kero ambazo zimetafutiwa ufumbuzi na wajumbe wa Bunge la
Katiba, wengi wao wakitokana na CCM.
"Mimi
ninaamini kuwa wananchi wakipelekewa Rasimu ya Katiba hii
inayopendekezwa na wakaiona kuwa imekidhi matakwa yao wataiunga
mkono,"alisema Aboud katika mahojiano hayo.
Aeleza kuhusu urais 2015 (t.k)
Tuesday, September 9, 2014
NAPE ATOA DARASA KWA VIONGOZI WA CCM UINGEREZA
- Written by Tupambane Blog
- Tuma Maoni
-
Share on facebook Share on google_plusone_share Share on twitter

Katibu wa
NEC itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akizungumza na viongozi wa
mashina ya CCM Uingereza ambapo aliwaambia matawi ya CCM nje ya nchi
yawe mawakala wa kuleta mabadiliko ndani ya chama pamoja na
kuwaunganisha watanzania kujikomboa kiuchumi

Baadhi ya
viongozi wa mashina ya CCM Uingereza wakifuatilia mafunzo kutoka kwa
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye aliyekuwa akitoa somo juu ya
Wajibu wa Matawi ya CCM nje ya Nchi.

Viongozi wa mashina wakisikiliza kwa makini.(P.T)

Viongozi wa mashina ya CCM nchini Uingereza wakiandika pointi muhimu.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa mashina ya CCM nchini Uingereza .

Katibu wa
NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa kwenye picha ya pamoja na
Viongozi wa mashina ya CCM London nchini Uingereza mara baada ya kutoa
somo linalohusu Wajibu wa Matawi ya nje ya CCM katika ukumbi wa kituo
cha mafunzo Barking,London ya mashariki.

Katibu
wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye akijibu maswali mbalimbali kutoka
kwa mwandishi maarufu nchini Uingereza Ayoub Mzee mara baada ya kumaliza
kutoa semina kwa viongozi wa mashina ya CCM nchini Uingereza
Subscribe to:
Posts (Atom)