Mabingwa
watetezi wa Kombe la FA, Arsenal imefanikiwa kutinga hatua ya robo
fainali na kukomesha safari ya Middlesbrough ya kuwania taji hilo baada
ya kuirarua mabao 2-0.
Magoli ya Arsenal yalifungwa na mchezaji wake Olivier Giroud.
Arsenal,
ambayo ilimaliza ukame wa mataji uliodumu kwa miaka tisa kwa kushinda
kombe la FA msimu uliopita, inaingia katika timu nane zitakazochuana
hatua ya robo fainali ikiwa miongoni mwa timu tano za ligi kuu, mojawapo
ni Liverpool iliyokwisha kata tiketi ya kucheza hatua ya robo fainali.
Katika
michezo mingine iliyochezwa jana Jumapili, Bradford imeigaragaza
Sunderland kwa kichapo cha mabao 2-0, huku Aston Villa ikiibwaga
Leicester magoli 2-1.CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment